Vitu ambavyo vingefanyika kama Mungu angekuwepo kweli

Mkuu hana kama hana huruma pumzi unalipia beigani mwenzetu?
yeye huyo Mungu aliyetuumba si ana wajibu wa kutupa pumzi ili tuishi? alipaswa atunyime tuilipie? kutupa pumzi sio favor mkuu, kwa kuwa ameumba viumbe hai ni sharti avipe pumzi ili viwepo, ni kama wewe unapopanda mimea ni sharti uipe maji ili iwepo na hiyo sio favor
 
Wakati ukulia na kusaga meno ndio utamkiri kristo, wakati huo atashuka na mawingu na kila jicho litamuona na ulimi utakiri, ndio utaamini kwamba Niko ambaye Niko yu! Hai,,
Kwahiyo kumbe ni wakristo tu ndo watakaoenda mbinguni?
 
Innalillah wainailah rajiun,EE MWENYEZI MUNGU tunakuomba utusamehe waja wako,walikuwepo wakina firauni walipinga na kutoa kejeli za kila namna mwisho wa siku ukaonesha utukufu wako,tunakuomba umdhihirishie mja wako huyu juu ya uwepo wako.
Utasubiri sana aisee
 
  • Thanks
Reactions: lsn
Sawa mkuu. Hivi, by the way how can you validate the existence of your grand grand parents some decades back? Je unaamini kwamba walikuwepo? Na kama unaamini kuwa walikuwepo huku hukuwahi kuwaona (mfano babu yako wa pili au wa tatu) ni kipi kinachokufanya uamini kuwa walikuwepo?
Ni kwasababu bado watu wanazaliana. Yaani kuna hatua za vyeo kwenye uzazi na vinaonekana
 
Mtoa mada namuona kama hayawani maana mawazo yake ni kama ya hayawani...

Discuss...
 
Mtoa mada namuona kama hayawani maana mawazo yake ni kama ya hayawani...

Discuss...
Wewe ndiye hayawani unaaminije kuwa huyo anayeitwa baba yako kweli ndiye aliyekuzaa , una uhakika gani? Is there a possibility that your mother cheated? Wanawake huwa wanadanganya ? Unaamini?
 
Vitu vyote tunavyovisikia na kuviona ni tafsiri ya akili ya mwanadamu.
Hata Mungu ni tafsiri ya akili ya mwanadamu. Ndio maana maelezo kuhusu Mungu yanafanana sana na sifa alizonazo binadamu isopokuwa miujiza.
 
Safi sana mkuu. Mm huwa napenda sana kukutana na watu wenye kutumia ubongo wao kufikiria. Siwapendi wale wanaolishwa vitu wakavikariri na kuvitumia. Kuna kundi nimelianzisha whatsap kwaajili ya wasio amini uwepo wa mungu. Kama vipi nitumie namba niku add ili tuwe pamoja kwenye hizi harakati za kuvikomboa vizazi vijavyo
Ni add mwanangu 0754828082
 
Vitu ambavyo vingefanyika kama mungu angekuwepo kweli;

1. Shetani asingekuwepo
2. Watu wote wangekua sawa
3. Dini zisingekuwepo. Hata kama zingekuwepo basi ingekua moja tu
4. Viumbe hai vyote vingeabudu.
5. Watu wangejua uwepo wake pale wanapozaliwa tu. Yaani isingekua ni taarifa iliyobebwa na watu fulani kuwaletea wengine.
6. Watu wasingekufa au kama wangekufa, basi kungekua na umri maalum wa kifo
7. Kungekua hakuna kazi nyingine zaidi ya kuabudu na kutukuza uwezo wake
___________________________

1. Shetani asingekuwepo

Hiki ndo kitu cha kwanza ambacho kingefanyika kama mungu angekuwepo kweli. Unajua kwanini nasema hivi? Kwasababu uwepo wa shetani kwenye ufalme wa mungu, una mashaka makubwa. Hivi ulishawahi kujiuliza, ulikua mpango wa nani kuwepo kwa shetani? Je, ni mpango wa mungu au ni kufeli kwa mungu?

Kama ulikua ni mpango wa mungu, sasa kwanini vitabu vimuone shetani ni muasi?

Na kama ilikua ni kufeli kwa mungu, basi huyu mungu hana nguvu kama tunavyoaminishwa

2. *Watu wote wangekua sawa*
Hii ni sababu kubwa sana. Kama mungu anayetajwa, angekuwepo kweli. Basi binadamu wote wangekua sawa. Kusingekua na matabaka wala kusingekua na utofauti wowote. Maana angewaumba watu kwa kusudi moja.

3. *Dini zisingekuwepo*. *Hata kama zingekuwepo basi ingekua moja tu*
Kwanini nasema hivyo. Kwasababu hizi dini zilizopo sasa zinapingana. Na ukiangalia utagundua wanaabudu miungu tofauti. Kwa mfano. Waislam wana mungu wao wanamuita _allah_. Huyu mungu ni tofauti kabisa na mungu wa wakristo anayeitwa _jehova_. Hata ukiangalia historia zao, utagundua hawa ni miungu wawili tofauti.

4. *Viumbe hai vyote vingeabudu*
Hili halina ubishi. Kama mungu angekuwepo kweli basi Viumbe vyote alivyoviumba yeye vingehudhuria ibada za kumtukuza maana vimepewa uhai kama alio nao mwanadamu

5. *Watu wangejua uwepo wake pale tu wanapozaliwa*
Hii Ina maana kwamba. Kama kweli mungu angekuwepo na ndiye aliyeumba kila kitu, kusingekua na haja ya watu kusafiri kutoka mataifa ya mbali eti waje watuambie kuwa Kuna kitu kilituumba na ndo kilifanya kila kitu. Pale pindi mtoto anapozaliwa, angekua na uwezo wa kutambua kuwa kilichomleta ni nini na amekuja kufanya nini. Kama ilivyo kwa anapo tafuta ziwa la mama yake

6. *Kusingekuwepo na kifo*
Kama Lengo la kumuumba mwanadamu lilikua ni kumuabudu mungu na kumtukuza, basi kifo kisingekuwepo. Kwanini nasema hivyo? Kwasababu uumbwaji wa dunia haukua wa majaribio

7. *Kungekua hakuna kazi nyingine zaidi ya kuabudu*
Hili lipo wazi kwa wale wenye uwezo wa kutafakari. Ukisoma kwenye bible juu ya uwezo wa mungu, utaogopa. Asingeshindwa kuondoa njaa na kiu kwenye mwili wa mwanadamu kama Lengo lake lilikua ni kuabudiwa.
Swali:Je wewe una mwili na roho au mwili peke yake bila roho? Kama Ina mwili na roho je uliwahi kiona roho yako? Je kwa vile huwezi kiona roho basi ni sababu tosha kusema haipo?
Mungu yupo Ila binadamu ana uwezo mdogo saaana kumuelewe matokeo yake tunabuni taratibu na kanuni nyingi na kusema zimetoka kwa Mungu. Fini zote Zina tatizo hilo
 
Siku hiz mtu akishiba anakuja na maada kuwa hakuna mungu
Halafu naona siku hizi hawa wapinga uwepo wa Mungu wanazidi kuongezeka Tanzania tofauti na miaka ya nyuma.

Naona taratibu litakuja kuwa janga la kitaifa kama ilivyoanza issue ya mashoga kwani nao walianza taratibu na kwa kujificha lakini sasa hivi hawajifichi tena.​
 
Kila kitu kiko balanced chini ya jua,vitu vyote ambavyo tunahisi/kudhani kwamba si hai
kiuhalisia ni viumbe hai mfano mawe,udongo/ardhi na vinginevyo.

Kilichofanyika kwa sisi wanadamu ni kupewa upeo ndogo sana juu ya dunia hii ambao
hauzidi 1/64 ya uwezo wetu katika kutumia ubongo kwa maana ya 3D (x,y,z),muda/time,nafasi/space hivyo
kufanya 5D + Dimension moja ya ziada (uganga wa jadi/mizimu/mazingaombwe n.k).

Dunia kama sayari nyingine kuna millions of millions of dimensions zinazotengeneza
viumbe/vitu vingi sana visivyoonekana na kunako dimensions hizo ndiko kunako
Uungu/uumbaji,ufuatiliaji wa matukio ya vitu/viumbe vingine kwa maana ya mienendo
mfano:- binadamu chochote afikiliacho kiko ndani yake lakini uwezo wa kukifanza huko
nje yake/utegemea mazingira/dimensions zinazomzunguka na wakati gani.

Kwa ufupi ni kuwa kama tungeweza kutumia/kupewa uwezo wa angalau 1/8 ya uwezo wetu
dunia isingelikuwepo,kwa kuwa baadhi yetu wangelijifanza miungu watu ilhali kimantiki
kila mtu ni mungu wa roho yake na ujumla wetu (viumbe hai na visivyo hai) ndio Mungu mkuu
/Muumbaji wa yote kwa kutumia maji.

Kwa kuyatazama mazingira yetu tunamoishi uwepo wa Mungu upo tena unaonekana sana
kama umepewa jicho la kuweza kuona mfano mdogo ni
1.pale sisimizi/chungu wanapojitengenezea makazi yao either juu ya mti au ardhini na kamwe hawachoki kila mara huingia na kutoka na mzigo mzito/kimchanga kadogo.
2.pale sisimizi/chungu anapoona sehemu kuna ganda la muwa la jana basi chungu/sisimizi
wengi ualikana/kupeana taarifa kwenda kuvuna tena si ganda lote bali chembex2 ndogox2 na wasilimalize ganda lote.
3.pale vitu visivyo hai vinavyopewa uhai wa kudumu (majengo,madaraja,motokaa,bidhaa za chakula na dawa) either kwa mahesabu kamili au kwa kukisia.
Kwa mantiki nyingine ni kuwa palipo na (+) kuna (-) pia palipo na (Spole) kuna (Npole),hivyo Mwenyezi Mungu yupo
na Shetani pia yupo kama ambavyo ilivyo kwa binadamu wengine ni mashetani wa ukweli na wengine ni malaika wa ukweli.
Asipokuelewa achana nae, umefafanua vema kabisa
 
Back
Top Bottom