Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,041
- 1,294
Mara nyingi tunapokua, tunapitia changamoto, mafanikio, au kupata maarifa mapya, mtazamo wetu kuhusu maisha huanza kubadilika.
Hali hii hufanya tuone vitu kwa jicho tofauti, hata kama hivyo vitu havijabadilika kabisa. Mlima tuliozoea kuuona kila siku ukiwa kama kivuli kwenye maisha yetu, ghafla unaweza kuonekana wa kuvutia sana tukianza kuuangalia upya.
Hali hii inathibitisha kwamba vitu vingine duniani havibadiliki ni sisi tunaobadilika. Ni fikra zetu, hisia zetu, na upeo wetu wa kuelewa ndivyo vinavyopanuka.
Mtu ambaye hapo awali alionekana wa kawaida, anaweza ghafla kuonekana wa thamani zaidi pale tunapoanza kuelewa undani wake.
Maeneo yaliyokuwa ya kawaida kwetu yanaweza kuonekana ya kipekee tukiyatembelea tena tukiwa na mtazamo tofauti.
Kwa hiyo, badala ya kulaumu hali au mazingira, mara nyingine tujiulize: je, tatizo ni vitu vyenyewe, au ni namna yangu ya kuviona? Mara nyingi, jibu linapatikana ndani yetu. Kwani mabadiliko ya kweli huanza na sisi wenyewe.
Abuuabdillah ✍️