Hivi Ladies kuolewa maana yake ni nini?
Mimi kuna vijambo vinanichosha mpaka imekuwa kero na kuona kama ndoa ni ngumu. Ni takribani mwaka mmoja na nusu sasa mme wangu kazi iliisha yupo nyumbani huku akiangaika kutafuta kazi sehemu zingine .
Hiyo sio big deal mie nafanya kazi thanks God kamshahara kangu kanasaidia kucover matatizo yote ya nyumbani ingawa sio kama tukiwa wawili. Kinachonichosha sana ni ratiba ya mme wangu.
Mimi nina watoto wawili wa kiume mmoja 5 years na mwingine 9 month. Mme hata mtoto akiwa analia eti yeye hawezi kumbembeleza anamwangalia tu ukimuuliza anasema yeye amfanyeje wakati hana maziwa ya kumnyonyosha, mimi hapa usiku silali mtoto anasumbua asubuhi kuamkia kazini, jioni kufika kumwangalia mtoto na kuandaa maakuli ya familia.
Nina binti anaenisaidia nikiwa kazini. Lakini mme anaamka saa nne kitanda hagusi kutandika mpaka nitoke kazini nakikuta hivyo hata net haijatolewa kutandika ndio basi tena pia hata akivua nguo za ndani atarundika hapo nije kufua mie.
Anapiga mswaki na kukaa kwenye kochi kusubiri atengenezewe chai na apelekewe, atabadilisha chanel mpaka lunch atakula atabadilisha Channel zake baadae anawasha gari kwenda kutembea.
Saa mbili au saa tatu atarudi atakula atakamata tena remote mpaka saa sita ataingia kulala na ukali sasa kitu kidogo tu manung'uniko.
Hivi jamani wanaume mkioa kazi yenu huwa inakuwa kutoa matumizi, kula na kulala tu?
Hakuna mnachoweza kusaidia?
Ladies hivi wote mko kwenye hali hii?