Vita ya madawa ya kulevya imeacha majeruhi!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Kwenye TV channel ya Aljazeera walikuwa na msemo usemao, There is nothing good in wars, except its end! Yani, hakuna mazuri kwenye vita isipokuwa mwisho wake.
Vita hii ya madawa ya kulevya imeacha majeraha makubwa sana katika taifa letu, hasa ukizingatia kuwa waliohusishwa kwenye vita hii ni public figures wenye wafuasi.
Manji ana wafuasi, hata pale mahakamani kulionekana kumejaa watu ambao walikuwa na sympathy naye,
Gwajiama ana wafuasi,
Wema ana wafuasi,
Makonda naye ana wafuasi
Mbowe naye ana wafuasi...
Ni dhahiri kwamba wote hawa na wengine ambao sijawataja ambao waliingia kwenye vita hii wameachwa na majeraha ambayo yatachukua mda mrefu kupona.

Kwa vita ilipofikia inabidi sasa kila mmoja aweke silaha chini. Huu uwe ni wakati wa kutafuta suluhu na suluhisho juu ya madawa kwa njia ya kidiplomasia...
 
Hili nalo linapotea taratibu yaleyale likianza kupotea kabisa litaibuliwa lingine TANZANIA nchi yangu.
 
Kwenye TV channel ya Aljazeera walikuwa na msemo usemao, There is nothing good in wars, except its end! Yani, hakuna mazuri kwenye vita isipokuwa mwisho wake.
Vita hii ya madawa ya kulevya imeacha majeraha makubwa sana katika taifa letu, hasa ukizingatia kuwa waliohusishwa kwenye vita hii ni public figures wenye wafuasi.
Manji ana wafuasi, hata pale mahakamani kulionekana kumejaa watu ambao walikuwa na sympathy naye,
Gwajiama ana wafuasi,
Wema ana wafuasi,
Makonda naye ana wafuasi
Mbowe naye ana wafuasi...
Ni dhahiri kwamba wote hawa na wengine ambao sijawataja ambao waliingia kwenye vita hii wameachwa na majeraha ambayo yatachukua mda mrefu kupona.

Kwa vita ilipofikia inabidi sasa kila mmoja aweke silaha chini. Huu uwe ni wakati wa kutafuta suluhu na suluhisho juu ya madawa kwa njia ya kidiplomasia...

Serikali bado inabidi iendelee kukamata wasanii wa bongofleva, Ridhiwani Kikwete, Kinjeketile Mwiru, Jo Kusaga, Ruge Mutahaba, na wababaishaji wengine.
 
Back
Top Bottom