Vitambulisho vya Machinga Arusha, RC Gambo Tumbo Joto

Vitambulisho vya Machinga Arusha, RC Gambo Tumbo Joto

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
469
Sakata la vitambulisho Vya wamachinga Mkoa wa Arusha,limechukua sura Mpya Mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuamuru wakuu wa Idara mbalimbali za serikali Jijini hapa wakiwemo TRA kuuza Vitambulisho hivyo kwa lazima.

Jambo hilo liliibuka katika baraza la madiwani wa halmashauri ya Jiji la Arusha waliokuwa wakihoji hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuwagawia watumishi wa serikali wakiwemo wakuu wa Idara ya mamlaka ya Mapato TRA Mkoani hapa kuuza vitambulisho hivyo .

Moja ya watumishi wa TRA jina (limehifadhiwa)amekiri kupatiwa vitambulisho 100 akaviuze jambo ambalo alidai limemfanya asifanyekazi aliyoajiriwa nayo kwa ufanisi badala yake amekuwa akishinda mtaani akisaka wamachinga ili auze vitambulisho hivyo alivyokabidhiwa na mkuu wa Mkoa Gambo baada ya kutishiwa asipoviuza atakatwa mshahara wake kufidia.

"Mimi nimepewa vitambulisho 100 Vya machinga nikauze ila sijui nitamuuzia nani maana kila ninayemfuata ananiambia tiyari anacho ,nimeamua kuvikopesa maana tunatishiwa kukatwa mshahara sijui nifanyaje maana hapa kila mkuu wa Idara amepatiwa vitambulisho 100" Alisema mmoja ya mkuu wa Idara TRA.

Wengine waliokumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na mamlaka ya maji AUWSA ambao pia wamepatia kuuza Vitambulisho pamoja na taasisi zingine za serikali Mkoani hapa.

Inadaiwa kuwa Gambo alichukua vitambulisho 125,000 kwa sifa ya kuonekana kwamba anauwezo wa kuuza Vitambulisho vingi na kuipita mikoa mingine jambo ambalo linawaumiza watumishi wengine wa serikali kwa kushinda wakiuza vitambulisho mitaani na kusahau Kazi walioajiriwa nayo.

Katika hatua nyingine ,Gambo anadaiwa kutokuwa na maelewano mazuri na viongozi wenzake wa serikali jambo libalisababisha kudhorota kwa shughuli za maendeleo ya Mkoa

Hivi karibuni Gambo aliamuru Takukuru Mkoani hapa kumkamata na Kumhoji katibu tawala wa Mkoa ,Richard Kwitega, pamoja na afisa salama aliyejulikana kwa jina moja la Kassimu kwa madai ya kupata mgao kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya uwindaji ya OBC ambaye bado anashikiliwa mahabusu kwa kosa la uhujumu uchumi.

Jambo hilo linadai kuwakera wafanyakazi mbalimbali Mkoani hapa kwa kitendo hicho kwani mbali ya kuwadhalilisha kimewapunguzia morari wa utendaji Kazi Mkoani hapo.
 
Sio Arusha tu Mikoa mingi wafanyakazi wanazunguka kama hawana akili nzuri

Wanachotaka ulete hela kulingana na idadi ya vitambulisho

Na kule kwa Happy si ndo wakubwa walinyimwa likizo eh!!!

Kazi ipo awamu hii
 
Hivyo vitambulisho vinaitajika sana huku kwetu wavilete haraka
 
Vileteni huku Mabwepande waliko wanaume
Tunavichukua vyote,wala hakuna sababu ya kuzunguka navyo mitaani
 
Kuna huyu bwana mdogo anaitwa hapi nae ni mihemko kila uchao ni swala la muda sanaa zao zitakua hadharani
 
Hivyo ndiyo tunavyo omba sana sisi wana wa Arusha ili hao wapinga maendeleo ya Arusha waparulane vilivyo
 
Hapo ndiyo wametufanya kuwaelewa nia ya o ya kuuza hivyo vitambulisho kuwa siyo kumsaidia mlala hoi bali ni kuongeza kipato
Kuna huyu bwana mdogo anaitwa hapi nae ni mihemko kila uchao ni swala la muda sanaa zao zitakua hadharani
 
Hapa ndo utajua manufaa ya kuongoza na madhara ya kutawala.
 
Kama kila mtu anayepekekewa kitambulisho anacho bas ajue tayar wote wamepata Kama alichukua kwa sifa ili aonekane mbele ya mtukufu Rais hapo atajua yeye na s kusumbua watu analifanya zoez kuonekana Kama kodi ya kichwa

Wakat utafika yasiyojulikana yatajulikana maana muda uliobaki n mchache Sana uchaguz upo jiran mirad mikubwa tusioijua bajet yake I anasuasua
 
Imekula kwako, ndo umefungua account Leo ili umchafue Gambo, acha unafiki. Hivi wewe ni ke ama me? Chaliangu hata mfanyeje chuga tunamwelewa Gambo wetu. Temana nae asee
 
Ninahitaji waniuzie viwili, kimoja changu na kimoja cha mke wangu. Ila hata hao wanaouza hivyo vitambulisho na wao wamekuwa wamachinga kwahiyo waanze kwa kununua wao. Vinginevyo watakuwa wanafanya biashara hiyo bila kuwa na vitambulisho.
 
Back
Top Bottom