Ujana kweli kaa la moto. Yaani kabisa nikapanda ndege. Safari ya masaa matatu. Halafu sasa tunakaribia kutua ndege inayumba balaa, mvua inanyesha balaa, upepo unavuma hali tete hatari. Nikiangalia nje kwenye dirisha giza tupu radi zinapiga chini maji ya bahari mpaka nikawa najiuliza sasa hii ndege ikianguka nitakwenda kusema nini mbinguni jamani mimi? Ila Mungu si Athumani tukatua salama aisee. Na mjidada wa kizungu nikaukuta hapo airport unanisubiri...heka heka zote zikasahaulika
View attachment 1811839