Asante sana kwa mada, mie ndio navurugwa kabisa na the so called viti maalum, wataalam wa siasa na uongozi tunaomba mtusaidie. Kwenye mkoa mmoja ninaamini kuna wilaya/majimbo ya uchaguzi kadhaa ambayo yatatoa wabunge (aka wawakilishi wa wananchi bungeni). Kisha, kila mkoa tena unapewa nafasi ya uwakilishi kwa kofia ya viti maalum bungeni, ambao hawa wanakuwa wabunge nao! Sasa huyu wa mkoa anaenda kusema nini tena bungeni jamani wakati wapo waliotoka kwenye wilaya/majimbo kede kede! Kama wabunge wote wa kuchaguliwa ndani ya mkoa mmoja wakakaa kama kamati hawawezi kuuwakilisha mkoa?
Hivi kweli si ndio maana wanazidi kutukandamiza na kodi ili ikawalee watu wote hawa, ili hali tungepewa fursa ya kuchagua tungesema hiyo kodi iende kwenye miundo mbinu/mahospitali!
Hii mifumo mizigo tunaitoa wapi au tuliirithi wapi toba yarabi?