Vitabu vya dini visitumike kuwaapisha wanasiasa!

Vitabu vya dini visitumike kuwaapisha wanasiasa!

Dini ni rubber stamp tu.Kwani kiuhalisia nani anaendesha maisha yake ya kila siku kwa kufuata maelekezo ya dini yake?.Wanasiasa ni zao la jamii hii hii iliyojaa unafiki.
Sisi wengine hatujawahi kuapa kwa kutumia vitabu vya dini!! Siyo kila mwanadini anaapa ili kuwa muumini wa dini husika!!
 
Viwatu vyenyewe vinaapishwa ni viongo viongo hadi ukweli umesha vikimbia,rushwa asubuhi ufisadi jioni,akiapishwa anaaaaapa huku ametoa macho utasema fundi saa kapoteza mshale wa sekunde.
 
kwanza itawasaidia sana wana siasa,maana wanaapa kwa jina la Mungu kwamba watalinda nakutetea katiba kumbe sio in reality.DHAMBI
 
Kweli kabisa Mkuu..
Kwa mfano huyu jamaa alipaswa kuapishwa akiwa amekumbatia SMG.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] daaaaah
 
Na pia viongozi wa kidini wasiwe wanaitwa kuongoza sala kwenye shughuli za kiserikali kama kumuapisha rais maana hapo dini na siasa vinakuwa vimeingiliana kabisa hapo

Na tusione viongozi wa kisiasa wakihutubia kwenye nyumba za ibada siku za sikukuu kama Pasaka na nyinginezo na tusioneshwe kwenye vyombo vya habari picha zao wakiwa kwenye ibada maana hatutaki watuchanganyie siasa na dini
 
Kwa muda mrefu nimeona kunakuwa na mgogoro mkubwa sana miongoni mwetu kwenye kukubaliana hasa ni wakati gani siasa na dini vinaweza kukaa pamoja. Ili kuondoa sintofahamu hiyo nashauri vitabu vya dini visitumike kumwapisha mwanasiasa yeyote yule ama mwanasiasa asitumie vitabu vya dini kumwapisha mtu mwingine.

Tusichanganye siasa na dini!!
Ni kweli sababu siasa si hasa,
 
Kuapa ni lazima kwa neno la Mungu kupitia vitabu vitakatifu vya Mungu,kwa kua hekima ya binadamu inatokana Na Mungu,kama mtu ataapa akatenda kinyume hiyo sio shauri ya binadamu yeyote ,ni shauri laMungu na hukumu ni ya Mungu.
kuapa sio lazima utumie neno la Mungu kuna watu hawana imani juu ya Mungu ndo maana mwl akasema kuwa wakichagua mtu ambaye haamini dini watatafuta namna ya kumuapisha.....
katiba ibara 19 inatoa uhuru wa kuabudu.......kuna wapagani nk
ukichagua mtu asiye na dini lazima utafute means ya kumuapisha na sio hii ya biblia n quran
 
Back
Top Bottom