Vita italetwa na CCM

Vita italetwa na CCM

Mdaiwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2025
Posts
696
Reaction score
1,533
Watanzania wote tumejionea na tumekiri vita italetwa na ccm. Hizi propaganda zao za kuwauzia uoga wananchi kuwa upinzani utaleta vita ni vichekesho. Mmeona Samuya alivyobaka uchaguzi na kujishindisha kwa 98% lakini akiogopa kusherehekea ushindi wake na hao watu milioni 31 waliomchagua.

Uchaguzi haukufanyika maeneo mengi, na tumeshuhudia video nyingi wasimamizi wakitumbukiza kura fake kwenye maboksi ya kura. Sasa hapa ni dhahiri ccm ndio wataleta vita kwa sababu ya kung’ang’ania kututawala kwa hila na mbinu chafu. Wananchi wakigoma kutawaliwa kwa hila kama walivyofanya 29 October na kama inavyotarajiwa kufanyika 9 December maana yake ccm ndio wataleta vita na sio wapinzani.

CCM muda wenu umekwisha, watanzania hawawahitaji tena, msilazishe kututawala kwa nguvu, mtatuletea vita. Ondokeni kwa amani japo amani ya kuondoka nayo haipo tena maana tayari mmeua watanzania ambao hawakuwa na siraha ila nyie mmewaua kwa kutumia siraha nzito za kivita. Basi ondokeni hivyohivyo bila amani, mlipotufikisha na mliyotufanyia yanatosha. Msitupasulie nchi yetu na kutuangamiza zaidi ya hapa.
 
Back
Top Bottom