sonaderm
JF-Expert Member
- Nov 9, 2015
- 618
- 1,817
Habari wadau..
Kwanza nianze kwa kukiri mimi ni mpenzi sana wa muziki wa bongofleva ila kuna kitu kinachoendelea naona huko mbele kutakuwa na giza kwa wasanii wetu wa bongo!
Katika ulimwengu wa sasa kibiashara, ushindani ni kitu muhimu ukikaziwa na ubunifu..Sasa hizi media zetu za Tanzania wanaushindani ambao utawaumiza sana wasanii wa bongo hasa kimaslahi na umoja..
Kila kukicha tumesikia vita ya kibiashara kati ya Radio clouds na EA radio, Clouds na EFM n.k..Vita hii ya kibishara si mbaya ila pale inapomgusa msanii kutopigiwa nyimbo zake kisa amekosana na watu flani si sawa hata kidogo..Au msanii anayesikika radio fulani, hatakiwi kusikika radio pinzani..Hapo wanakosea sana..
Chanzo kingine cha Tatizo hili ambalo linaelekea kuumiza wasanii ni pale Clouds au watangazaji inapowasimamia wasanii flani..Hii si kitu kizuri hata kidogo maana watawapendelea wasanii wao kwa maslahi yao, vivyo hivyo kwa radio zingine. Kitu ninachopendekeza wasanii wangetakiwa kuwa na menejiment ambazo ni independent au zisifungamane na radio au media yoyote..Kwa style ya kuwasimamia wasanii na kupiga nyimbo zao kwa kutumia kampuni ile ile au washirika wale wale, inaleta mgawanyo wa kimaslahi na wasanii lazima wawe kwenye madaraja na kutengana..Maana wale wanaopewa promo na hiyo radio au media watajiona wako juu kumbe wanabebwa na kampuni wakati wenye vipaji vyao wakiminywa kidizaini.Noma sana!
Ni wakati sasa hizi media zisiwagawe wasanii kwa kisingizio cha kuwasimamia au maslahi yao kibiashara, waachwe wawe independent hata kama hizo media zina compete kwenye biashara, pili wasanii waachwe huru kwenye maamuzi ya maslahi yao na si kushurutishwa!Ninamaanisha msanii anakuwa huru ku negotiate bila aibu wakati wa show na matamasha yanayoandaliwa na hizo media..Na wanaposhindwana asichukuliwa kama adui, nyimbo zake zipigwe tu!Kwani Tatizo ni mziki wake au maslahi yake?
Hizi media na watangazaji waachane na mambo ya kuwasimamia wasanii maana italeta conflict of interest na mfano mzuri ni issue ya dada yetu Jide na Ruby..Pia ifike mahali wasanii nao wajitambue, wamezidi kulia lia wakati hawana ushirikiano linapokuja suala la maslahi yao..Its the time wanatakiwa kuwa free na kuamini kwenye vipaji vyao na si kubebwa au promo kupitia kituo fulani cha radio au runinga!Wajiamini..Mbona engineer anaposhindwa maslahi au kukosana na kampuni fulani hatengwi?Kwa nini wasanii?
Huko kwa wenzetu hakuna cha kusimamiwa na maredio au maTHT yenu, mtu anatoka from hood au kitaa na anatusua tu vizuri to the world, hiki kitu naona kipo Tanzania pekee, yaani bila kupitia kwa vituo fulani hautoboi..Mfano mzuri ni huyu dogo kwenye picha, anaitwa Young Ma hajasainiwa na lebo yoyote na wala hajabebwa na radio yoyote lakini anatesa kimataifa from hood.