Vita ya kiuchumi inapiganwa wapi?

Vita ya kiuchumi inapiganwa wapi?

mzee wa kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
947
Reaction score
690
Inapiganwa wapi hii vita? nataka kujiunga ili na Mimi nitoke kimaisha.
Sasa kinachonitatanisha Nikae upande upi? Wa wenye nazo au upande Wa wasionacho? Upande Wa wenye nacho Hawana maneno wao ni vitendo tuu na kweli wanazidi kufanikiwa, naona huu upande ni mzuri isipokuwa hawatanikubali maana Mimi ninaongea sana.

Upande Wa wasionacho Ndio upande ninaostahili kiukweli. Huku maneno,vitisho,wivu usipime utafikiri tutashinda kesho asubuhi.
Tupo wengi sana hatubaguani isipokuwa adui wetu mkubwa ni mtu au watu waliofanikiwa na wanaowashabikia.

Swali ninalojiuliza ni je nasisi tukifanikiwa siku moja adui yetu atakuwa nani ? Je huyu aliyefanikiwa na yeye hapo kabla sii alikuwa upande huu wetu Wa walala Hoi?

Chuki dhidi ya waliofanikiwa zitasaidia mafanikio yetu?
Mbona Mimi naona tofauti? Tunatakiwa kuwa rafiki Wa waliofanikiwa tujifunze leão.

Vita ya kiuchumi ni muhimu ipiganwe baada ya kuoanisha maadui Wa umaskini wetu. Ninaamini adui Wa maskini sii tajiri bali ni umaskini wenyewe.

Tajiri ni mtu aliyeushinda umaskini na wala sii mtu aliyemshinda maskini.

Tuondoe chuki dhidi ya matajiri kama tunataka kufanikiwa.

Hakuna mtu hakuna Taifa duniani lililofanikiwa kwa kupigana na matajiri.

Historia ya nchi yetu kiuchumi ipo wazi sana, tuliamua kuchagua kushirikiana na maskini toka Mwanzo na tulivuna umaskini Wa kutosha (socialism)

Mzee Mwinyi, Mkapa,Kikwete walifanya maamuzi magumu, waliamua kurudi upande Wa matajiri (capitalists) na Matokeo Yale Leo tunamatajiri na utajiri ambao hatukuwa nao.

JPM anasema tumekosea, anasema tupigane nao, sijui kama watanzania wamejiandaa kwa mambo haya:-
Kupiga foleni Kununua unga,sukari nk
Kuvaaa jinja na Nguo za Mwatex,kilitex,nk
Kutumia Umeme usiku tuu
Mafuta ya Magari kwa mgao????

Kisingizio hiki kinachoitwa vita ya kiuchumi imemweka madarakani Robert Mugabe Hadi amezeeka, Mseveni aliingia kwa jina lá mkombozi Wa uchumi Hadi sasa hataki kuondoka maana adui hajakimbia.

Magufuli anapigana na kivuli chake???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mtu anayepingana na utajiri wa mtu ambaye ameutafuta kwa jasho lake mwenyewe.....

Dunia nzima inapambana utajiri uliopatikana kwa njia haramu kwa sababu utajiri wa aina hiyo huwa unadhurumu haki za wengine.......

Pablo Escobar ni mtu tajiri sana lakini ameandamwa na vyombo vya usalama mpaka amekamatwa sio kwamba watu wanachuki na utajiri wake bali wanachukia vyanzo vya utajiri wake.......

Hata hapa kwetu matajiri wengi wamecheza rafu sana hadi kufikia hapo....wamedhurumu haki za wengi kwa manufaa yao.....je watu kama wanapaswa kuheshimiwa.......

Marehemu Ndesamburi ni mtu mwenye mafanikio lakini haijawahi kusikika kwenye kashfa yoyote ya ubadhirifu au ufisadi..........

Tunawapenda matajiri lakini wawe matajiri wenye manufaa kwa wote kutokana na utajiri wao.....sio matajiri wanaotuibia rasilimali zetu na kuzihifadhi nje......
 
" Tajiri ni mtu aliyeushinda umasikini na wala sii mtu aliyemshinda masikini"

Hiyo ni strong point kuliko maneno yote uliyoandika...

Wanaema " If you cant beat them, join them" umasikini ni fikra, lakini hakuna masikini, ukipambana unafanikiwa...


Cc: mahondaw
 
Hakuna mtu anayepingana na utajiri wa mtu ambaye ameutafuta kwa jasho lake mwenyewe.....

Dunia nzima inapambana utajiri uliopatikana kwa njia haramu kwa sababu utajiri wa aina hiyo huwa unadhurumu haki za wengine.......

Pablo Escobar ni mtu tajiri sana lakini ameandamwa na vyombo vya usalama mpaka amekamatwa sio kwamba watu wanachuki na utajiri wake bali wanachukia vyanzo vya utajiri wake.......

Hata hapa kwetu matajiri wengi wamecheza rafu sana hadi kufikia hapo....wamedhurumu haki za wengi kwa manufaa yao.....je watu kama wanapaswa kuheshimiwa.......

Marehemu Ndesamburi ni mtu mwenye mafanikio lakini haijawahi kusikika kwenye kashfa yoyote ya ubadhirifu au ufisadi..........

Tunawapenda matajiri lakini wawe matajiri wenye manufaa kwa wote kutokana na utajiri wao.....sio matajiri wanaotuibia rasilimali zetu na kuzihifadhi nje......
Tajiri Ana fikra pevu ambazo masikini anaweza kuwa nazo pia, tofauti ni hatua ujasiri au uthubutu kitu ambacho masikini wengi hawana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ya maskini ni kupeleleza utajiri Wa matajiri ili kukosoa njia au jinsi ulivyopatikana, hii nayo inadhihirisha chuki za maskini dhidi ya matajiri, Matajiri wengi wanajua hizi chuki dhidi Yao, na Ndio mana wengi huwachunia maskini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inapiganwa wapi hii vita? nataka kujiunga ili na Mimi nitoke kimaisha.
Sasa kinachonitatanisha Nikae upande upi? Wa wenye nazo au upande Wa wasionacho? Upande Wa wenye nacho Hawana maneno wao ni vitendo tuu na kweli wanazidi kufanikiwa, naona huu upande ni mzuri isipokuwa hawatanikubali maana Mimi ninaongea sana.

Upande Wa wasionacho Ndio upande ninaostahili kiukweli. Huku maneno,vitisho,wivu usipime utafikiri tutashinda kesho asubuhi.
Tupo wengi sana hatubaguani isipokuwa adui wetu mkubwa ni mtu au watu waliofanikiwa na wanaowashabikia.

Swali ninalojiuliza ni je nasisi tukifanikiwa siku moja adui yetu atakuwa nani ? Je huyu aliyefanikiwa na yeye hapo kabla sii alikuwa upande huu wetu Wa walala Hoi?

Chuki dhidi ya waliofanikiwa zitasaidia mafanikio yetu?
Mbona Mimi naona tofauti? Tunatakiwa kuwa rafiki Wa waliofanikiwa tujifunze leão.

Vita ya kiuchumi ni muhimu ipiganwe baada ya kuoanisha maadui Wa umaskini wetu. Ninaamini adui Wa maskini sii tajiri bali ni umaskini wenyewe.

Tajiri ni mtu aliyeushinda umaskini na wala sii mtu aliyemshinda maskini.

Tuondoe chuki dhidi ya matajiri kama tunataka kufanikiwa.

Hakuna mtu hakuna Taifa duniani lililofanikiwa kwa kupigana na matajiri.

Historia ya nchi yetu kiuchumi ipo wazi sana, tuliamua kuchagua kushirikiana na maskini toka Mwanzo na tulivuna umaskini Wa kutosha (socialism)

Mzee Mwinyi, Mkapa,Kikwete walifanya maamuzi magumu, waliamua kurudi upande Wa matajiri (capitalists) na Matokeo Yale Leo tunamatajiri na utajiri ambao hatukuwa nao.

JPM anasema tumekosea, anasema tupigane nao, sijui kama watanzania wamejiandaa kwa mambo haya:-
Kupiga foleni Kununua unga,sukari nk
Kuvaaa jinja na Nguo za Mwatex,kilitex,nk
Kutumia Umeme usiku tuu
Mafuta ya Magari kwa mgao????

Kisingizio hiki kinachoitwa vita ya kiuchumi imemweka madarakani Robert Mugabe Hadi amezeeka, Mseveni aliingia kwa jina lá mkombozi Wa uchumi Hadi sasa hataki kuondoka maana adui hajakimbia.

Magufuli anapigana na kivuli chake???

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah...Umejichanganya kwelikweli...haihitaji digrii ya maneno mengi ili uelewe......kwa urahisi kabisa....Ni vita ya wazalendo dhidi ya wapiga dili/wezi wa mali ya umma....😎😎
 
Back
Top Bottom