singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,538
VITA inayopiganwa sasa dhidi ya ufisadi ni muhimu sana na imeleta tija kubwa. Huo ni ukweli usio na shaka. Katika siku 30 za kwanza za utawala wa Rais Dk. John Magufuli.
Fedha nyingi ambazo zingepotea kutokana na ukwepaji wa kodi zimeokolewa na juhudi zinaendelea. Rais Magufuli ameokoa shilingi trilioni kwa kudhibiti ubadhirifu na ufisadi. Pia, kama sehemu ya juhudi hizo, wafanyabiashara wengine waliokwepa kodi wamepewa siku saba, ambazo sasa zinaelekea ukingoni, walipe kodi waliyokwepa.
Wananchi wana matumaini makubwa kuwa sasa ufisadi na rushwa vinakwisha. Na mimi ninayo matumaini makubwa, lakini pia nina shaka. Wananchi wamekuwa tukijiuliza, serikali za awamu zilizopita zilikuwa wapi hadi ufisadi mkubwa wa aina hii usifichuliwe miaka yote hiyo.
Swali hilo ni muhimu lakini kwangu hilo ni swali la pili. Swali langu la kwanza la msingi ni nini kimesababisha kuporomoka maadili ya Watanzania hadi tukawa wezi kiasi hiki na kuibomoa nchi yetu wenyewe?
Ni baada ya swali hilo ndio nitauliza swali lile la pili zilikuwa wapi serikali zilizopita hadi kushindwa kudhibiti hali hii? Kwa mujibu wa taarifa ya Transparency International ya 2014, Tanzania ni ya 119 kati ya nchi 175 katika viwango vya dunia vya usafi dhidi ya ufisadi.
Kwa hali ilivyo sasa, inaonekana kuwa ufisadi na rushwa ni kansa iliyosambaa katika kila sekta ya maendeleo na pia nchi nzima. Miongoni mwa watumishi wa serikali waaminifu ni wachache, wezi ni wengi. Na sisi wananchi tunategemea serikali iwadhibiti hawa wezi wengi
Je, serikali ya awamu ya tano inayopambana na ufisadi ina mkakati wa kubadili mioyo ya watumishi waanze kuchukia wizi au tunategemea waache wizi kwa kuogopa mkono mrefu wa serikali?
Nionavyo, pamoja na ukali wote wa Rais John Magufuli na wasaidizi wake wakuu, kama mioyo ya watu haitobadilika na kuanza kuchukia rushwa na ufisadi, vita hii haitazaa matunda makubwa. Pia, hata serikali yenyewe inaweza ikaishiwa pumzi ya kufukuzana na wezi.
Maana ya mafanikio ya ukweli katika vita hii ni pale itakapofikia asilimia kubwa ya watumishi na wafanyabishara wengi wanachukia ufisadi na rushwa. Pia vitendo hivyo viwe vinatokea mara chache na vikitokea jamii ishangae. Vile vile watuhumiwa wanapokamatwa waone aibu. Tunaweza kufikia kiwango hiki cha maadili?
Kwa hali ilivyo sasa, sio siri kwamba jamii inaona fahari kuwa na ndugu ?anayepiga? fedha za umma. Utasikia, ?Jamaa ana akili sana. Mwaka tu tangu aanze kazi TRA kashajenga nyumba mbili na ana gari tatu. Yule ndugu yetu mwingine kazubaa?.
Swali muhimu la kujiuliza ni je wakati tukisuka mikakati ya kupambana na rushwa, tunaweza pia kufikiria mipango ya muda mrefu ya kujenga taifa la watu wenye maadili na uzalendo, wanaomugopa Mungu na ambao wanachukia rushwa na ufisadi? Ili tuweze kufikia lengo hilo, lazima kuwe na mabadiliko ya kimtazamo.
Kwa mfano, tuanze kuangalia uwezekano wa kufundisha maadili ya kiutu na kitanzania katika ngazi zote za elimu ili wanafunzi waelewe kuwa elimu inaweza tu kuwa na manufaa kama itatumiwa kwa uaminifu. Tunahitaji kuingiza katika mitaala na kusisitiza maadili katika elimu kuanzia ngazi ya chekechea, msingi, sekondari hadi chuo kikuu.
Kwenye fani nyingi za kielimu katika ngazi za chuo, maadili ya kazi husika hufundishwa. Hata hivyo, maadili haya hufundishwa kama taaluma zaidi. Mwisho wa siku wanafunzi hufaulu somo la maadili kwa alama A, lakini je wanaamini kutoka mioyoni kuwa ni jambo zuri kufuata maadili ya kazi husika?
Tunapofundisha maadili twende mbali zaidi ya kuwapa wanafunzi ufahamu wa maadili ya kazi na ufahamu wa namna ya kufanya maamuzi sahihi wanapokabiliana na ugumu wa kuchagua mawili au zaidi (ethical dilema). Zaidi ya hayo mawili, wanafunzi washawishiwe ili waamini kuwa kufuata maadili ni jambo sahihi kwa faida zao binafsi, familia zao, jamii na nchi.
Namna mojawapo ya kuwaaminisha wanafunzi kuwa kufuata maadili ni jambo sahihi ni kwa kujenga hofu ya Mungu, na hapo ndio umuhimu wa viongozi wa dini na unapojitokeza. Viongozi wa dini wanapaswa kuhimiza waumini wao kumuogopa Mungu kwa kusimamia maadili sio tu ya kikazi (professional ethics) lakini pia maadili ya ya kiutu na ya kitanzania.
Changamoto kubwa ambayo viongozi wa dini watakumbana nayo ni kuondoa fikra potofu miongoni mwa waumini kuwa maana ya ?ibada? ni kwenda kanisani na msikitini. Maana sahihi ya kuabudu ni kutekeleza ni kuishi kwa kufuata miongozo ya Mungu. Tunapozungumzia maisha tunamaanisha vipengele vyote: utendaji kazi, malezi ya familia, mahusiano ya ndoa, siasa, biashara na kadhalika.
Tukirekebisha mtazamo wetu juu ya dini, tutamuogopa Mungu katika kila tulifanyalo badala ya kumtii Mungu pale tu tunapoingia katika nyumba za ibada, kama tufanyavyo wengi wetu sasa hivi.
Hata kwa wale wasioamii Mungu wanapaswa walau kuwaonea huruma watanzania wenzao kwani fedha za serikali zinazoibwa ndio chanzo cha mapato kinachotegemewa kwenda kuboresha huduma mbalimbali za kijamii kama afya, elimu, maji na kadhalika
Ukilielewa hili vema, kila ukiona wakina mama wamelala kitanda kimoja watu watatu katika hospitali za serikali, wagonjwa wanalalamika hawapewi dawa na hawana pesa za kununulia, wagonjwa hawapati vipimo kwa sababu vifaa tiba havitoshelezi ? utahisi kuwa unahusika kutengeneza hali hii kwa kuiibia serikali.
Fikra potofu nyingine ni kuwa hakuna tatizo kuiibia serikali. Wizi ni wizi tu na hauwi na nafuu kwa sababu iliyoibiwa ni serikali. Tena kismingi, kuiibia serikali ni jambo baya zaidi kwa sababu unauibia umma wa Watanzania.
Inashangaza kuwa kwa hali ilivyo sasa katika jamii yetu tunaua vibaka kwa kutuibia vitu vidogo lakini tunawasifu mafisadi walioiba mabilioni. Nilitegemea wale tunaowajua kuwa ni mafisadi wanapoonekana katika hafla za wazi wazomewe ili kuonesha kuwa hatupendi kuibiwa.
Jambo hilo ni gumu kutokea kwa sababu kama ilivyo ngumu kwa mafisadi kujua uhusiano wa umasikini wa Watanzania wanaowazunguka katika jamii na vitendo vyao vya kifisadi, imekuwa ngumu vile vile kwa watanzania wenyewe kung?amua kuwa umasikini wao unasababishwa kwa kaisi kikubwa na ufisadi.
Wakati Rais Magufuli akipambana kuondoa ufisadi, nikiamini kuwa mafisadi wataficha makucha yao kwa muda kwa kuogopa kukamatwa na kisha wakipata nafasi watarejea kwa kasi kubwa kubwa zaidi, nahofia mafanikio yetu yanaweza kuwa ya muda tu.
Ninachotamani kuona ni Watanzania wanachukia rushwa na ufisadi na wanafanya kazi na biashara zao kwa uaminifu. Natamani pia serikali ianze kuondoa vikwazo vinavyolazimsha watu wapokee na kutoa rushwa. Kozi nyingi zisizolipika, lakini bial kusahau maslahi ya watumishi.
Raia Mwema