jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 25,996
- 24,594
CCM wezi, adai Mabere Marando
na Prisca Nsemwa
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimezidi kutuhumiwa kuwa kinashinda chaguzi mbalimbali kwa kuiba kura.
Baada ya viongozi kadhaa wa kambi ya upinzani kutoa tuhuma hizo kwa nyakati tofauti, hususan baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, tuhuma za hivi karibuni zimetolewa na wakili maarufu hapa nchini ambaye pia ni muasisi wa mageuzi, Mabere Marando.
Akizungumza jana katika kongamano la kutathimini hali na mwelekeo wa vyama vya siasa kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya uchaguzi mkuu wa 2005, lililoandaliwa na Asasi ya Maendeleo Tanzania (TADIP), Marando alisema udanganyifu na wizi wa kura unaofanywa na CCM wakati wa uchaguzi, ni suala linalosababisha kuwepo kwa mchafuko wa kisiasa visiwani Zanzibar.
Marando ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Rorya kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, alisema bila kuwepo ukweli na uwazi wakati wa kuhesabu kura, CCM itaendelea kuiba kura na kupata ushindi usio halali jambo ambalo litazidisha mgogoro wa kisiasa hapa nchini, hasa visiwani Zanzibar.
Alitahadharisha kuwa mgogoro wa kisiasa Zanzíbar unahatarisha usalama wa wananchi wa visiwani humo na pia unachafua sifa nzuri ya Tanzania kuwa ni nchi yenye amani katika Bara la Afrika.
Alisisitiza kuwa, tuhuma zinazoiandama CCM kuiba kura za urais Zanzíbar hazina ubishi na kwamba viongozi wa serikali iliyopo madarakani wanatambua ukweli huo, lakini wanashindwa kuweka wazi.
Ni kweli kilichofanyika Zanzibar kipindi cha uchaguzi mwaka 2005 ni wizi wa kura, hakuna mtu ambaye anaweza kubisha na hata serikali inalifahamu hilo ila haiwezi kuwa wazi, alisema Marando.
Akizungumza kuhusu madai ya kuwepo kwa mabadiliko ya katiba, alisema hayatasaidia kubadili matokeo ya chaguzi zinazofanyika hapa nchini kwa sababu wizi wa kura katika chaguzi mbalimbali utaendelea kwa kuwa serikali hutumia zaidi fedha ili kushinda.
Alisema, vyombo vya usalama wa taifa kwa kushirikiana na serikali vinaongoza kuiba kura ili kukisaidia chama kilichopo madarakani kiendelee kutawala.
Marando aliwataka wanasiasa wa kambi ya upinzani kufahamu kuwa suala la wizi wa kura kwa serikali iliyopo madarakani si jambo la kushangaza tena, hivyo hoja za msingi kwa vyama vya upinzani ni kujipanga na kujadili mbinu thabiti za kukabiliana na wizi huo.
Aidha, alivitaka vyama vya upinzani kuwa na hoja nzito zitakazokubalika kwa wananchi ili kuwajengea imani badala ya kudai kuendelea kulilia katiba mpya ama mabadiliko ya sheria.
Vyama vya upinzani tusikate tamaa kwa kuibiwa kura, suala hapa ni kujipanga kwa kuwa na hoja nzito ili kuweza kufanikiwa katika chaguzi zijazo, alisema.
Aidha, alivishauri vyama vya upinzani kuelekeza nguvu zake vijijini ili kujiwekea misingi bora kwa wananchi wa huko ambao wengi wao ndio wapigakura.
Alisema, yaliyotokea Kenya wakati wa uchaguzi mkuu hadi kusababisha machafuko ni zaidi ya wizi wa kura na kuongeza kuwa uporaji wa kura uliofanyika Kenya ndio unaofanyika sasa Zimbabwe, mambo ambayo yanaweza kusababisha kuibuka machufuko yanayohatarisha maisha ya wananchi wa kawaida.
Naye Mhadhiri kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally, alisema tatizo la Tanzania si sheria wala katiba bali matumizi mabaya ya pesa za walipakodi wakati wa uchaguzi yanayofanywa na serikali.
Tatizo lipo kwenye uchaguzi, wagombea wote si wasafi hata kidogo, wanakuwa na matumizi mabaya ya pesa, wanawalaghai wananchi na hili nina uhakika nalo, alisema Ally. Katika mjadala huo, zaidi ya wadu 120 kutoka asasi mbalimbali, taasisi za serikali na vijana walishiriki. Huo ni mjadala wa tatu kufanywa na TADIP ambako mwaka jana ulizungumzia tathimini ya miaka 15 ya vyama vingi hapa nchini.