Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,028
- 828,818
Siku moja baada ya Israel kushambulia Iran siku ya Ijumaa, ndege ya mizigo ilipaa kutoka China.
Siku iliyofuata, ndege ya pili iliondoka kutoka mji wa pwani, Kisha Jumatatu, nyingine ikaondoka, wakati huu kutoka Shanghai - safari tatu za ndege kwa siku tatu.
Takwimu zilionyesha kuwa katika kila safari, ndege hizo ziliruka kuelekea magharibi kando ya kaskazini mwa Uchina, ikivuka hadi Kazakhstan, kisha kusini hadi Uzbekistan na Turkmenistan na kisha kupotea kwenye rada zilipokaribia Irani.
Ili kuongeza fumbo, mipango ya safari za ndege hizo ilionyesha kuishia Luxembourg, lakini zinaonekana hazikuruka karibu na anga ya Ulaya.
Kuna wasiwasi juu ya kile ambacho kinaweza kutumwa kutoka China kuelekea Iran wakati vita vya Tehran na Israeli vikiendelea.
Wataalamu wa masuala ya usafiri wa anga wamebainisha kuwa aina ya ndege inayotumika, Boeing 747, hutumika kwa kawaida kusafirisha vifaa vya kijeshi na silaha, na kukodishwa kuruka kwa amri za kandarasi za serikali.