Vitambulisho vya Magufuli, mtu anatakiwa awe na mtaji wa bei gani?

kitotola

New Member
Mar 25, 2017
4
0
Habari wanaccm wenzangu!

Kwa anayefahamu ni mjasiriamali mwenye mtaji kiasi gani anatakiwa alipie kitambulisho cha Tsh 20000/=?

Nauliza kwa sababu naona huku kwetu Mipingo-Lindi hata mtu ambaye amepanda bamia za kula mwenye nyumbani kwake siku akikosa pesa ya kusaga akiamua kuchuma fungu tano ili apate Tsh 1000/= tu anazuiliwa na kutakiwa alipe Tsh 20000/= How comes mtu mwenye bamia ambazo akiuza zote anapata buku tu tena hufanya hivyo mara moja kwa mwezi kwa lengo la kupata pesa ya kusaga naye huyu ni mjasiriamali au mchambikaji.

Mtu mwenye kuku wa tatu siku mmoja anaumwa akiamua kumchinja na kuuza supu kwa kutembeza ili hasipate hasara kabisa ,anazuiliwa na kutakiwa alipe Tsh 20000/= je hii ndio maana aliyomaanisha Rais au watendaji wetu huku chini wametafsiri vibaya?

Mimi nilivyokuwa chuo nilikuwa napenda kuhudhuria mafunzo ya ujasiriamali na wawezeshaji walikuwa wanatuambia hata Tsh 10000/= inatosha kuwa mtaji kwa kutoa mfano kuwa unaweza kununu karanga kg 4 kwa Tsh 2000 @kg jumla tsh 8000/= na Tsh 2000/= mifuko ya kufungia karanga na hivyo ukikaanga na kuuza unaweza kupata faida ya Tsh 2500/= ukiuza siku kumi unapata faida ya Tsh 25000/= lakini leo ukiwa na mtaji wa Tsh 10000/= utashindwa kuanzisha mradi kwakuwa utazuiliwa kuuza kwa sababu tu hauna Tsh 20000/=

Is this what our president meant? au ametafsriwa vibaya?

Hili sakata linakwenda kuwa agenda kwa wapinzani na linaweza kutuumiza CCM serikali za mitaa na hata uchaguzi mkuu.

Mimi nawaomba viongozi wa chama kuisimamia serikali katika hili ili lisiwaumize wachambikaji bali ichukue 20000 kwa wajasariamali na si wachambikaji.

Serikali iseme wazi ni mwenye mtaji kuanzia Tsh ngapi ndio wanatakiwa walipe Tsh 20000/= ili kuondoa sintofahamu na sio viongozi wa juu kuwapa maagizo viongozi wa chini wamalize vitambulisho walivyowapa hata kwa kuwaumiza wachambikaji.

I don't think kama Mhe Rais alikuwa na lengo hili.

Naomba ufafanuzi
 
Mmoja kashaliwa kichwa huko kisa vitambulisho vya mkulu, watendaji kutaka sifa usishangae hayo yanayoendelea
 
Kuanzia mtaji wa shilingi moja hadi milioni nne,lazima uwe na kitambulisho iwapo unataka kufanya biashara ya kuuza chochote kwenye ardhi ya Tanzania,ni Tshs 20,000/= kwa mwaka.Ila hupaswi tena kulipa ushuru wa aina yoyote ile.
 
Hiyo lugha uliyoitumia kuwasilisha ujumbe wako ni matusi.
Kila kona ya paragraph lipo! Hivi mchambikaji ni nani na mchambaji ni nani katika muktadha wa mada yako?
 
Kuanzia mtaji wa shilingi moja hadi milioni nne,lazima uwe na kitambulisho iwapo unataka kufanya biashara ya kuuza chochote kwenye ardhi ya Tanzania,ni Tshs 20,000/= kwa mwaka.Ila hupaswi tena kulipa ushuru wa aina yoyote ile.
Mbona tukienda tra wanatuchanganya na hata tulipoenda kuchukua hivyo vitambulisho wanataka mtu Mwenye mauzo yasiyozidi million 4 Kwa mwaka hii imekaaje
 
Back
Top Bottom