Vitabu vya ict | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitabu vya ict

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mtazamaji, Nov 24, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wahenga walisema elimu haina mwisho. Hivyo hivyo kwenye Teknohama umuhimu wa wadau kupitia pitia mabukuleti na machapisho ya wataalam . Ni sababu hiyo naleta chapisho linalohusi VITABU

  Kwa wale wanaopenda kuchimba chimbua zaidi kupitia vitabu mambo ya Teknolojiaya ICT Chapisho hili litataja baadhi ya vitabu vya kutafuta kulingana na mada. Kwa wale wanojua vitabu vizuri zaidi y nilivyotaja nitashukuru nikifahamishwa na kupata mrejesho(feedback) ili niviongeze katika list. Vtabu hivi vingi vnapatikana mtandaoni kama ukishindwa kukipata unachohitaji nishtue...............

  VITABU VYA DATABASE
  Database Systems – Design, Implementation & Management by coronel- morris- rob
  [​IMG]

  Tovuti maarufu ya kuuza vitu kutumia mtandao ya amazon inaeleza katika topic ya database kitabu hiki ndio kinaongoza kwa mauzo. kitabu kina mpa msomaji msingi wa uelewa wa nadharia na vitendo jinsi ya kufanya mchakato , kudesign na kuunda Database katika mazingira fulani. Msomaji atakutana na kuelewa maana ya maneno kama kama Data Modeling, Normalisation , ERD nk . Kina mifano na maswali ya database yanayotokea katika ulimwengu halisi tunaoishi au ambayo wataalamu wanakutana nayo na kutakiwa kuyapatia ufumbuzi.


  Database Management Systems – Ramakrishnan
  [​IMG]
  Kitabu hiki kinaelezea sifa za mifumo ya database (DBMS) . Maudhurio ya wanafunzi yaliyoingizwa wenye Ms excel ni tofauti na maudhrio ya wanafunzi yaiyongizwa kwenye DBMS.(Sqlserver, mySql, oracle, etc) kitabu kinaeleza aina ya DBMS zilizopo na jinsi zinavyofanya kazi . na tofauti ya DBMS na application nyingine. Kina kurasa zisizozidi 1098. Kitabu hkii na pamoja na kile nilichotaja pale juu kwa pamja vinamuwezesha mtu kudeal na Issue za database kwa DBMS yeyote iwe ni MySql, Microsoft SQL server, Oracle, na nyinginezo.

  VITABU VYA PROGRAMMING
  Let Us C – Yashwant Kanetkar
  [​IMG]

  Mwandishi Yashwant Kanetkar katika buku hili anatumia lugha rahisi na nyepesi .Kimenisaidia kuelewa misingi (Basics) za programmming . Bahati mbaya nilisoma kitabu hiki nikiwa nimemaliza kanumba's college.Kilifanya niiipende na kuwa na mwamko tena na programming. Kila sura ya kitabu inaelezea mambo muhimu katika mtiririko mzuri ambao msomaji akielewa itamsaidia hata kwenye program language nyingine zinazotumika sasa kama Java, C#, phyton, etc Kwa mtu anayeanza na kutaka kujua Concept za programmming Lets C ni kitabu kizuri.  Design Patterns.Elementt of Reusable object Oriented Software
  [​IMG]

  Kimeandikwa na waandishi wanne, Erich Gamma , Richard Helm , Ralph Johnson na John Vlissides. Kwa progrmmaer ambaye ameshakuwa na uzoefu basi kitabu aina hii ni hatua ya pili kuingia ndani zaidi katika ulimwengu wa programming. Hasa hasa katika design pattern za Object Oriented.


  MABUKU YA NETWORK
  Internetworking technology handbook- by Cisco Systems
  Kitabu ni msingi mzuri kuelewa mambo ya network.(mtandao) Kinaongelea na kufafanua mambo kama kama vile LAN, WAN, TCP/IP, switching, ethernet, X.25, etc . vile vile kinaongelea management na designig ya network. ROUTING ambayo ni moja ya mada muhimu kwenye network nayo imechambuliwa vilivyo kwenye buku hili ambalo pia linapatikana kwenye Wiki ya CISCO.  Computer Networking A Top Down Approach–James F. Kurose, Keith W. Ross
  [​IMG]
  Buku hili linajaribu kungia deep kidogo kuhusu mambo ya protocols na standard zinazotumika kwenye mawasialiano ya komyuta kompyuta. Kwa kufuata nadharia ya madaraja saba yaliyowekwa ( (7 layers of OSI Model)Kitabu hiki kinafafanua na kinampa msomaji mwanga wa kujua hatua , protocol,ulinzi(Security) yanayofanyika katika kila daraja mpaka signal kufika kwa kifaa cha mlengwa.


  VITABU VYA KUHUSU OS
  Operating Systems – Internals and Design Principles – W. Stallings
  Mwandishi ni mshindi wa tuzo ya kitabu bora mwaka 2009 kutoka Chama cha "Text and Academic Authors Association" (TAA)! . Stalling kaweza kufafanua kwa urahisi na kuelewea dhana muhumu za OS itu mbacho kwa vitabu vingine imekuwa kazi kumpa msomaji picha kamili. ​
  Modern Operating Systems by Andrew S. Tanenbaum
  [​IMG]


  Pamoja na kitabu hiki wandishi Andrew S. Tanenbaum kaandika vitabu vingine vinavyohusiana na OS kama Distributed systems na Operating systems. Nimesoma baadhi yasur za Katika toleo a tatu la itabu hiki na inabainisha teknolojia au mbinu mpya zinazotumwa kwenye version mpya za OS kama Linux , Winodws na Mac. vile Vile lina KItabu kinaonglea jinsa OS za kisasa zina deal na Multmedia , virtual machine na hata antivirus. Kwa mujibu wa Amazon mwandishi huyu vitabu vykae vinaongoza kwa mauzo kwenye mambo ya OS.


  VITABU KUHUSU TOVUTI (Web)
  Internet World Wide Web How to Program by Deitel  MABUKU KUHUSU HARDWARE

  Computer Architecture - A Quantitative Approach L.Henessy nd D. A Patterson

  Computer Organization and Design
  D. A. Patterson and J. L. Hennessy.pdf

  Upgrading and Repairing_PCs -_Scott_Mueller
  [​IMG]katika mambo ya kompyuta hardware buku hili au muandishi huyu anaongoza kwa Mauzo. Ameadika kitabu kaa hiki pia kwa ajili ya Laptop (Upgrading and Repairing Laptops). Scot Muller katoa pia video DVD zinazoyesha kwa vitendo yale yanazyozungumziwa kwenye vitabu vyake . "Edisheni" ya kitabu hiki niliyono ni ya 20.

  Bado chapisho linaendelezwa....... na linapatikana pia kwenye Gym ya mtazamaji
   
 2. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Vitabu vingine vya ICTvizuri kwa sef study vinakwenda kwa kibwagizo cha SAM teach yourself..............

  Mfano
  kwenye web kipo ia title ya Sams Teach Yourself HTML and CSS in 24 Hours. ( Size 8 MB) hiki cha SAM kinafanana fanana mtiriko wake ni hiki cha Teach Yourself Visually HTML and CSS ( size 90 MB)

  Vitabu vingine vya SAM's

  Programming SAMs Teach yursef C++ in 24 hours. Ni kizuri kwa begginers
   
 3. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,741
  Likes Received: 1,748
  Trophy Points: 280
  Bei gani
   
 4. qq.com

  qq.com JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 9, 2012
  Messages: 370
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  umenisaidia sana mkuu
  kesho naongeza fedha kunako moderm nishushe vitu,wengine tunasoma bila vitabu safi sana mkuu
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kama unataka Paper Book/Hardcopy nenda amazon u google books utakuta vipya na used ,lakini vingi niivyoandika hapa bei yake ni MB za interent yako tu kwani vinapatikana kama e-book/softwcopy sehemu mbali mbali. Si unoana vingine nimeweka hata viunganisho vya kupakua.

  Ni buku gani unataka kwani?
   
Loading...