Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 218
- 297
Salaam nyingi sana kwenu wadau wa Jukwaa hili linalotumia ubongo mwingi sana huku nguvu za Mwili zikiwa kisoda.
Katika mambo ambayo nimewahi kuyafikiria na sikuwahi kupata majibu au kukaribiana na majibu ni kuhusu vitu vinavyofikirisha akili sana. Kwa upeo wangu vitu hivi nadhani havina mwanzo wala mwisho.
1. Ulimwengu, hapa namaanisha sayari zote, magimba yote, ombwe, nyota, jua na vyote ambavyo vipo katika pande zote za ulimwengu. Kwa upande wa Dunia utazunguka lakini utarudi ulipoanzia. Kwa upande wa nje ya Dunia ukiondoka hakuna mwisho ni kwa upande wowote utakaoelekea kwasababu ukisema kuna mwisho kinachothibitisha mwisho ni kitu gani?
2. Suala la Mungu. Mungu tunaambiwa hakuanza wala hana mwisho. Hii maana yake hakuna kilichosababisha uwepo wa Mungu, yeye alijikuta tu yupo.
Tafakuri za mambo haya yote huenda ni ngumu Kutokana na upeo mdogo wenye ukomo yaani ni sawa na kuku amtafakari anayemfuga kwamba alitokea wapi na mwisho wake ni upi, kamwe hatapata majibu.
Kuna stori Moja kwenye maandiko ya kihistoria ndani ya Kanisa Katoliki kuhusu Mtakatifu Agustino, kwamba alipita ufukweni mwa bahari akiwa amejaa mawazo mengi kumtafakari Mungu hasa mwanzo wake na mwisho wake, akakutana na mtoto mmoja anachota maji kwa kifuniko kidogo mithili ya kisoda kutoka baharini na kujaza kwenye kishimo alichochimba pembeni ya bahari, Mtakatifu Agustino akamuuliza, we mtoto unafanya nini? Mtoto akajibu, nataka kuhamisha maji ya baharini yote yaingie kwenye kishimo hiki kidogo, Mtakatifu Agustino akamwambia yule mtoto, we mjinga sana bahari ilivyo kubwa hivyo itahamiaje kwenye kishimo kidogo hicho! Naye mtoto akajibu, na wewe ulivyo na akili ndogo utaweza kumtafakari Mungu alivyo mkubwa na ukapata majibu?
Pamoja na yote naomba tushirikishane pengine mtu amewahi kusoma tafiti mbalimbali kuhusu ukomo au mwisho wa mambo niliyoyazungumzia.