Doppelganger
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,858
- 748
Ni serikali ya ccm chini ya uongozi wa J'K' unategemea nini kama sio u-K mwanzo mwisho!
Madai ya Daily Mail ni kuwa NYARA karibu zote zinazotoka nchini zilikamatwa nje ya nchi badala ya ndani.
Mheshimiwa Waziri kuonesha kuwa Daily Mail ni wazushi Katoa takwimu zifuatazo:
1.Katika miaka mitatu kuanzia 2010 hadi mwaka jana , jmla ya kilo19,943 sawa na tani 20 za meno ya tembo zilikamatwa nchini ambapo watuhumiwa 322 walikamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
2. tani 12.2 za meno ya Tembo zilikamatwa nchni mwaka jana pekee ambapo watuhumiwa 145 walitiwa mbaroni akiwamo raia wa Uingereza.
Nani mkweli katika hili Daily Mail au Waziri Nyalandu? Tuache kupiga mipasho humu jf kwa sababu tu eti habari imaeandikwa na chombo cha nje kwani inawezekana kabisa wametumiwa kuandika uzushi ili kuifedhehesha serikali. Nani hajui mahusiano kati ya Chama kinachoongoza uingerereza na baadhi ya vyama vya upinzani hapa nchini na hasa ukizingatia kuwa vyma hivyo vimepigwa mweleka na chama tawala kwenye uchaguzi mdogo wa Madiwani. Mimi naamini Dail Mail wametumiwa na Wafuasi wa CHADEMA walioko Uingereza kuifedhehesha serikali yetu. Ni kweli kuwa tatizo la ujangili ni kubwa siyo Tanzania tu bali nchi nyingi za kiafrika, lakini siyo sahihi kutoa taarifa za kizushi kiasi hiki.
adolay, don't waste your time. The guy can't speak English, unless he responds to you with a support from his cohorts.
You can read his posts and discover that, his is being used. If he had a bit of brains, he could be able to differentiate between matters of national interests and those of political mileage.
watanzania tumelala sana. Daily mail wamelishwa maneno na Makamanda wa CHADEMA walioko U.k ili kumfedhehesha Rais kwenye mkutano ulioitwa na Mwana mfalme sisi tunarukia kushabikia, mbona hawakuandika zamani?[/QUOTE
Kaka mbona unaleta utetezi wa kipuuzi..mimi ni ni mwachama wa CCM kama ulivyo wewe lakini linapokuja suala la ustawi wa rasilimali zetu hakuna unazi yapo kabisaaa. Hapo sijaona utetezi wowte wa maana wa Waziri ati. Kuna kipindi mtandao mmoja wa mareiani walitoa taarifa ya utafiti juu ya uwepo wa bandari kavu kibao zinashusha madawa ya kulevya na huwa yanasindikizwa na magari ya vyombo vya usalama lakini ikakanushwa kwa kudai serikali iko makini lakini wapi madawa yanakatwa kutoka Tanzania na mengine hapa hapa DSM lakini hakuna hata mmoja ktk mtandao aliyekamatwa. Ndio maana kwa sasa wanaamua kufuatilia wauza unga toka nje ya nchi majeshi ya wahisani na kuyaangaiza wenyewe sababu hatuaminiki.
Kukamata vikilo 200 hivyo ataamka mwanansiasa mzigo ajisifu tunapigana kuvunja mtandao..hakuna kitu hapo. Waziri anazungumzia tu meno ya tembo yaliyokamatwa tu lakini yale ambayo yanapita na kwenda kutengenesha hayo mapambo sijui tunayajua na yalikuwepo kwenye takwimu!! TUusitumie takwimu tu zinazoonekana wakati zile ambazo hazijaonekana zipo na tembo wanateketea. Katika hili kwa kweli sio CHADEMA CUF au hata shetani nitamuunga mkono akizungumzia ushenzi huu. Serikali haina namna kukwepa lawama sababu rushwa tuliamua kuvunja azimio wana CCM wenyewe ili tumalize mali asili zetu tubaki tunatazamana tu kama maboga..PATHETIC
Wamejikanyaga sana. Wametumia nguvu kubwa sana kujibu gazeti la udaku...
Wanasema raisi pekee ndio anamamlaka ya kutumia jeshi...sasa kwanini raisi kupitia Pinda aliwatimua mawaziri wa mambo ya ndani , ulinzi etc???? Au ndio kusema kamati ya wabunge wa ccm walipewa maagizo kulaumu mawaziri tu...ili Kikwete aonekane msafi nje?
Wamesema kuhusu kuuza meno ya tembo yaliokamatwa, ccm haielekezi serikali
Wapi pakupata pesa ya uchaguzi..... Rais Kikwete amesahau ameingia vipi Ikulu???? Hakumbuki wakina Rostam wasio na wadhifa serikalini bali waweka hazina wa chama waliagiza serikali itoe pesa za EPA kwa ajili ya uchaguzi wa ccm na kikwete. Na lilipolipuka serikali kupitia MEGHJI walikana kabisa kuwepo kwa huo wizi. Baadae wakasema ni siri za serikali, mara siri za jeshi...eventually ndio tukapata picha ya KAGODA....bado mnataka tuamini ngonjera mlizoandika hapo juu???
Kila siku tunaona wanaokamatwa kwenye madawa ya,kulevya, ujangiki etc...hata Hosea alimwanbia ofisa wa ubalozi wa marekani...Kikwete hataki kushugulikia wazito.juzi juzi..mkuu wa kikosi cha madawa ya kulevya amefunga safari kwenda south africa kuhakikisha mtuhumiwa kutoka tanzania anapata dhamana na arudishwe tanzania...jamaa huyo huyo alishalalamikiwa na Mengi live kwenye TV akihusika kumbambikia mtoto wake madawa ya kulevya.
Serikali yetu imezoea kuwa inashitaki na kuhukumu magazeti na kuyafungia..baadala ya kuyapeleka mahakamani, kuwasilisha ushahidi ili mahakama iamue kama kweli gazeti limefanya kosa..sasa kwenye hili wanepanic...
Rais Kikwete akitaka aaminike aweke effort kwenye intelligence.. Kamata viongozi wa hii mitandao... Wengi ni watu wakaribu sana na chama na serikali.... Kutoa statistics zinazoonyeha mmekamata wanavijiji wakiwinda wanyama au walalahoi wamebeba unga nimchezo wa kitoto.
Mnasema mmewekeza pesa nyingi kupambana na ujangili etc....hata kwenye budget za matumisi ya serikali mnaongeza ma billions kila mwaka, mpaka wakina Jairo wanaagiza mashirika kuchabga 50m each ili wabunge wahongwe budget ipite...kisa??? Zipatikane pesa za maendeleo au za kula viongozi wa chama na serikali..??? Reports za CAG zina majibu.. Zifanyie kazi..