Vita ya kiuchumi nini maana yake

Mr faru john

Senior Member
Dec 22, 2016
173
298
Mara moja ukitizama jinsi mambo yanavyo elekea Tanzania utabaini hayayote si kwa bahati mbaya ila ni makusudi ya jumla jumla.

Kulingana na takwimu,uchumi wa Tanzania kama nchi unakuwa kwa kasi ya mwanga wakati uchumi wa mtanzania mmoja mmoja unadondoka kwa haraka sana(centralized government),hiii huingilia maslai ya watu wengi sana mfanyabiashara mtanzania, wafanyabiashara wa nchi marafiki, nchi marafiki, taasisi mbalimbali wote mwenye maslai ya kufaidika na nchi tanzania, nchi kama nchi,sasa ukitumia nguvu kubwa kuaminisha (central government)kwa vitendo vya wazi wazi,watu wote hugeuka maadui,

Serikali inakwendwa kuwa na maadui wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania,maadui wa Tanzania vijana mwenye nguvu ambao hawana ajira,maadui taasisi mbali mbali ndani ya Tanzania na zile za ng'ambo zenye ushawishi wake hapa Tanzania sasa hapa kama kuna nchi marafiki ambao hawapendi kuona maendeleo ya Tanzania ni rahisi sana kupenyeza ushawishi wao na kufanya chochote kwa mshtuko wa hatari.

Je, ni kweli ndani ya Tanzania kuna watu wanaonekana kama maadui?

Na kama ni maadui ni kwasababu maslai yao yameguswa,au katika harakati za kubadili mfumo nao wameathiriwa,je tutegemee nini?

Vita ya uchumi ni vita ya kiakili sana inayo hitaji hekma ya hali ya juu kwani tunaweza tukawa wamoja katikati yetu wakatokea ambao huonekana hawafai si kuwapaka matope na kukejeli la.

Hekma itumike kuweka mambo sawa na kusonga mbele

Upepo unavyo enda ni hasara kwa mama Tanzania, vidonda hivi kwa kivuli cha vita ya uchumi vitaligharimu Taifa

Vita hii isiwe dhidi ya walio Nazo(fedha na biashara,taasisi)kwa kivuli cha wasio navyo(wanyonge)
Tutengeneze maelewano ili walionavyo wasaidie wasio navyo.

Hapo vita hivi kwa kiasi twaweza pambana navyo.
 
Back
Top Bottom