Vitu visivyolipiwa na kodi bandarini/posta

Vitu visivyolipiwa na kodi bandarini/posta

Chief Lugina

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2011
Posts
286
Reaction score
77
Habari wakuu!
kuna taarifa kuwa kuna baadhi ya vifaa ukivinunua nje ya nchi huwa havina kodi. Pia kuna baadhi ya vitu hupokelewa POSTA na siyo Bandarini, naomba kujuzwa baadhi ya vitu vifuatavyo au zaidi kama vinalipiwa kodi na vinapitia wapi? bandarini/ posta.

1.LAPTOPS/SIMU
2.VIFAA VYA MICHEZO
3.VITABU
4.
5
 
Habari wakuu!
kuna taarifa kuwa kuna baadhi ya vifaa ukivinunua nje ya nchi huwa havina kodi. Pia kuna baadhi ya vitu hupokelewa POSTA na siyo Bandarini, naomba kujuzwa baadhi ya vitu vifuatavyo au zaidi kama vinalipiwa kodi na vinapitia wapi? bandarini/ posta.

1.LAPTOPS/SIMU
2.VIFAA VYA MICHEZO
3.VITABU
4.
5

Inategemeana na njia aliyotumia mtumaji kutuma hivyo vitu. Kama katuma Posta ,utapokelea posta. Kama katuma kwa kampuni binafsi kama DHL,UPS, FEDEX au TNT, unapokelea ofisi za kampuni husika bila kujali kuwa bidhaa zinapita melini au angani kwenye ndege. Kwa posta, bidhaa nyingi ndogo ndogo huwa hazilipwi kodi. Kwa DHL, bidhaa lazima zipite kwenye ukaguzi wa maofisa wa forodha kuona kama zinastahili kulipiwa kodi. kama zinastahili, mawakala wa kampuni husika hushughulikia taratibu zote za clearance ikiwemo na kulipa kodi baada ya wewe kuwapatia TIN yako. Mziigo ukifika unajulishwa na kwenda kulipa gharama za clearance ikiwemo kodi kama ni stahili.
Kama bidhaa zilitumwa bila kutumia agent yeyote wa Clearing & forwarding, utalazimika kufuatilia mzigo wako wewe mwenyewe mara tu baada ya kuingia nchini ili ukamilishe taratibu zinazotakiwa, ukiwa na documents za mzigo.
Kuwa na uhakika wa kupokea mzigo (ingawaje si kwa 100%), mwambie mtumaji ausajili mzigo au atumie EMS (ni ghali na haraka) au atumie makampuni binafsi ya usafirishaji tajwa hapo juu(ghali zaidi na haraka zaidi).
Hii ni kwa mujibu wa wwerewa wangu.
 
Back
Top Bottom