Vitisho kwa Maafisa wa Elimu.....!

Shagiguku

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
406
225
Ndugu zangu wanaNzengo wa Tanzania popote pale mlipo duniani habari zenu.....!!!!?

Ama baaada ya salaaamu, napenda nishirikishane na ninyi mambo machache hapa kupitia kipande hiki kidogo cha video.

Katika hii picha ya video anaonekana na kusikika mtu mmoja akiongea na maafisa elimu (sina uhakika kama walikuwa ni maafisa elimu wakuu au wa michezo au wa vifaa na takwimu au wa taaaluma au wa sayansi kimu) isipokuwa wanatamkwa tu kuwa ni maaafisa elimu.

Ndugu zangu wanaNzengo wa Tanzania, katika video hii huyu bwana anayeongea na hawa maafisa elimu naona anawashutumu kwa kuwa wanafunzi hawajafauru darasani (TAALUMA). Lakini kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba, watoto hao hao wamefauru viwanjani (MICHEZO) na kuchukua vikombe mbalimbali.

Ikumbukwe kwamba, michezo ni SOMO kama yalivyo masomo mengine shuleni, na lipo kwenye ratiba ya vipindi vya shule kama yalivyo masomo mengine ya Kiswahili, Uraia, Historia, Jiografia, Stadi za Kazii nk! Na somo hili kwenye ratiba ya shule lipo likijulikana kama HAIBA NA MICHEZO.

Lakini pia somo hili lipo kwenye Muhtasari wa Masomo wa Tanzania. Lakini pia somo hili lina walimu ambao wamelisomea vyuoni (eg Butimba chuo cha ualimu, Malya chuo cha michezo nk). Isitoshe somo hilo la michezo linatambulika na serikali kupitia wizara yake ya elimu kwamba linapaswa kufundishwa katika shule zetu zote za awali, msingi, upili ya chini na upili ya juu, hadi vyuo na vyuo vikuuu. Isitoshe, serikali hadi imekuwa ikigharamikia michezo ya shule za msingi, shule za upili, vyuo, na vyuo vikuu kwa maaana kwamba hao wanafunzi wanafundishwa hili somo katika shule zao, hivo wanahitaji sehemu ya kwenda kulifanyia kazi (ku-practice) kile walichofundishwa na walimu wao.

Na kama wamefundishwa vizuri na kufauru hilo somo, basi matokeo yake yatajidhihirisha kwenye mashindano ima ya UMITASHUMTA au UMITASETA au katika vyuo kwa kutwaa vikombe vya michezo kama walivofanya hao wanamichezo wanaosemwa kwenye hii video.

Hoja yangu hapa ni kwamba:

1. Kwa nini washutumiwe maafisa elimu kwamba watoto wamefeli darasani!?? Kwa nini huyu mtu hapongezi kwamba wamefaulu viwanjani? Kwani michezo hiyo waliyofaulu siyo sehemu ya masomo waliyofundishwa? Na kama ni sehemu ya masomo waliyofundishwa na kufaulu vizuri kwa nini huyo mtoa shutuma anaangalia kona (Angle) moja tu ya ELIMU, yaaani taaaluma tu!!? Kwa nini michezo iliyopo kiutalatibu asiithamini!!??

2. Kwa nini awatishe maafisa wa elimu!!??? Kwani wao ndiyo waliofeli hiyo taaaluma ya darasani au wanafunzi shuleni!!??? Kazi ya afisa wa elimu ni ipi!? Je, ni kufundisha wanafunzi darasani au kusimamia elimu kwa ujumla wake (ikiwepo na ELIMU KWA MICHEZO....!!!?????). Na kama kazi yao ni kusimamia tu utekelezaji wa elimu kwa ujumla katika maeneo yao, anajuaje kwamba hawakuutekeleza huo wajibu wao???

3. Kama anawashutumu hao maafisa wa elimu kwamba "wamesababisha" wanafunzi kufeli darasani. Yeye akiwa kama bosi wa hao maafisa wa elimu katika eneo lakwe, amefanya juhudi gani ili kusababisha wanafunzi wafaulu hiyo TAALUMA anayoitaka!!!? Je, haoni kwamba na yeye ni mmoja wa watu waliosababisha wanafunzi kufeli kwa yeye pia kutokuchangia ufaulu wa wanafunzi kwa kufanya tendo la kuwafaulisha!!!!? (Najua hapa wanaNzengo wenzangu hamjanielewa kwenye hiii pointi).

4. Je, huyu bwana mtoa shutuma kwa maaafisa wa elimu walioaminiwa na serikali na kupewa dhamana ya kuongoza shughuli za elimu katika maeneno yao; haelewi na kufahamu kwamba UFAULU wa mwanafunzi DARASANI huchangiwa na mambo mengi na siyo afisa elimu tu!!!!????

Je, amewauliza WAZAZI walichangia nini katika ufaulu wa watoto wao kule shuleni DARASANI!!!????

Je, amewauliza hao maafisa wa elimu kama wana walimu wa kutosha kuhudumia kila mtoto mmoja mmoja darasani hadi aje afaulu!!!???

Je, amewauliza walimu wanaowafundisha hao wanafunzi kam wana vyumba vya madarasa vya kutosha kuwaweka wanafunzi kwa kiwango kinachotajwa kwenye SERA YA ELIMU!!!!???

Je, amewauliza walimu kule madarasani wanakofundisha kama wana vitabu vya kutosha angalau kitabu kimoja kwa watoto WATATU!!!???

Je, huyu mtoa shutuma kwa maaafisa wa elimu walioaminiwa na serikali amewauliza walimu kule shuleni kama wana VYOOO (hapa unaweza kusema matundu ya vyoo) vya kutosha wanafunzi walionao shuleni!!? Ikumbukwe pia upungufu au ukosefu wa vyoo huchangia KUFELI kwa wanafunzi shuleni (kwa mujibu wa utafiti).

Je, huyu mtoa shutuma na vitisho kwa maafisa wa elimu walioaminiwa na serikali, amefuatilia na kuona kuwa wanafunzi wana maeneo ya kutosha ya kuchezea michezo (na hapa namaanisha viwanja vya michezo YOTE) ikumbukwe kwamba michezo huchangia kufaulu darasani.

Je, huyu mtoa shutuma na vitisho kwa maafisa wa elimu walioaminiwa na kukubalika na serikali ya jamhuri ya Tanzania amekutana na wanafunzi wenyewe na kuwauliza kwa nini HAWAKUFAULU masomo yao!!!!??? Kwamba walifanya juhudi gani za kuonesha kwamba walikuwa na NIA ya kufaulu!!!??? (Ikumbukwe kwamba, mwanafunzi anamchango mkubwa saana katika kufaulu kwake yeye mwenyewe).

5. Nikija kwenu rafiki zangu maafisa wa elimu "washutumiwa na watishwa"

Je, kuna chuo chochote mlichowahi kwenda kusomea hivyo vyeo vya uafisa wa elimu!? Kama havipo vyuo vya uafisa wa elimu kwa nini mtishwe na mtu ambaye anashida kwenye kiyoyozi ofisini na kwenye gari asiyejua magumu ya kazi mnayokutana nayo katika kusimamia ELIMU (Taaaluma na Michezo!!!!????) Kwa nini kwa pamoja na umoja wenu msimwandikie kwenye hizo "plain paper" msimwandikie kile anachotaka au anachowatisha nacho ili aone kwamba ninyi siyo wa kutishwa!!!??

Ama ndo ule msemo niliwahi kuusoma kwenye gazeti la RAI la kipindi hicho ambapo gazeti la rai lilikuwaga bado gazeti! Msemo usemao, "kila mtu na ka-mhogo kakwe....!!!???"" Kwamba kila afisa wa elimu "mshutumiwa na mtishiwa" anaogopa kukapoteza ka mhogo kakwe!!!!???

MwanaNzengo miye binafsi nilikuwa naona huuu ndo ulikuwa wakati wa kumwoneshea huyu mtoa shutuma na vitisho kwenu kwamba mna ile kitu inaimbagwa kila siku ya mei mosi, kwamba "SOLIDARITY FOREVER" hapa ndo ilikuwa muda wa kumuonesha huo mshikamano wenu kwa kumwandikia ninyi nyote kwa pamoja kwamba MNAAACHA KAZI YA UAFISA ELIMU....! (Teheeee teheeee teheee, najua ni ngumu saaana kumeza hiii, na hamtanielewa hapa maaana kila mtu na "ka-mhogo kakwe" hatukuja pamoja, tulikutana tu ofisini).

6. Kwako Bosi mtoa shutuma kwa maaafisa wa elimu walioaminiwa na serikali, kumbuka kwamba, siyo kila jambo hutatuliwa kwa kutoa vitisho. Hivi wakikuzilia hapo huo uafisa wa eliu kwa pamoja kwa wakati mmmoja utafanya nini!!??

Jiruhusu kichwani mwako BUSARA iwe inatawala zaidi kuliko vitisho. Ukiwa kama kiongozi wa watu sehemu yoyote kisaikolojia vitisho kwa watu unaowaongoza ni njia inayoonesha udhaifu wako wa kiuongozi, kwamba umeshindwa wewe kama bosi wao kutatua changamoto za kielimu katika eneo lako la kiutawala kwa kubuni na kutumia njia zenye tija katika kufanya wanafunzi wafaulu, na sasa unawatisha wasimamizi wa elimu walioaminiwa na serikali ili wakuogope wewe, ili na wao watoke hapo wakiwa wamejawa na woga na hofu nao waende wakawatishe walimu wakuuu shuleni, ili walimu wakuuu nao wajawe hofu na woga wakawatishe walimu wa madarasa na walimu wa masomo darasani, ili nao wakawatishe wanafunzi tunaoTAKA WAFAULU (Ninachoelewa hapa kwa huyu huyu mtishiwa wa mwisho ataishia kuchezea stiki za nguvu ili afaulu kwa lazima kwa kuwa kufaulu kwa hiyari kumeshindikana).

Kisaaaaa! Eti bosi mtoa vitisho kasema, Ebooooo....!!

Matokeo yakwe tunakuwa na watu waliojaaa vitisho tu na siyo wabunifu wa kutatua changamoto zinazowakabili.

MwanaNzengo miye napenda kuwasilisha sasa...!

Nakala kwa bosi mtoa vitisho, aisome kwa ufahamu na uelewa wa kiuongozi (Managerial Skills in Leadership).
 
Devon sawa

Senior Member
Apr 30, 2017
164

Bila shaka utakua mwalimu wa art,hebu npatie summary mkuu prngine ntaweza pata madodoso
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,786
2,000
Walimu wanaonewa sana na ma DC na ma RC nchi hii, aende akawachezee madaktari aone cha moto
 
Nkolandoto

JF-Expert Member
Sep 18, 2016
2,876
2,000
Huyu jamaa alikuwa ameingia kichwa kichwa namtoa belenge

Namwandikia madai yote ya waalimu

Vifaa vyote pungufu

Idadi ya waalimu standard wanaoitajika

Na miundo mbinu yote ktk eneo langu

Namwambia nitimizie hivi ufaulu utapanda

Kama stafanya hata kimoja
 
UKAWA2

JF-Expert Member
Apr 22, 2014
2,186
2,000
Wewe unaumiza akili yako na unatumia muda wako wote kujadili mambo ya zero brain in Gwajima's voice!
 
exit

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
1,662
2,000
Mimi naona wamsamehe tu huyo mtoa shutuma maana hajuwi atendalo, sababu yeye mwenyewe shule imempiga chenga. Kwa muelewa angejiuliza alifanya investment gani msimu uliopita mpaka matokeo yakawa hivyo. Kama hayakuwepo basi angeakaa nao chini na kuweka mikakati ya kuboresha elimu kwenye mkoa wake kwanza,wangekuja kufeli baada ya mikakati kuwekwa na muda kutumika hapo angewashutumu sasa. Ndio shida ya kuongozwa na vilaza. On Gwajima voice zero brain ahah.
 
kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
3,704
2,000
Mnajihangaisha namtu ambaye hajawahi kushinda chochote maishani...siyo cheti sio mtoto!! Anachoweza ni kuongea tuuu....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom