Vitambulisho vya taifa

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema awamu ya kwanza ya Vitambulisho vya Taifa imekamilika na vitaanza kutolewa mapema mwezi ujao.

Imesema kuwa uzinduzi wa kutoa vitambulisho hivyo ulikuwa ufanyike jana katika maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini ilishindikana kutokana na shughuli nyingi na ukubwa wa tukio hilo.

Ofisa Habari wa NIDA, Rose Mdami alisema uzinduzi huo unatarajiwa kufanywa na Rais Jakaya Kikwete ambapo wiki ijayo watazungumza na waandishi wa habari na kuelezea utaratibu mzima utakavyokuwa.

Source;

HabariLeo | Vitambulisho vya Taifa vyakamilika
 
mmh mi nna wasiwasi na hizo habari za kutoa vitambulisho mwezi ujao mi toka nimejaza fomu mwezi wa kwanza wakasema watarudi kuchukua finga print na picha hawajarudi tena sasa vitatoka kwa style gani? hizo ni ngonjera tu ngoja tuone kama wameanza kuwa wakweli
 
Back
Top Bottom