TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Jana jumatatu 20/02/2017 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Aikaeli Mbowe alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa mafichoni ili kukabiliana na tuhuma za kuhusika na biashara ya Dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa taarifa, MBOWE alikamatiwa MIKOCHENI akiwa katika harakati za kutoroshwa na Dereva wake kutoka kwenye Appartment moja kwenda nyingine kwa kutumia gari namba T830 DEW VX nyeusi.
Baada ya taarifa za kukamatwa kwa Mbowe kuandikwa humu( jamiiforums) na LIZABONI, zilianza juhudi kubwa za kutaka kupotosha(sababu haijajulikana kwanini upotoshaji huu) kutoka kwa baadhi ya wanachama wa CHADEMA. Miongoni mwa watu waliokuwa wakitumia nguvu nyingi kutaka kuuaminisha Umma kuwa Mbowe hakukamatwa bali amejipeleka mwenyewe Polisi ni pamoja na anayejiita afisa habari wa CHADEMA, TUMAINI MAKENE, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Dar es Salaam, Henry KILEWO na JOHN MREMA.
Wakati hao wakipotosha taarifa ya Mbowe kukamatwa, Mwanasheria wa CHADEMA, TUNDU LISSU yeye aliweka wazi kuwa MBOWE amekamatwa na Jeshi la Polisi na siyo kwamba amejipeleka Polisi.
Jana kabla MBOWE hajakamatwa, wanasheria wa CHADEMA, JOHN MALLYA na TUNDU LISSU waliripotiwa kwa nyakati tofauti, wakimtaka Mwenyekiti wao KUTOJIPELEKA POLISI na kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba Mbowe alipofikishwa Kituo cha Polisi cha Kati(Central) na kuulizwa sababu za kukaidi kujisalimisha Polisi, alijibu na kusema Wanasheria wake walimkataza huku watu wengine wakimwambia hakua na kosa.
Mytake:
Nini tafsiri hii ya MBOWE kujificha na Watoa habari wa chama kupotosha kihusu kukamatwa kwake? Tuamini Mbowe alijua anakosa ndiyo maana alikuwa anaogopa kwenda polisi?
Kama taarifa ya Kukamatwa kwa BOWE inaweza kupotoshwa na viongozi wakuu wa CHADEMA kama Afisa habari wa CHAMA na Mwenyekiti wa Chama wa Mkoa , ni taarifa ngapi zimepotoshwa kuhusiana na namna CHADEMA wanavyoendesha chama? Tukiamini kuwa CHADEMA ni wasanii wasanii ilimradi tu kutaka kuaminiwa na wananchi tutakuwa tunakosea? Na je TUMAINI MAKENE aendelee kuaminiwa kama Afisa habari wa CHADEMA? HENRY KILEWO NA JOHN MREMA hawaoni kama wanazivunjia heshima nafasi zao ndani ya Chama kama wanafanya usanii usanii kwenye taarifa nyeti kama za kukamatwa kwa Mwenyekiti wao?