nusuhela
JF-Expert Member
- Jan 26, 2014
- 5,818
- 7,106
Vitu ambavyo vingefanyika kama mungu angekuwepo kweli;
1. Shetani asingekuwepo
2. Watu wote wangekua sawa
3. Dini zisingekuwepo. Hata kama zingekuwepo basi ingekua moja tu
4. Viumbe hai vyote vingeabudu.
5. Watu wangejua uwepo wake pale wanapozaliwa tu. Yaani isingekua ni taarifa iliyobebwa na watu fulani kuwaletea wengine.
6. Watu wasingekufa au kama wangekufa, basi kungekua na umri maalum wa kifo
7. Kungekua hakuna kazi nyingine zaidi ya kuabudu na kutukuza uwezo wake
___________________________
1. Shetani asingekuwepo
Hiki ndo kitu cha kwanza ambacho kingefanyika kama mungu angekuwepo kweli. Unajua kwanini nasema hivi? Kwasababu uwepo wa shetani kwenye ufalme wa mungu, una mashaka makubwa. Hivi ulishawahi kujiuliza, ulikua mpango wa nani kuwepo kwa shetani? Je, ni mpango wa mungu au ni kufeli kwa mungu?
Kama ulikua ni mpango wa mungu, sasa kwanini vitabu vimuone shetani ni muasi?
Na kama ilikua ni kufeli kwa mungu, basi huyu mungu hana nguvu kama tunavyoaminishwa
2. *Watu wote wangekua sawa*
Hii ni sababu kubwa sana. Kama mungu anayetajwa, angekuwepo kweli. Basi binadamu wote wangekua sawa. Kusingekua na matabaka wala kusingekua na utofauti wowote. Maana angewaumba watu kwa kusudi moja.
3. *Dini zisingekuwepo*. *Hata kama zingekuwepo basi ingekua moja tu*
Kwanini nasema hivyo. Kwasababu hizi dini zilizopo sasa zinapingana. Na ukiangalia utagundua wanaabudu miungu tofauti. Kwa mfano. Waislam wana mungu wao wanamuita _allah_. Huyu mungu ni tofauti kabisa na mungu wa wakristo anayeitwa _jehova_. Hata ukiangalia historia zao, utagundua hawa ni miungu wawili tofauti.
4. *Viumbe hai vyote vingeabudu*
Hili halina ubishi. Kama mungu angekuwepo kweli basi Viumbe vyote alivyoviumba yeye vingehudhuria ibada za kumtukuza maana vimepewa uhai kama alio nao mwanadamu
5. *Watu wangejua uwepo wake pale tu wanapozaliwa*
Hii Ina maana kwamba. Kama kweli mungu angekuwepo na ndiye aliyeumba kila kitu, kusingekua na haja ya watu kusafiri kutoka mataifa ya mbali eti waje watuambie kuwa Kuna kitu kilituumba na ndo kilifanya kila kitu. Pale pindi mtoto anapozaliwa, angekua na uwezo wa kutambua kuwa kilichomleta ni nini na amekuja kufanya nini. Kama ilivyo kwa anapo tafuta ziwa la mama yake
6. *Kusingekuwepo na kifo*
Kama Lengo la kumuumba mwanadamu lilikua ni kumuabudu mungu na kumtukuza, basi kifo kisingekuwepo. Kwanini nasema hivyo? Kwasababu uumbwaji wa dunia haukua wa majaribio
7. *Kungekua hakuna kazi nyingine zaidi ya kuabudu*
Hili lipo wazi kwa wale wenye uwezo wa kutafakari. Ukisoma kwenye bible juu ya uwezo wa mungu, utaogopa. Asingeshindwa kuondoa njaa na kiu kwenye mwili wa mwanadamu kama Lengo lake lilikua ni kuabudiwa.