Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,366
- 2,796
Hivi majuzi mamlaka zilifanikiwa kufunga akaunti Zaidi ya 200 za mitandao ya kijamii kwa kutangaza kuuza dawa za kulevya, silaha, picha , bidhaa mbalimbali nk.
Ukiwa Dubai jihadhari sana na mambo yafuatayo 👇
🛡️ Kutuma picha za watu bila wao kujua
Ikitokea uko Jiji la Dubai jihadhari sana kupiga piga picha ovyo maana unaweza kwenda jela kwa kumpiga mtu picha bila yeye kujua au umetuma kwenye mitandao ya kijamii ukikamatwa faini ya dirham 150,000
🛡️ Ikiwa umeshare taarifa za mtu mtandao
Kama unatabia ya kushare taarifa za watu mitandaoni basi jihadhari maana Dubai unaweza pelekwa jela au ukalipishwa faini dirham 1,500,000 kwa kusambaza taarifa nyeti za kampuni au mtu Fulani.
🛡️ Ikiwa umetuma post mbaya au za kuchukiza
Ikitokea umeamua kumchafua mtu mtandao kwa kutuma post kuhusu mtu Fulani juu ya tabia zake mbaya au matendo machafu au kitu chochote cha kuchukiza toka kwa mtu, kampuni au muajiliwa wako basi unaweza pigwa faini ya dirham 250,000/=.
🛡️ Utakiwi kutumia program Haram za kupiga simu
Upaswi kutumia program Haram za kupiga simu kuanzia Whatsapp au Skype zimezuiliwa unaweza lipishwa dirham 250,000 ni lazima utumie program ambayo ni salama kama vile botim badala ya Whatsapp, Skype nk.
🛡️ Upaswi kupost kitu kinacho chafua dini ya uislamu
Jihadhari sana ukiwa nchi za watu kupost vitu vinavyo kashfu dini za watu unaweza jikuta jela au kupigwa faini bila kutarajia pia post zote kuhusu picha za ngono , uchi au ulevi faini yake inaweza mpaka kufikia dirham 500,000
Pamoja na makosa mingine ya kimtandao kama vile kuchochea chuki , ubaguzi wa Rangi au ghasia , kuvunja sheria Za nchi za kifalme za kiarabu au kiongozi pamoja na kufanya michango bila leseni.
Jihadhari sana ukiwa unatembelea nchi za watu kuwa makini vipi ulikua unajua hii au ndo tunakujuza?
Usisahau kutembelea page Yetu ya Instagram Login • Instagram
#dubai #safari #dubailifestyle #TAMADUNI #Fahamu #fahamuzaidi #safarilife