Vita vya fahari wawil | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita vya fahari wawil

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by oba, Jun 29, 2012.

 1. oba

  oba JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimefuatilia sana mgogoro uliopo kati ya serikali na madaktari na kugundua kuwa;
  1. wakati madaktari wana madai yao kwa serikali kutekeleza yenyewe inafanya kila mbinu kuyazuia madai hayo na kufanya yasitekelezeke.
  2. Wakati mgogoro huo unaendelea ni watanzania maskini wanaoumia kwa kukosa huduma za afya, na bahati mbaya ni wachache kati ya hao wanaojua kwa undani kiini cha mgogoro huu achilia mbali wale waliodanganywa na vyombo vya habari vya serikali wakati ikifanya propaganda za kuwazima madaktari
  3. ni raia wachache sana wanaojua mgawanyo wa majukumu ya kutoa afya kwa jamii, wachache sana wanajua kuwa ni wajibu wa serikali ( na siyo madaktari) wa kutoa huduma ya afya kwa watanzania. Madaktari wanatumika tu kama house boy kuhakikisha ng'ombe ( wananchi ) wa baba mwenye nyumba wamekula na kunywa maji. Endapo baba mwenye nyumba hajaacha miundo mbinu ya chakula cha ng'ombe nisahihi kumlaumu houseboy kwamba hajafanya kazi yake?

  Ushauri;
  Wananchi waingie barabarani kumshinikiza baba mwenye nyumba (rais na serikali yake ) kuwapa chakula (matibabu)!!!!!!!
   
Loading...