Ni muhimu tujiadhari na watu kama kina Marando ambao licha ya kwamba wana ujuzi wa kisheria bado wanadai katiba haina haja ya mabadiliko!Ni Nyaucho huyu huyu aliyeu uwa upinzani wakati wa vurugu zake na Mrema huko NCCR-Mageuzi..na baadae kupewa madaraka na CCM...na sasa kutumia taaluma yake bila msimamo kwa kuzungumza maneno ambayo si rahisi kujua kama ni mpinzani ama CCM lakini ni mwenye kujali tumbo tu!Kama yeye na kina Lamwai!Hatutaki walete vurugu!Kwani wao wamesha expire na sasa tuna wakina tundu lissu na kina Slaa upande wa upinzani na watu wengine wenye nia nzuri na wazalendo ambao bado wamebaki kwenye mtego wa chama bila ya kujua kuwa ni hatua gani waichukue!Tunawatakia kila la kheri..either kufanya mabadiliko makubwa ndani ya chama chao..ama kujiunga na wapinzani na kuleta chachu ya uwajibikaji na maendeleo!Marando yeye akae pembeni kwanza!Akizungumza kuhusu madai ya kuwepo kwa mabadiliko ya katiba, alisema hayatasaidia kubadili matokeo ya chaguzi zinazofanyika hapa nchini kwa sababu wizi wa kura katika chaguzi mbalimbali utaendelea kwa kuwa serikali hutumia zaidi fedha ili kushinda.
Alisema, vyombo vya usalama wa taifa kwa kushirikiana na serikali vinaongoza kuiba kura ili kukisaidia chama kilichopo madarakani kiendelee kutawala.
Marando aliwataka wanasiasa wa kambi ya upinzani kufahamu kuwa suala la wizi wa kura kwa serikali iliyopo madarakani si jambo la kushangaza tena, hivyo hoja za msingi kwa vyama vya upinzani ni kujipanga na kujadili mbinu thabiti za kukabiliana na wizi huo.
Aidha, alivitaka vyama vya upinzani kuwa na hoja nzito zitakazokubalika kwa wananchi ili kuwajengea imani badala ya kudai kuendelea kulilia katiba mpya ama mabadiliko ya sheria.
Vyama vya upinzani tusikate tamaa kwa kuibiwa kura, suala hapa ni kujipanga kwa kuwa na hoja nzito ili kuweza kufanikiwa katika chaguzi zijazo, alisema.
Sio hoja dhaifu kwasababu Marando alishiriki kikamilifu kuumaliza upinzani yeye na Lamwai kwa kutumia usomi wao..hawakutaka kuwa upande wa haki..na ndio maana wamelipwa fadhila!Marando akapewa ubunge wa East Africa kwa kura nyingi za CCM huko bungeni dhidi ya kura chache za upinzani ambao waliona kuwa ni msaliti!Mimi sina chama ila ninaamini kuwa upinzani na utofauti wetu wa kimawazo ni namna za tofauti na mitizamo ya tofauti ya namna ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo na sio kuwa wajali matumbo na mafuska wa kisiasa kama walivyoonyesha Marando na mwenzake Lamwai!Ni kweli ni hoja dhaifu
Katiba ni lazima ibadilishwe kama kweli tunataka viongozi wawe wawajibikaji na maslahi ya taifa kusimamiwa kikamilifu na mwananchi wa kawaida kulindwa na katiba hiyo!Kwa maoni yangu hivi sasa siasa za vyama zinawekwa mbele zaidi ya maslahi ya taifa!Maamuzi magumu yanayowagusa raia wote bila kujali itikadi zao hayahitaji mwongozo wa chama..bali mwongozo wa katiba!Ni wakati wa kuiangalia katiba ya nchi yetu ambayo ndio kimbilio la mwisho la myonge!kutumia katiba inayomlinda kudai haki na mabadiliko!JMushi,
Katika dunia ya leo hakuna haja ya kuogopa mawazo tofauti cha msingi ni kujadili hoja kwa kueleza yale unayodhani ni kwanini katiba ibadilishwe na si kuhadharisha watu na kina Marando.
Hoja yako hii ni dhaifu sana.
Wanatayarishwa/Kujitayarisha..wanaanza kujipanga ili kuleta tafrani nyingine ambayo itapelekea nothing to be done!Wanaibukia kipembeni pembeni ili kuanza kujikita mawazoni mwa wananchi!wanaona kuna ulaji zaidi unakuja kwenye hayo makesi ya ufisadi!Usishangae akiwa anajipanga kwenye timu ili na yeye aendelee kulijaza tumbo!na Lamwai we subiri tu utamsikia!So ndio maana natoa taadhari kwasababu anaanza kuyapima maji!Halafu Tanzania Daima inadiriki kumpa cheo cha uasisi wa upinzani?!KWA MAONI YANGU MABERE NYAUCHO MARANDO NI MWENYE MURDER CASE YA UPINZANI!AKAE MBALI NA AENDELEE KULIJAZA TUMBO LAKE KWENYE HUO UBUNGE ALIOPEWA NA CCM..NA AWAACHE WAHANGA WAIPIGANIE NCHI YAO!damn this puppet amerudi tena?the guy is dishonest to the core na politician kama huyu is like a poison in any democracy,hawa ndio wameweka base ya siasa za kitapeli Tanzania na ndio maana tuna suffer
Binafsi sina sababu ya kumwogopa Marando et al,Kwani Marando kapewa cheo gani tena kwenye chama cha kijani mpaka tujihadhari naye?Kama walivunja upinzani zamani zile basi ijulikane leo wana inji si bendera fuata upepo kwa kununuliwa kwa kuongwa kanga na kofia na fulana.Hata wasipobadili katiba tutapambana kwa silaha tulizo nazo.NO RETREAT NO SURRENDER
Kweli kabisa SingleD,
kuna haja gani ya kumuogopa Marando ambaye tayari yuko kijani kama kina Lamwai na wengine? Ngoja aseme anachopenda lakini for the rest of us maisha ni kwenda mbele.
You go to war with the army you have - Donald Rumsfeld
Kuwa kijani haina maana kwamba hawatakuwa na uwezo wa kuleta mikanganyiko kwa kauli zao tata ambazo zinaonyesha ufuska wa kisiasa kwa kuwa mguu mmoja nadani na mwingine nje..they're distractive and divisive evil forces able and ready to once again disrupt the freedom movement!Kwa kujidai kuwa wana sympathize na ku ushauri upinzani wakakti ni wao walioshiriki ku uua..hilo kwangu lina mashaka!Kweli kabisa SingleD,
kuna haja gani ya kumuogopa Marando ambaye tayari yuko kijani kama kina Lamwai na wengine? Ngoja aseme anachopenda lakini for the rest of us maisha ni kwenda mbele.
You go to war with the army you have - Donald Rumsfeld
Ni kweli kabisa mkuu Koba!Mrando amesahau kuwa wizi wa kura na wa wanasiasa ni kitu kimoja!KWANI NANI ASIYEJUA KUWA MARANDO ALINUNULIWA YEYE PAMOJA NA KURA?Akae pembeni asituletee kichefu chefu!Anajua sheria lakini bado ana yale mawazo ya kukandamiza haki za wananchi kwa maslahi ya tumbo lake!Mwasisi wa upinzani?!Marando..these guys must be kidding!...hakuna mtu anamwogopa marando ila asitupe lecture ya wizi wa kura wakati huo huo anatuambia tatizo sio katiba,wakati ukiangalia vizuri matatizo yote ya wizi wa kura yako rooted kutokana na hiyo katiba,marando njaa yake na tabia zake za kitapeli zilisaidia sana kurudisha nyuma upinzani.
Kuwa kijani haina maana kwamba hawatakuwa na uwezo wa kuleta mikanganyiko kwa kauli zao tata ambazo zinaonyesha ufuska wa kisiasa kwa kuwa mguu mmoja nadani na mwingine nje..they're distractive and divisive evil forces able and ready to once again disrupt the freedom movement!Kwa kujidai kuwa wana sympathize na ku ushauri upinzani wakakti ni wao walioshiriki ku uua..hilo kwangu lina mashaka!
Cheo alichopewa ni pale alipopigiwa kura za fadhila na wabunge wa CCM pale walipomchagua huko bungeni kuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye bunge la east Africa!Wapinzani wao walikuwa na chaguo jingine lakini CCM kwa kusaidiana na pandikizi lao Marando waliwazidi nguvu upinzani!
Ni wazi kuwa hawana nia nzuri popote pale wanapopeleka pua zao!
Kuhusu wizi wa kura ni kweli..lakini yeye haja qualify kutueleza kuhusu wizi wa kura!Yeye mwenyewe aliibwa ama alinunuliwa!sasa anataka kutueleza kuhusu wizi wa kura!Yeye ni mwanasheria mzuri tu..lakini he can't have it both ways!abaki huko aliko aendelee kula tu..nafikiri uanasheria na uzalendo ni vitu viwili proven to be far away from each other during this man's courier!Alichosema je kina ukweli?
Kuhusu wizi wa kura ni kweli..lakini yeye haja qualify kutueleza kuhusu wizi wa kura!Yeye mwenyewe aliibwa ama alinunuliwa!sasa anataka kutueleza kuhusu wizi wa kura!Yeye ni mwanasheria mzuri tu..lakini he can't have it both ways!abaki huko aliko aendelee kula tu..nafikiri uanasheria na uzalendo ni vitu viwili proven to be far away from each other during this man's courier!
Nisawa tu ila mimi nimefanya utafiti na uzoefu wa kisiasa unaonyesha kuwa anataka kurudi mawazoni mwa watu!Kumbuka makala hiyo imemtaja kuwa ni mwasisi wa upinzani!Hapo ndio nilipojua kuwa ana agenda maybe kamtumia mwandishi..lakini nia ya huyu jamaa siyo nzuri!Narudia tena jamaa anayapima maji na anajitayarisha kurudi kwenye ulingo wake wa kawaida wa divisive and destruction!Sawa tu tsikilize kwani ni haki yake kutoa maoni..lakini tahadhari ni lazima!Mimi nakubaliana nawewe katika hili. Labda kama ungeungana naye katika hoja yake na kisha umpinge yeye binafsi pembeni. Au wewe unaonaje?
Huyu Mabere Marando alikuwa mwanasiasa machachari sana nchi ya Tanzania ilipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Hivi yuko wapi siku hizi?
Ni nini kimemaliza umaarufu wake katika uwanja wa siasa hapa TZ?