Mbona hivi vitabu vipo tele tu katika maduka ya kuuzia vitabu "book shops", ingekuwa upo visiwani ningekuelekeza kwa Farouk Karim, Masomo BookShop, Darajani.
Bytheway, Huyu muandishi wa Riwaya hizi yupo wapi siku hizi, na anafanya kazi gani?
Nilizipenda sana kazi zake kama hizo ulizozitaja, lakini iliyonisisimua zaidi ni ile ya KIKOMO.
Du! Mkuu umenikumbusha mbali saaana . . . Mwaka 1985 nadhani, mpaka maneno ya chaper ya kwanza nakumbuka kutoka Liwaya ya "Kufa na Kupona" . . . .
"Ilivyo ni kwamba, mimi siku ya Jumapili hulala mpaka saa nne asubuhi, na kama huamini hiyo si shida yangu . . . ."
Nadhani mkuu, ukiwaomba jamaa wanaouza vitabu mtaani kama maeneo ya Tancot House wanaweza wakakusaidia.
mkuu ikbidi nije huko visiwani nitakuja,
ninavojua huyu Elvis Musiba sasa hivi ni mtu mzito, nadhani alikuwa mwenyekitiwa shirikisho la wenye viwanda na kilimo, sina hakika kama ni kama ana wadhifa huo hadi sasa,,
sawa sawa, mr. Aristablus elvis musiba alikuwa mwenyekiti wa tanzania chamber of commerce and agriculture.sasa hivi anafanya biashara zake.
wakuu naombeni msaada wenu kama kuna anayejua ninakoweza kupata hivi vitabu ya Elvis Musiba, vikiwa na stellingi Willy Gamba.
Vitabu hivyo ni kama vile:
1.Kikosi cha Kisasi
2.Kufa na Kupona
3.Hofu.
4.Njama
5.Uchu
na vinginevyo. nimevisoma baadhi zamani lakini sasa hivi sina nakala tena ningependa kujua ninakoweza kuvipata.
shukrani!
Mbona hivi vitabu vipo tele tu katika maduka ya kuuzia vitabu "book shops", ingekuwa upo visiwani ningekuelekeza kwa Farouk Karim, Masomo BookShop, Darajani.
Bytheway, Huyu muandishi wa Riwaya hizi yupo wapi siku hizi, na anafanya kazi gani?
Nilizipenda sana kazi zake kama hizo ulizozitaja, lakini iliyonisisimua zaidi ni ile ya KIKOMO.
Unfortunately sipo zanzibar muda mrefu sasa, lakini kama unavitaka kweli Masomo Bookshop, Darajani ni pahala pa uhakika zaidi, unaweza kuwasiliana na Farouk Karim mwenyewe anakuwepo dukani hapo, au unaweza kupata kontakti zake katika Ofisi yoyote ya ITV/Redio One, Dsm hapo,(yye ni mwandishi wa habari wa vituo hivyo), au mwandishi yeyote wa vituo hivyo anaweza akakupatia kontakti zake.Kama utaweza kufika zanzibar, ukifika soko kuu la Darajani, ukimuuliza mtu yeyote wapi Masomo Bookshop kwa Farouk Karim atakupeleka wala si mbali kutoka sokoni.Mkuu, kama kweli unaweza kuvipata vitabu hivi please tuwasiliane, Kikosi cha Kisasi, Kikomo, Kufa na Kupona, na Njama. Au nielekeze vizuri kwa jamaa na mawasiliano yake ni mpigie nivipate hivyo vitabu kaka!
Yeah,jamaa alikuwa mzuri sana kwenye masuala ya Riwaya but hata mimi nashawishika kwamba alikuwa anagandamizia kwa James Hadley Chase...Za masiku kaka.....Elvis Musiba alikuwa mwandishi mzuri wa vitabu vya riwaya...sijui kwanini ameacha hiyo kazi. Kama kuna mtu amewahi kusoma vitabu vya James Hadley Chaseatakubaliana nami uandishi wake unashabihiana sana na wa Musiba, watu wanawasi wasi huenda mzee Musiba alikuwa anafanya tafasiri ya baadhi ya kazi za Chase kwenda kiswahili na mazingira ya kitazania na kuongezea vikolombwezo vya majina ya kibantu. Nimesoma almost vitabu vyote vya Musiba na baadhi ya kazi za James Hadley Chase kama
The Sucker Punch
A Coffin From Hong Kong
Tell It To The Birds
Knock, Knock! Who's There?
A Can Of Worms
na You never know with women
Nashawishika huenda bwana Musiba alikuwa anasoma novel hizi pia na kuzitafasiri......
Pamoja na mtizamo wangu huo bado anabakia mwandishi mzuri wa riwaya aliyewahi tokea Tanzania
Yeah,jamaa alikuwa mzuri sana kwenye masuala ya Riwaya but hata mimi nashawishika kwamba alikuwa anagandamizia kwa James Hadley Chase...Za masiku kaka.....
Habari ndo hiyo...Nashukuru nimerudi salama ndani ya jamvi Nkwingwa baada ya likizo ya muda mrefu,hao wazee wa kulialia bado tu hawajaacha!!!!!...Salama ndugu yangu, tupo na ugumu ugumu wakulalamika hapa JF!
Nimeona watanzania kwa kugandamiza tupo makini ...inasemekana hata Marehemu Mwalimu Nyerere alikuwa anagandamiza kazi za William Shakespeare!
Habari ndo hiyo...Nashukuru nimerudi salama ndani ya jamvi Nkwingwa baada ya likizo ya muda mrefu,hao wazee wa kulialia bado tu hawajaacha!!!!!...
YoYo sina taarifa zake...Nenda mkuu,mi mwenyewe nimetoka Usukumani karibuni tu,siku hizi kule maji bwerereKama likizo poa, nilihisi uko na Yo Yo Jela..... nami nategemea chukua mwishoni mwa week ijayo nikatembelee makaburi ya wahenga usukumani!
Yoyo sina taarifa zake...Nenda mkuu,mi mwenyewe nimetoka Usukumani karibuni tu,siku hizi kule maji bwerere