Vision ya mama ni simple and very clear (4Rs)

Vision ya mama ni simple and very clear (4Rs)

ukiwa na njaa utakuwa corrupt tu utake usitake wewe ulipwe laki tano kazi yako ni kupass contract za million 500 utakataa 10%!!!? na ukoo mzima unakutegemea for strong institutions nazani waafrika tunamezeshwa sumu na wasomi wa elimu za magharibi we need strong leaders kwanza watujengee uchumi imara kwa kuzuia unyonyaji kama ule wa congo, kudhibiti ubadhiifu na mentality za utegemezi then uchumi imara utatuletea hizo institutions imara

uongozi mzuri kwa vipi na kulinganisha na upi au kwa standards zip?
Lakini ajabu wanaokula rushwa kwa sehemu kubwa ni wenye mishahara minono na marupurupu kibwena na ni wale wenye nafasi zao na rushwa zao zinaathari miaka ya kuhesabu.Achana na trafiki na watendaji wa vijiji wale ni hongo
 
Mkuu Naona ajira imeshika hitimu kabisa hutaki mchezo
Kitendo cha kiongozi kuwa na kauli nzuri tu, za kufariji na kutia moyo ( hata kama hamna anachofanya) tayari ni hatua kubwa sana ya mafanikio.

Hivi unajua kuwa hatua ya kwanza ya uwekezaji ni imani? Bila imani hakuna mtu yoyote anaweza kuingiza mtaji wake mahali?
 
Kuna watu wanauliza hivi maono ya mama ni yapi?
Naona upo kwenye mipasho zaidi kuliko halisia ya swali ulilouliza.

Imekuwa wazi sasa kwamba huyu haamini kwamba waTanzania wanaweza kuleta maendeleo kwa nchi yao bila ya kuwa vitegemezi kupindukia. Matokeo ya 'Vision' hii, kama unaweza kuiita hivyo ni kuwa Tanzania itakuwa nchi tegemezi milele, na maana ya hilo ni kwamba wananchi wake watabaki kuwa wasindikizaji ya hao wanaotazamiwa kuleta maendeleo, badala ya wao kuwa ndio wamiriki na waendesha maendeleo hayo.

Nina hakika hali hiyo wataikataa, kama siyo leo, huko mbeleni.
 
Kuona ni jambo moja, jambo la pili ni nini unafanya baada ya kuona? Kuna mtu akiona umefanya jema anakutia moyo, mwingine anakukatisha tamaa, mwingine anakuloga ukafie mbali. wewe upo kundi lipi?
Sina kundi hapo je wewe upo kundi gani?
 
Naona upo kwenye mipasho zaidi kuliko halisia ya swali ulilouliza.

Imekuwa wazi sasa kwamba huyu haamini kwamba waTanzania wanaweza kuleta maendeleo kwa nchi yao bila ya kuwa vitegemezi kupindukia. Matokeo ya 'Vision' hii, kama unaweza kuiita hivyo ni kuwa Tanzania itakuwa nchi tegemezi milele, na maana ya hilo ni kwamba wananchi wake watabaki kuwa wasindikizaji ya hao wanaotazamiwa kuleta maendeleo, badala ya wao kuwa ndio wamiriki na waendesha maendeleo hayo.

Nina hakika hali hiyo wataikataa, kama siyo leo, huko mbeleni.
Kwa kawaida binadamu tunaishi kwa kutegemeana. Na nchi zinategemeana. Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa comparative advantage. Unajiimarisha kwenye kile ulichonacho halafu kile ambacho huna au ni vigumu kuzalisha kwako kwa faida, unachukua kwa mwenzako. Ndio dunia ilivyo.

So tunatakiwa tupambane na sisi tuwe na dhamani ya kuitoa hapo dunia ni lakini wakati huo huo tuendelee kunufaika na thamani wanazotoa wenzetu huko duniani.

Kuhusu mikopo, kuna kitu kinaitwa poverty cycle. Ukiwa kwenye hiyo cycle hakuna namna unaweza kutoka hadi aibuke mwamba akupige tafu na ndicho kinachofanyika
 
kwakuwa mtaji wa wanasiasa katika zama zote ni nguvu ya ushawishi kwa watu nchi hii ilimuhitaji mtu atakae waaminisha watu kuwa ataleta mabadiliko na kwa haiba ya JPM alionekana kuwa nabii anaefaa kwa zama hizo nae akaishika nafasi hiyo na kuicheza kama ilivyotakiwa
Hapana.

"Hakuicheza kama ilivyotakiwa."

Katika kucheza huko alinogewa sana sifa na kuchanganya na mengine ambayo hayakuwa sehemu ya mchezo kabisa.

Haya mengine ndiyo yaliyoharibu kila kitu.
 
Kwa kawaida binadamu tunaishi kwa kutegemeana. Na nchi zinategemeana
Uwe unaelewa unaposoma yaliyoandikwa.
Sikuandika popote Tanzania kutotegemeana na nchi zingine, wala kujitoa katika ushiriki wa watu wengine katika maendeleo yetu.

Usiwe unapitiliza katika mapenzi yako kwa mtu na kufunga akili kabisa juu ya mambo mengine.
 
Kwa kawaida binadamu tunaishi kwa kutegemeana. Na nchi zinategemeana. Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa comparative advantage. Unajiimarisha kwenye kile ulichonacho halafu kile ambacho huna au ni vigumu kuzalisha kwako kwa faida, unachukua kwa mwenzako. Ndio dunia ilivyo.

So tunatakiwa tupambane na sisi tuwe na dhamani ya kuitoa hapo dunia ni lakini wakati huo huo tuendelee kunufaika na thamani wanazotoa wenzetu huko duniani.

Kuhusu mikopo, kuna kitu kinaitwa poverty cycle. Ukiwa kwenye hiyo cycle hakuna namna unaweza kutoka hadi aibuke mwamba akupige tafu na ndicho kinachofanyika
Kiujumla, bandiko lako halina 'focus' hata kidogo, na kama ni hiyo "dira" unayozungumzia, haiwezi kuwa kiujumla jumla hivi.

Focus ni lazima iwe katika uwezeshaji wa waTanzania, no matter what! Na ninajua hata hili utakuwa na shida nalo sana kulielewa.
 
Tunapozungumzia strong leadership Africa, tunazungumzia dictators na sio lazima dikteta awe na akili, anaweza pia kuwa mtu dhalimu na akawa anadhulumu haki za watu hata kufanya mauaji kwa dhulma huku akifanya propaganda na kama hamna taasisi imaraza kumzuia kufanya hivyo kama ilivyo kwa nchi nyingi za Africa, anaweza kufanya mambo ya kuogofya sana. Ndio maana wanaolina hilo, wanafikiri taasisi imara ni muhimu zaidi ya mtu moja mmoja.
North Korea ina dictator China ina Dictator Urusi ina Dictator tofauti ya madictator hao na Kagame na Gadafi ni role ya mataifa ya magharibi kwetu ni madictator pale wanapocheza na interest zao tu
 
North Korea ina dictator China ina Dictator Urusi ina Dictator tofauti ya madictator hao na Kagame na Gadafi ni role ya mataifa ya magharibi kwetu ni madictator pale wanapocheza na interest zao tu
Mkuu, korea kasikazini raia ni maskini sana. Utajiri wa china umetokana na nidhamu ya wachina na si udikteta. Kama udikteta huleta maendeleo, unazizungumziaje nchi kama norway, sweeden, denmark na.k?

Yaani hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya udiktata na maendeleo au demokrasia na maendeleo
 
Hapana.

"Hakuicheza kama ilivyotakiwa."

Katika kucheza huko alinogewa sana sifa na kuchanganya na mengine ambayo hayakuwa sehemu ya mchezo kabisa.

Haya mengine ndiyo yaliyoharibu kila kitu.
Mengine yataje, alicheza ipasavyo kwa maana ilitumbua mafisadi alisimamia na kudhibiti matumizi alianzisha miradi na kuweka nidhamu ya utumisbi wa umma hakufanya 100% kwan haiwezi kuwa ivo
 
Mengine yataje, alicheza ipasavyo kwa maana ilitumbua mafisadi alisimamia na kudhibiti matumizi alianzisha miradi na kuweka nidhamu ya utumisbi wa umma hakufanya 100% kwan haiwezi kuwa ivo
Sijasema afanye kwa mia kwa mia, kwa sababu najua haiwezi kuwa hivyo bila wewe kunikumbusha.

Sasa nikuulize, hayo uliyotaja hapo ndiyo pekee uliyoyaona wewe? Sitajihangaisha na kukuandikia uchafu unaoujua aliufanya.
 
Kuna watu wanauliza hivi maono ya mama ni yapi? nani anayejua Rais Samia anakotupeleka? hivi nyie mnamuelewa huyu mama? mbona kama hana vision? n.k haya ni maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na baadi ya wananzengo.

Jamani eeh; vision ya mama ni very simple and clear. Ni '4Rs' yaani (Reconciliation, Resiliency, Reforms & Rebuild).

'Reconciliation'
– Kujenga uhusiano mwema miongoni mwa makundi yaliyokuwa yanahasimiana bila sababu. Hii ni kati ya vyama vya siasa, taasisi na mashirika, wadau wa maendeleo, Tanzania na nchi nyingine na ushirikiano wa kikanda na kimataifa, NGO's n.k.

'Resiliency' - Kuwaponya walioumizwa, kuwatetea waliodhulumiwa, kujaribu kuwarejeshea haki walipokonywa, kuleta furaha kwa wenye huzuni na kuwarudishia matumaini waliokata tamaa n.k.

'Reforms' – Kufanya marekebisho makubwa ya kimifumo ikiwemo kurekebisha sheria mbovu kila zilipobainika, Kutupatia katiba mpya (kwa wakati muafaka ), kufanya mabadiliko ya kiuchumi kutoka uchumi wa ku force hadi uchumi wa kuvutia kisayansi.

'Rebuild' – Kurekebisha penye makosa na kuendeleza kujenga miundombinu muhimu ambayo iko kwenye pipeline.

Na R zote zinaenda kwa mpigo, usiponufaika na 'R' utanufaika na 'R' na usipofikiwa na 'R&R' lazima Upate japo 'R". Enjoy 'R' inayokuhusu huku ukitimiza wajibu wako kwa kuwa mafanikio ya kweli hupatikana pale kila mmoja wetu anapotimiza wajibu wake kikamilifu huku akitanguliza dhamira njema.

Haya yanajulikana na mama mwenyewe....yawezekana ndo ID yake hii
 
Na point sio udictator na maendeleo nilitaka uelewa na udifine udictator kwa mtazamo sahihi sio kwa propaganda za west yaan ulitegemea IMF iseme n.korea wana postive economic growth!? Kweli utakua hujui IMF ni nani na nini tofauti Yake na CNN
Mkuu, korea kasikazini raia ni maskini sana. Utajiri wa china umetokana na nidhamu ya wachina na si udikteta. Kama udikteta huleta maendeleo, unazizungumziaje nchi kama norway, sweeden, denmark na.k?

Yaani hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya udiktata na maendeleo au demokrasia na maendeleo
H
 
Sijasema afanye kwa mia kwa mia, kwa sababu najua haiwezi kuwa hivyo bila wewe kunikumbusha.

Sasa nikuulize, hayo uliyotaja hapo ndiyo pekee uliyoyaona wewe? Sitajihangaisha na kukuandikia uchafu unaoujua aliufanya.
Kukiri kuwa hakufanya 100% ni kusema kuna uchafu alifanya na hilo ni sawa pia
 
Na point sio udictator na maendeleo nilitaka uelewa na udifine udictator kwa mtazamo sahihi sio kwa propaganda za west yaan ulitegemea IMF iseme n.korea wana postive economic growth!? Kweli utakua hujui IMF ni nani na nini tofauti Yake na CNN

H
Mkuu sio kwa tafsiri ya IMF. Ni ukweli unaoonekana kwamba ndani ya korea kaskazini, wananchi wako hoi kiuchumi japo wamewekeza sana kijeshi.

China, dictor mkuu alikuwa Mao, ndani ya utawala wake aliua watu mamilioni kwenye cultural revolution, lakini bado watu zaidi ya 40milioni wakafa kwa njaa. Ndio maana nasema hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya udikiteta na maendeleo ya uchumi.

Kwa kifupi; kuna nchi za kidemokrasia ni tajiri na nyingine ni maskini na kuna nchi za kidikteta nyingine ni tajiri na nyingine ni maskini. Hivyo suala la maendeleo ya uchumi halina uhusiano wa moja kwa moja na demokrasia au udikteta.
 
Ukiona hizo R nazo zinakuchanganya, falsafa ya mama ni rahisi zaidi ya hapo. Ni "peace& love" kwa kiswahili mafanikio kwa wote bila kuumizana wala kudhulumiana. Hivyo tu yaani, hakuna mambo mingi.
Mafanikio wakati kila kitu kimepanda Bei?
 
🤣🤣🤣Kwani maana ya kuwa specific ni kusema Tanzania ya Viwanda
Kusema tunajenga uchuni ni tofauti na kusema tunajenga uchuni wa viwanda. Angeweza kuwa specific zaidi kwa kusema tunajenga viwanda vya nguo japo ingemnyima nafasi ya kuja kujitetea kwamba hata blenders za juice nazo ni viwanda!

Ndio maana hakutaka kuwa specific to that extent akiacha matoleo ya kuja kuchomokea hapo baadaye.
 
Back
Top Bottom