Isike Moses
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 2,789
- 4,245
Hii ni mara yangu ya kwanza kuweka bandiko hapa JamiiForums, miaka yote nimekuwa mchangiaji kwa mabandiko ya wadau wengine.
Naelewa ugumu wa vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya, naelewa jinsi inavyohusisha maofisa wa serikali katika kuwalinda wafanyabiashara hao wenye utajiri mkubwa.
Eneo la Mwananyamala ni moja ya maeneo ambayo biashara ya dawa za kulevya imeshamiri sana, na hufanyika kwa uwazi pasipo hofu kwa wahusika maana wanapewa ulinzi na askari wa vituo vya maeneo husika.
Pale Mwananyamala 'kwa Kopa', eneo la Peace Bar, kuna nyumba maarufu kwa jina la KOSOVO ambayo inamilikiwa na familia ya mama kwa jina la Binti wa Maulid. Ndani ya nyumba hiyo kuna biashara ya dawa za kulevya, pombe aina ya gongo na ngono huendeshwa.
Familia hiyo kwa upande wa dawa za kulevya inapewa (inasambaziwa) na mwajiri wao ambaye anajulikana kwa jina la KAZI.
Huyu ni mwanamtandao wa wafanyabiashara hiyo Dar es salaam mwenye ukaribu na kijana Kinje.
KAZI amelimiliki eneo la Mwananyamala na kuwa ndiyo ngome yake kuu. Nje ya biashara hiyo pia ni mwanamtandao wa kukodisha silaha kwa watu wanaofanya matukio ya uhalifu.
Kituo cha polisi kwa Kopa (askari) kwa miaka yote ndiyo wanatoa ulinzi kwa mwanamtandao huyo na wenzake. Hufika kwake na kupata gawio (pesa).
Naelewa humu wapo wadau na watu wa mamlaka ya serikali wenye kuweza kufuatilia mtu huyo na sheria kuchukua mkondo wake.
Nawasilisha..