Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,462
- 32,985
MAREKANI IMETENGENEZA MPANGO WA KUMALIZA VITA VYA IRAN NA ISRAEL
Baada ya saa 24 In Shaa Allah vita baina ya Iran na Israel In Shaa Allah vita kuwa vimemalizika.
Vita vimedumu kwa siku 12.
Hizi siku 12 mimi binafsi nimejifunza mengi na si kwa mwalimu kunisomesha darasani bali kwa kushinda, kulala na kuamka katika mitandao ya Kijamii.
Kumalizika kwa vita hivi hili ni jambo kubwa na la kushukuriwa.
Vilipoanza vita mitandao ya kijamii hapa nyumbani ilijaa chereko chereko furaha na vifijo.
Nini lilikuwa kinafurahiwa?
Furaha hiyo ilitokana na kushambuliwa vibaya Iran na kuuliwa kwa wataalamu wake muhimu katika Nuclear na viongozi wake katika jeshi.
Iran ikaingia vitani.
Haukupita muda vita vikanoga kwani kulikuwa kunaliwa kote kwa mwalimu na kwa kungwi.
Taratibu nderemo zikawa zinapungua haziandikiki tena kwani rundinga zilikuwa zinaonyesha Tel Aviv na Haifa inayofanana na Ghaza.
Nyoyo za washangiliaji ziliumia.
Macho yao hayakuweza kuamini walichokuwa wanashuhudia.
Miji ya Israel ilikuwa ikiangamizwa kwa makombora.
Tehran inapigwa na Tel Aviv inapigwa.
Furaha mitandaoni ya kufurahia kupigwa kwa Iran ghafla ikatoweka na pakawa na utulivu na ukimya mkubwa usio na kifani.
Hata Marekani ilipoingia vitani kuisaidia Israel paliendelea kuwa na ukimya mitandaoni.
Wapiga vigelegele waliinamisha vichwa vyao kwa fadhaa kwani walikuwa washaijua tafsiri isiyo na shaka ya kitendo hicho.
Kitendo hicho kilidhihirisha ukweli kuwa Israel imeelemewa haina uwezo wa kupambana na Iran.
Vyombo vikubwa vya habari duniani vikawa vinauliza endapo Iran itapambana na Marekani kulipiza kisasi.
Jibu limetolewa tena kwa haraka.
Iran katika muda mfupi sana imepiga kituo cha kijeshi Qatar.
Marekani katika muda mfupi mno imetangaza kusitishwa kwa vita baina ya Iran na Israel.
Naamka usiku mkubwa natupia jicho Al Jazeera ndiyo nakuta "Breaking News."
Israel hii ambayo leo Wayahudi wanaamka na kurejea majumbani mwao na kuangalia barabara na mitaa yao ya Tel Aviv si ile waliyoiacha walipoingia katika sehemu za kujificha mabomu.
Tel Aviv imekuwa mfano wa Ghaza kwa magofu na kifusi.
Ukweli wa vita utawadhihirikia.
Wengi Wayahudi wamekimbia vita kupitia baharini kujificha Cyprus na kwengineko.
Wayahudi waliofanikiwa kukimbia na wale waliobakia nyuma wote wana kitu cha kujifunza katika vita hivi.
Vipi kuhusu Iran?
Wamarekani wanawatazama vipi Wairani?
Halikadhalika dunia inawaonaje Wairani?
Leo Israel ina lipi la kusema kuhusu Iran?