Vitu vya kuepuka kufanya pindi unapoachwa na mpenzi wako

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
37,212
85,331
Ni raha sana kwenye mahusiano yako ukimpata mtu ambae mnapendana kwa kila hali kwani wataalmu wa masuala ya saikolojia wanasema itakuongezea siku za kuishi na kukufanya uwe mwenye furaha siku zote.

Katika hali ya kawaida maisha yanabadilika kila kukicha hivyo kuna ugumu kidogo kumpata mtu ambae mtaendana nae na kuishi kwenye ndoa au hata kwenye uchumba mpaka kuja kuona nae hapo ndiyo kwenye msingi wa ndoa yenyewe kwani mkikurupuka furaha utaisikia tuu kwa wenzio.

Kwa miaka ya hivi karibuni ndoa zinaonekana kuvunjika sana sababu kubwa ikiwa ni mabadiliko ya kiuchumi, tamaa, ulemavu wa ukubwani, ugumba huku wengine wakienda mbali hata kusiingizia umri.

Katika imani ya baadhi ya dini hurusu mke/mme kuomba talaka ya kuachana huku imani nyingine wanaamini kuwa ndoa ni kiapo ambacho kamwe hakiwezi kutenganishwa na binadamu mpaka mmoja wenu afariki dunia ndiyo upate ruksa ya kutafuta mwingine.

Anyway ushawahi kujiuliza ghafla mtu uliyenae kwenye uchumba au ndoa akatangaza kuachana na wewe kwa sababu zake binafsi na wewe ndiyo ulimtegemea kwa kila kitu kwenye maisha yako? utafanya nini?

Bila shaka ni kipindi kigumu sana katika mahusiano kwani ni muda ambao kama hautapata ushauri basi huenda ukapatwa na msongo wa mawazo au hata kupoteza uhai wako kwani takwimu kutoka Shirika la afya duniani (WHO) zinaonesha watu laki 8 duniani kote hupoteza maisha kwa msongo wa mawazo wengi wao wakiwa ni kuanzia miaka 15-29 na kesi nyingi hutokana na mahusiano.

Kama umepatwa na matatizo hayo ya kuachwa au ndiyo penzi lako lipo njia panda basi ni muda wa kujiandaa kisaikolojia ili usijekupatwa na majanga kwani watu wengi baada ya kuachwa na wapenzi wao huishia pabaya kutokana na kutojiandaa.

INAPO TOKEA UMEACHWA:-

1. Epuka kulipiza kisasi,
mwachie Mungu na kubali yote yaliyotokea na kuruhusu yapite. Unapoachwa ni kama adhabu fulani hivi kwani akilini mwako utajiona kama huna thamani na kuanza kujitoa kasoro kwa kujiuliza maswali kibao mfano sikumridhisha, sina mvuto na mambo mengi utafikiria.

Kipindi hiki unashauriwa kufunga mlango kabisa kwa ex wako tena ikubali hali hiyo ikupite ili ukaribishe maisha mengine ya furaha huku ukimuomba Mungu sana.

31313726523_773c8b4388_k.jpg

2. Epuka kusikiliza nyimbo za huzuni au kubembeleza.

Baada ya kupigwa chini na mpenzi wako, epuka kusikiliza nyimbo za huzuni au mapenzi zenye kubembeleza hizi zitakufanya ufikirie majanga yaliyokukuta badala yake sikiliza nyimbo za kufurahisha zenye kuchezeka na zenye kukufanya ujione wewe ni mshindi muda wote na mwenye furaha.

images-7.jpg

3. Epuka kuita mahusiano yako ni magumu (Complicated)


Watu wengi hususani wanawake wanapoulizwa na wanaume kuhusu status zao za mahusiano asilimia kubwa majibu yao nina mtu lakini tumezinguana, majibu ambayo huwafanya waumie kisaikolojia hii ni kutokana na kujiona kuwa umri unaenda na bado hawajapata mtu wa kuishi nae.

Hiki kitu huwapata wanawake kwani huwa ni wagumu sana kuruhusu mioyo yao kusahau mapema vitu kutoka kwa ex wako nakumbuka mwaka 2014 Amber Rose alivyomwagana na WizKhalifa alikuwa akilalama kila siku mitandaoni akiamini hiyo itampunguzia machungu kumbe ndiyo kwanza ilimzidishia machungu.

BzTU5vECYAA1yLp.jpg

4. Epuka kumsema vibaya ulieachana naye


Mwenza wako anapoamua kuondoka na kwenda kwa mwingine usiwaambie marafiki zako kuhusu mabaya yake kwani itakufanya uonekane mtu mbaya bila wewe kujua, utaharibu mwonekano wako, na tabia yako, ukisema vibaya kuhusu yeye, pia na wewe utaonekana mkosaji, maana wakosaji ndio huongea mabaya kwa wale ambao hawakufanikiwa.

03-secrets-of-happily-married-couples-friends.jpg

5. Epuka kutuma meseji za bahati mbaya,au kumfuatilia ex wako kwenye mitandao ya kijamii


Epuka kutuma meseji za kujitekenya mwenyewe SMS kama oooooh!! samahani, pole, nimekosea. habari yako, sikuwa namaanisha kukutumia wewe. yote ya nini? punguza kuongea nae ikibidi acha hadi akutafute maana kitendo cha kummtafuta utakuwa unaongeza chumvi kwenye jeraha lako mwenyewe.

Kwasasa kutokana na utandawazi ni vyema ukampa tofali (Block) hii itakufanya umtoe kichwani kirahisi kwani kitendo cha kumfuatilia mitandaoni kitakuumiza zaidi hebu fikiria wewe usiku mzima hujalala kutokana na maumivu ya kuachwa halafu asubuhi unaingia tuu Instagram unakutana na picha ya ex wako kaposti picha ya Mwanamke/Mwanaume mzuri halafu kaweka emoji ya vikopa kopa hapo lazima urudi kitandani uendelee kulala.

shutterstock_222935632.jpg

6. Epuka kujibadilisha mwonekano wako

Hii inawahusu sana wanawake kwani hao ndiyo wahanga wakubwa kwa hili, Wanawake wengi wakishaachika huanza kujibadilisha muonekano kwa kuamini kuwa muonekano wao wa zamani haukuwa mzuri ndiyo maana waliachika.

Wengi hubadili mavazi,ngozi, Makalio kuweka tatoo nk. kwa lengo la kuwavutia wanaume bila kufikiria madhara yake, mwanamke usidanganyike na chochote kile kufanya hivyo ni kupoteza muda tuu focus kwa kufanya mambo ya maendeleo kama biashara na ujasiriamali kwa maendeleo yako ya baadae.

Vera-Sidika-before-after-IG.jpg

7. Usikumbuke yaliopita mkiwa pamoja


Tafuta kitu cha kufanya ili kukuweka bize muda wote, wakati mwingine soma vitabu vya namna ya kufanya ili kupata maendeleo,Angalia tamthilia mbalimbali ,isipokuwa za mapenzi achana nazo. tafuta marafiki wazuri wa kutoka nao na kufurahi pamoja. usikumbuke ya nyuma, jinsi mlikuwa mnafanyaje, labda sasa anafanyaje na mwingine, achana na hayo mawazo.

Hayatakusaidia badala yake utaumia. ukikaa muda wa kutosha fungua akili yako kwa ajili ya mambo mengine yanayostahili maisha yako. lakini ukirudisha mawazo ya nyuma sio tu utaumia bali hata wale wanaokuzunguka watashindwa kukusaidia.

woman_onlineshopping.jpg

8. Usianzishe mahusiano mengine kwa kukurupuka

Watu wengi wakiachika kwenye mahusiano basi hukimbilia kutafuta chaka jipya ili kumuonesha ex wake kuwa na yeye anapendwa kumbe hajui hata huyo aliyempata kwa muda mfupi watadumu nae kwa muda mfupi na kujikuta akiachwa kila uchwao.

waswahili wanasema ukiwa na furaha sana usichukue maamuzi na hata ukiwa na hudhuni usifanye hivyo kwani busara hutoe kwa wakati cha kufanya tulia muombe Mungu hayo mengine utafanikiwa tuu.

Natumaini kwa wewe ambaye bado unaugulia maumivu ya kuachwa ukizingatia haya utakuwa umepata mwanga wapi kwa kuanzia na kurudisha furaha na tabasam iliyokuwa imepotea.

new-relationship-advice-to-have-a-perfect-start.jpg


Godfrey Mgallah
 
Ushauri mzuri kaka. Na pia nataka kuongezea kuwa, aliekuacha kwa matusi na dharau, usimlipize kisasi. Hata kama ukisikia kuwa huko nje anakusema vibaya, usilipe kisasi.

Kulipa kisas hakuta kusaidia zaid ya kukupotezea muda.
The best way ni kukata mawasiliano kabisa na ex wa aina hiyo, mawasiliano ya simu au mitandao ya kijamii.
Jipe muda, kama unalia lia, vyovyote vile acha mwili wako u react sababu ya maumiv uliyopata. Baada ya muda utaona unaanza kuona kawaida, hali ya maumiv inapungua na kuondoka kabisa. Mwishowe unapona na kuendelea na maisha.
 
Safi sana,maelekezo mazuri kweli kweli,hiyo namba 8 wanawake wengi imewagharimu sana,kwani kwa wanaume waonjaji inakuwa kama ni loophole kwao...
 
Safi sana,maelekezo mazuri kweli kweli,hiyo namba 8 wanawake wengi imewagharimu sana,kwani kwa wanaume waonjaji inakuwa kama ni loophole kwao...
Absolutely comrade....
Hii binafsu nimeishuhudia enzi za ujana wangu
 
Back
Top Bottom