Vitisho vya Mwigulu vyamng'oa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya

Imebidi

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
339
163
CHADEMA wana kazi kubwa huku Iramba Magharibi. Miezi miwili iliyopita Mwenyekiti wa Wilaya wa CHADEMA alibambikiziwa uchawi nyumbani kwake huko Kijijini Kisana. Wanakijiji wakakusanyika na kutaka kumpiga akakimbia. Tangu kipindi hicho amekuwa akijificha. Watu walidai kipindi hicho kwamba mpango ulisukwa na Mwigulu ili kumchafua na kuharibu taswira ya CHADEMA kwa kuonyesha kwamba viongozi wa CHADEMA ni wachawi! Watu hawakuamini sana.

Sasa mhe Mwigulu amerudi juzi Bungeni na ameanza mikutano katika Jimbo lake. Juzi Mwenyekiti aliitwa akaambiwa kama anataka atulie nyumbani aache kutangatanga kama kunguru arudishe majeshi na yeye Mwigulu atamsafisha kwa sababu mpango mzima anaujua. Kweli, kijana wa watu amejisamisha leo kwenye mkutano na kutangaza kwamba, kwa maneno yake, 'anarudi kwa baba'. Kwa hivyo Mwenyekiti wa Wilaya wa Iramba Magharibi, Bwana Sembe, leo amesalimu amri kwa vitimbi vya Mwigulu na kukamata kadi ya magamba.

Nawapa angalizo CHADEMA: Katibu wenu wa wilaya pia yupo njiani. Actually huyu alikuwa CCM siku zote na amekuwa akitumiwa kuwachota CHADEMA. Sasa inasemekana CHADEMA wamesimamisha ruzuku kwa muda kwenda wilayani, na leo ameripoti kwa mabosi wa CCM hapa wilayani akidai kwamba kama ruzuku hamna hana haja ya kuendelea kubaki CHADEMA. Anasema bora yeye aondoke arudi rasmi na kuwazika CHADEMA hapa wilayani. Hii nimeipata mwenyewe kwa viongozi wa CCM waliokuwa wanaongea kwa kucheka na kutusema sisi tunaoshabikia CHADEMA hapa Kiomboi.

Kwa kifupi: CHADEMA ina watu wengi sana hapa Iramba Magharibi lakini haina VIONGOZI. Viongozi wengi wilayani wapo mfukoni wa Mwigulu na anawakatia kila akija. Ni vizuri kumuwahi huyu katibu mkampiga chini kabla Mwigulu hajamrudisha rasmi. Ni ushauri tu.
 
Mkuu si uanze wewe kuonyesha njia, maujanja yote utayapata hapa hapa jamvini, na huyo mwigulu hawezi kukufanya kitu ukiwa jamvini!! tafuta network yakwako, tengeneza then nguvu ya umma mbele!!
 
WATAKAOLETA MAGEUZI NI WANANCHI WA KAWAIDA WAACHE WAJIDANGANYE KWA KUCHUKUA VIONGOZI KWANI HUKO HAKUONGEZI KURA ZAO.vITISHO NI KAWAIDA KWA MTU ALIYEFIKIA MWISHO KISIASA.CCM BYEBYE
 
Who the hell is mwigulu? Acheni woga huyo bingwa wa kuropoka akipiga colabo na lusinde kibajaji pori aka darasa la saba. anawaogopa ndo maana anafanya hivyo chadema z a threat to ccm. Stand strong n lead others jf ipo kuwapa mwongozo

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
hao viongozi naona wako after money zaidi, hata hivyo tunahitaji viongozi wazalendo zaidi wenye kujenga hoja majukaani katika kuwatetea wanyonge
 
huyu mwigulu si ndio mtunza hazina wa ccm,basi atatumia gharama kubwa sana kujiokoa na M4C.
 
Kuna ukweli kuhusu mwigulu kuhusika na EPA, fuatilieni fedha chafu mtakubaliana nami.
 
kanu ilkuwa na watu kama hawa dakika za mwisho wakajikuta wako wachache nao wakakimbia .
 
Haana maana,yeye ni mtu 1 kati ya 1000!then by then who is he?hana lolote hana chochote!akadeki choo cha Mwingulu,ndo atajua ubaya wa kurudi ccm
 
Tusimlaumu mwigulu ambaye kazi yake ni siasa,tumlaumu mwenyekiti alieamua kwa akili yake mwenyewe kurudi kundini.
 
Watu kule iramba wameistukia chadema kufuatia mauaji waliyoyafanya kule ndago ambapo mwenyekiti wa vijana wa ccm aliuawa.
 
wana mpango mkakati baada ya bunge kwisha wafanye hujuma ya aina yeyote kwa cdm nchi nzima wanaanzakuwapa pesa viongozi wilayani wa cdm mtasikia mengi mwaka huu.
wamesahau kabla ya uchaguzi 2015 kuna chagzi ya chama hata hivyo cdm wapo kibao si mtu mmoja
 
huyo alijiunga na chama cha magamba kwa biti la chizi nchemba si kiongozi mpambanaji bali lilijichomeka ndani ya cdm kama kibaraka.atembee mpuuzi huyo!!_
 
Safari ya Ukombozi ina Mengi sana, msitishike, Amini kile unachokiona ni sahihi mwisho wa siku kitakulipa.

Bado wengi watatishika na kwenda CCM, na wengine watatangaza kuwa Siasa haiwalipi

(Mfano Dada yangu Nakaaya, aliama Chama kwa Busu na mbwembwe nyingi, akaporomoka kisiasa na kimuziki pia, Kupitia Mkasi akatangaza kuwa siasa haimtoi kakaa pembeni, sababu ni aibu ya kurudi CDM).

Singida msitishike, Arumeru walikuwa waoga sana, walitishwa sana, wale wachache walobaki na msimamo sasa ndio washindi.

Muda ndio kipimo.
MSIOGOPE
 
Back
Top Bottom