Vitu ambavyo vingefanyika kama Mungu angekuwepo kweli

Kadri mapinduzi ya Sayansi yanavyoendelea, taratibu watu wataacha kuamini. Japo itachukua muda mrefu
Ni kweli,,watu wanao muabudu mungu wanapungua taratibu kadiri siku zinavyokwenda ila bado ni suala gumu kuondoa imani hii katika mioyo ya waamini wengi kwa sasa..!
 
Mungu ananiongelesha kwa sauti yake kila wakati. Naogopa hukumu zake na moto wake. Naisikia sauti ya mwanaume. Nimekua nikiandika hapa mkasema ni neurological issue.
Kwahiyo Sauti hiyo ndo mungu?
 
Ni kweli,,watu wanao muabudu mungu wanapungua taratibu kadiri siku zinavyokwenda ila bado ni suala gumu kuondoa imani hii katika mioyo ya waamini wengi kwa sasa..!
Ni kweli. Ila taratibu itawezekana hasa vizazi vijavyo. Kikubwa ninachotaka tuwe nacho sisi. Hasa sisi ngozi nyeusi, ni uwezo wa akidadisi
 
Endelea kutumia akili kidogo sana kutafakar haya-vipi kungekuwa ni miti tuu, vipi kungekuwa ni bahar tuu, vipi kungekuwa ni wanaume tuu au vipi kungekuwa ni wanyama wa kuliwa tuu,,
Japo tuna bahari tuna hitaji nchi kavu ili watu kuwa na machaguo ya njia, kadhalika wanaume tunahitaji wanawake ili upatikane utofautishaji (uelewa) wa jinsia, kadhalika tungekuwa na misitu tu bila kuwa na majangwa na pia tunahitaji mboga za majani pindi tunapo ona au hisi hatuhitaji nyama, swali je unaweza ajili walimu shuleni kisha usiwape majukumu kuwa wanahitajika kufundisha wanafunzi???? Na hakika utasema hapana... Ikiwa watahitajika kufundisha utatakiw uwape mtaal wa kufundishia na pia ukaongeza kwa kuwambia muda fulani mtoto wawe wamefika hatua fulani.
Hivyo basi imiwa iko hivyo basi ukiwa umeumbwa basi unatakiwa kujua lengo la alie kuumba ww ni nini??(mie najua)
Kwa kumalizia Lazima kuwe na heri na shari na wataalam wa sheria wasema hii kavunja sheria na hii ./
 
Okay tufanye huyo mungu yupo. Tena yupo kwa kutizama vitu vilivyopo. Yaani ni kwamba imani yetu inasema hakuna chenye uwezo wa kutokea bila kuwekwa. Sasa mimi na wewe nataka tujiulize kwa pamoja. Hivi kama mungu yupo basi Kuna kitu kilichomuweka? Maana sisi tunaamini kila kilichopo kimewekwa
Akili ya mwanadamu siku zote huwa inakikomo,atajaribu kutafuta jibu lakini mwisho wa siku atasimama ktk mstariwake wa kuamini na kusema ukitaka utaamini usipotaka basi! Wana ujamaa waliposema kuwa Mungu hakuna na mwanadamu katokana na mada na walipoulizwa nini asili ya mada? wakasema mada ni ya tangu na tangu mpaka leo hii hakuna jibu. Mtoa mada anafikra za kikomunisti ambazo ni out of date na hazina tija duniani na wala hakuna kizazi kitakachokuja kuzisapoti. Wazazi wa kiislamu na kikristo wanazidi kuwasomesha dini vizazi vyao.

If we ordered to choose good from bad, we choose good if we ordered to choose right and wrong ,we choose right.
 
Kila kitu kipo kutokana na mazingira mkuu. Hebu jiulize swali moja tu kubwa. Hivi kwenye uumbaji mungu aliumba sayari zote au aliiumba dunia tu? Alafu naomba nikushauri kitu. Penda sana kuwa mdadisi. Itakusaidia
Hamna unachoweza kudadis zaid ya kilichokuwepo!! Huwez kudadis zaid kwan wewe hukuzaliwa wakat wa kuumbwa ulimwengu
 
Vitu ambavyo vingefanyika kama mungu angekuwepo kweli;

1. Shetani asingekuwepo
2. Watu wote wangekua sawa
3. Dini zisingekuwepo. Hata kama zingekuwepo basi ingekua moja tu
4. Viumbe hai vyote vingeabudu.
5. Watu wangejua uwepo wake pale wanapozaliwa tu. Yaani isingekua ni taarifa iliyobebwa na watu fulani kuwaletea wengine.
6. Watu wasingekufa au kama wangekufa, basi kungekua na umri maalum wa kifo
7. Kungekua hakuna kazi nyingine zaidi ya kuabudu na kutukuza uwezo wake
___________________________

1. Shetani asingekuwepo

Hiki ndo kitu cha kwanza ambacho kingefanyika kama mungu angekuwepo kweli. Unajua kwanini nasema hivi? Kwasababu uwepo wa shetani kwenye ufalme wa mungu, una mashaka makubwa. Hivi ulishawahi kujiuliza, ulikua mpango wa nani kuwepo kwa shetani? Je, ni mpango wa mungu au ni kufeli kwa mungu?

Kama ulikua ni mpango wa mungu, sasa kwanini vitabu vimuone shetani ni muasi?

Na kama ilikua ni kufeli kwa mungu, basi huyu mungu hana nguvu kama tunavyoaminishwa

2. *Watu wote wangekua sawa*
Hii ni sababu kubwa sana. Kama mungu anayetajwa, angekuwepo kweli. Basi binadamu wote wangekua sawa. Kusingekua na matabaka wala kusingekua na utofauti wowote. Maana angewaumba watu kwa kusudi moja.

3. *Dini zisingekuwepo*. *Hata kama zingekuwepo basi ingekua moja tu*
Kwanini nasema hivyo. Kwasababu hizi dini zilizopo sasa zinapingana. Na ukiangalia utagundua wanaabudu miungu tofauti. Kwa mfano. Waislam wana mungu wao wanamuita _allah_. Huyu mungu ni tofauti kabisa na mungu wa wakristo anayeitwa _jehova_. Hata ukiangalia historia zao, utagundua hawa ni miungu wawili tofauti.

4. *Viumbe hai vyote vingeabudu*
Hili halina ubishi. Kama mungu angekuwepo kweli basi Viumbe vyote alivyoviumba yeye vingehudhuria ibada za kumtukuza maana vimepewa uhai kama alio nao mwanadamu

5. *Watu wangejua uwepo wake pale tu wanapozaliwa*
Hii Ina maana kwamba. Kama kweli mungu angekuwepo na ndiye aliyeumba kila kitu, kusingekua na haja ya watu kusafiri kutoka mataifa ya mbali eti waje watuambie kuwa Kuna kitu kilituumba na ndo kilifanya kila kitu. Pale pindi mtoto anapozaliwa, angekua na uwezo wa kutambua kuwa kilichomleta ni nini na amekuja kufanya nini. Kama ilivyo kwa anapo tafuta ziwa la mama yake

6. *Kusingekuwepo na kifo*
Kama Lengo la kumuumba mwanadamu lilikua ni kumuabudu mungu na kumtukuza, basi kifo kisingekuwepo. Kwanini nasema hivyo? Kwasababu uumbwaji wa dunia haukua wa majaribio

7. *Kungekua hakuna kazi nyingine zaidi ya kuabudu*
Hili lipo wazi kwa wale wenye uwezo wa kutafakari. Ukisoma kwenye bible juu ya uwezo wa mungu, utaogopa. Asingeshindwa kuondoa njaa na kiu kwenye mwili wa mwanadamu kama Lengo lake lilikua ni kuabudiwa.
Umetumia neno "kama angekuwepo" kwa maana kuwa hayupo na ndiyo maana umeorodhesha vitu ambavyo vingefanyika endapo angekuwepo. Sasa mie mkuu ningependa unieleza vitu vinavyoonesha kuwa hakuna uwepo wa mungu,kwa sababu kama mungu yupo basi hayo mambo yako uliyoyaeleza yatakuwa hayana maana.
 
Umetumia neno "kama angekuwepo" kwa maana kuwa hayupo na ndiyo maana umeorodhesha vitu ambavyo vingefanyika endapo angekuwepo. Sasa mie mkuu ningependa unieleza vitu vinavyoonesha kuwa hakuna uwepo wa mungu,kwa sababu kama mungu yupo basi hayo mambo yako uliyoyaeleza yatakuwa hayana maana.
Wewe unamuamini mungu kupitia dini gani mkuu?
 
Unakubaliana na mimi kwamba biblia unayotumia wewe iliandikwa na ancient philosophers?
N.B usibishe kama hujui just omba ueleweshwe
Naomba nikuulize swali mkuu kama wewe ni msomaji wa biblia. Hivi mwanadamu aliumbwa siku ya ngapi?
 
Back
Top Bottom