Vitendo 19 vya kifisadi vya blandina nyoni.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitendo 19 vya kifisadi vya blandina nyoni....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jozzb, Feb 11, 2012.

 1. j

  jozzb Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Hivi ni baadhi ya vitendo vya kifisadi vya Mama huyu ambaye kwa wengine wanamuona kama mchapa kazi hodari asiyekuwa na doa na anaezuia mianya ya wizi:-


  1. Amekuwa akilipwa mshahara wa ziada na Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) wakati tayari serikali inamlipa mshahara wa ngazi ya Commissioner kupita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  2. Ametengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na afisa manunuzi wake badala yake ame centralize kwake mwenyewe. Kwa maana hiyo, manunuzi yote ya Wizara anamlazimisha (Comand) Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi kumpa kazi zote ndugu yake anaeitwa Donatha Koko.  3. Amekuwa akicomand wizara kununua uniform za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na
  Maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za manunuzi.


  4. Katika mikutano yote inayofanyika Wizarani, amekuwa akicomand kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa tenda ya kulisha chakula washiriki tangu alipotua Wizarani
  kama Katibu Mkuu.


  5. Miezi mitatu iliyopita aliiteua kampuni ya Soft tech ambayo yeye ni mbia kwenda kukagua Accounts System ya Muhimbili kinyume na kanuni za kikaguzi kwa kuwa tayari ana ‘Conflict of Interest’


  6. Amekuwa akiongoza Wizara kwa kutumia Informers ambao kazi
  yao kubwa ni kumpelekea habari nani anasema nini na nani anasema nini kuhusu yeye binafsi na uongozi wake. Informers wake wakuu ni Elias Mkumbo ambaye ni dereva na Donatha Koko ambeye ni ndugu yake wa damu damu na ni afisa ugavi wa wizara


  7. Amemkopesha gari la serikali aina ya Suzuki Informer wake Elias Mkumbo (dereva) ambae kimsingi hastahili kukopeshwa gari kutokana na cheo chake. Kwa dereva wa serikali, anachoruhusiwa kukopa ni Baiskeli, Piki piki na Piki piki ya miguu mitatu (Bajaj)


  8. Amenunua vingamuzi vya magari manne kwa shilingi 1.3 Billion bila kufuata taratibu za manunuzi kwa kucomand Single source procurement kutoka kampuni moja yenye makao yake huko
  Israel. Manunuzi haya yamefanyika wakati Hospitali nchini zikiwa hazina dawa, Interns doctors hawajalipwa mishahara yao, watumishi wake wakidai fedha za likizo, uhamisho na vyuo vingi vya afya vilivyo chini yake vikiwa na madeni lukuki.


  9. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamisha kiasi cha Shilingi 1,968,475,931
  mali ya Wizara ya Afya kwenda National Institute for Medical Research (NIMR) bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizi zilikuja kuhojiwa na CAG katika ripoti yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010


  :A S 465:NIMEYAKUTA HUKU << BLANDINA NYONI>>
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,954
  Likes Received: 23,831
  Trophy Points: 280
  Hii thread mbona inarudiwa kila siku?
   
 3. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kumbe babu huwa unapita pande hizi?
  Hata mimi nashangaa!!!
   
 4. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  wengine ndio tunaiona kwa mara ya kwanza. Thanx mdau kwa kuileta tena.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  inaboa sasa.... imerudiwa mara ya karibia nane
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,954
  Likes Received: 23,831
  Trophy Points: 280
  Napita sana huku kucheki mnavyotoana mapovu na kina bigirita....
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,954
  Likes Received: 23,831
  Trophy Points: 280
  Nausi sana hii marudio asee...naumisa sana..... nakuwa kama ile nyimbo ya mgogo pale Port View.
   
 8. H

  Hhm Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Aisee....kweli kama haya ni kweli na kamati au vyombo vya dola vilivyopewa kazi yakumchunguza vikithibitisha haki ya nani asipowekwa segerea yatupasa watz tuandamane....serious...hii inauma sana wanaume jf @ Asprin acha irudiwe tuu hii ni tuhuma mzito.nilikuwa sijaiona....kumbe mtoto wa mkulima aliiona hii .....duh mulika mwizi jf big up.
   
Loading...