Vision ya mama ni simple and very clear (4Rs)

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,197
Reaction score
7,533
1652544418351.png
Kuna watu wanauliza hivi maono ya mama ni yapi? nani anayejua Rais Samia anakotupeleka? hivi nyie mnamuelewa huyu mama? mbona kama hana vision? n.k haya ni maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na baadi ya wananzengo.

Jamani eeh; vision ya mama ni very simple and clear. Ni '4Rs' yaani (Reconciliation, Resiliency, Reforms & Rebuild).

'Reconciliation'
– Kujenga uhusiano mwema miongoni mwa makundi yaliyokuwa yanahasimiana bila sababu. Hii ni kati ya vyama vya siasa, taasisi na mashirika, wadau wa maendeleo, Tanzania na nchi nyingine na ushirikiano wa kikanda na kimataifa, NGO's n.k.

'Resiliency' - Kuwaponya walioumizwa, kuwatetea waliodhulumiwa, kujaribu kuwarejeshea haki walipokonywa, kuleta furaha kwa wenye huzuni na kuwarudishia matumaini waliokata tamaa n.k.

'Reforms' – Kufanya marekebisho makubwa ya kimifumo ikiwemo kurekebisha sheria mbovu kila zilipobainika, Kutupatia katiba mpya (kwa wakati muafaka ), kufanya mabadiliko ya kiuchumi kutoka uchumi wa ku force hadi uchumi wa kuvutia kisayansi.

'Rebuild' – Kurekebisha penye makosa na kuendeleza kujenga miundombinu muhimu ambayo iko kwenye pipeline.

Na R zote zinaenda kwa mpigo, usiponufaika na 'R' utanufaika na 'R' na usipofikiwa na 'R&R' lazima Upate japo 'R". Enjoy 'R' inayokuhusu huku ukitimiza wajibu wako kwa kuwa mafanikio ya kweli hupatikana pale kila mmoja wetu anapotimiza wajibu wake kikamilifu huku akitanguliza dhamira njema.
 
Urefu wa kamba ni vision au sera?
Urefu wa kamba maana yake upate malipo sawa na unachostahili kwa mujibu wa sheria na ukubwa wa kazi uliyofanya. Yaani usidhulumu wala kudhulumiwa. Haki bin haki. Aidha, usiingilie mamlaka yasiyo yako kwa kibri bali uwe mtu wa kadiri na unaye heshimu haki za watu wengine. Hii inaangukia kwenye 'R' zote. Ukiona mtu anaipinga hii, ujue anataka kuzingua mahali.
 
... angesimama jukwaani kuelezea vision yake hiyo ingekuwa jambo la maana sana. Kiongozi bora sharti aeleweke na anaowaongoza anawapeleka wapi clearly and loudly! Pia, kama ile sera ya Tanzania ya Viwanda imezikwa rasmi wananchi na taifa kwa ujumla liambiwe ukweli badala kukaa tu kimya.
 
Mkuu, viwanda ni part and parcel ya maendeleo ya kiuchumi. Sio falsafa ya jumla ya kiongozi bali ni sehemu ya mipango ya maendeleo.

Kama unakumbuka mwaka jana kulikuwa na mazungumzo na China kujenga baadhi ya viwanda vya HiTech hapa nchini, hizi ni moja ya stratejia za kukuza viwanda nchini, miongoni mwa nyinginezo.
 
... shukrani kwa ufafanuzi. Ila nakumbuka aliyepita alikuwa very specific - Tanzania ya Viwanda.
 
Mkuu, mambo mengine tulishaambiwa na mzee JK kuwa; za kuambiwa unachanganya na zako. so hata ninachokuambia mimi kipime kama kinafanana fanana na ukweli? usikichukue tu jumla jumla mkuu wangu.
 
Mleta mada I salute you, nimetoka kumuambia mke wangu jana, nasisitiza jana, nimemuambia nikimuangali Mama na staili yake ya kuongoza, namuona ni mtu anayetaka kila mtu awe na hela, awe na maisha mzuri, kifupi mama anataka kila mtu ale ili asisumbuliwe na kelele, tatizo letu Watanzania hatuzioni fursa, tunataka kila kitu tuwekewe mezani, AWAMU HII, NARUDIA AWAMU HII, KAMA UKIWA NA MCHONGO, BIASHARA, KAZI NA JUHUDI, HUU NI WAKATI WA KUTOKA.
Naziona fursa nyingi awamu hiu tofauti sana na kipindi cha Bwana yule aliyekuwa anakula na Genge lake huku akituita sisi wanyonge.
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Mama ni mtu mwema mwenye dhamira njema kwa watu wote. Yaani anataka aone kila mtu anafanikiwa. Hata asipofikia lengo hilo kikamilifu, bado ukweli utabakia huo huo.

Moja ya changamoto kubwa kwake na kwetu sote ni kwamba jamii yetu imejaa watu wengi wa ajabu ajabu. Kwa mfano watu wanaonun'guika kwa kila wanachofanyiwa, watu wenye shida ya kila solution inayotolewa huku wao wakiwa hawana solution, watu wanaopenda kuona wenzao wanaumia bila sababu n.k. Hivyo unapoongoza jamii ya watu wa namna hiyo, unaweza kuwa na dhamira njema, ukachukua hatua muhimu kwa kadiri ya uwezo wako na bado usifanikiwe sana.

Ndio maana tunasisitiza kuwa pamoja na reformations zinazofanyika, bado ni muhimu sisi kama raia mmoja mmoja tukawajibika kikamilifu vinginevyo bado ni tatizo.
 
... shukrani kwa ufafanuzi. Ila nakumbuka aliyepita alikuwa very specific - Tanzania ya Viwanda.
Hivyo viwanda vipo wapi, maana mpaka anaenda zake hali ya ajira ilikuwa inazidi kuwa tete huku akituita wanyonge, biashara zilifungwa,mashirika rafiki yakaondoka zake, kila sehemu ikawa vilio, jamaa alikuwa anatumaliza hakika.
 
Kuna watu wanauliza hivi maono ya mama ni yapi? nani anayejua Rais Samia anakotupeleka? hivi nyie mnamuelewa huyu mama? mbona kama hana vision? n.k haya ni maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na baadi ya wananzengo.

Jamani eeh; vision ya mama ni very simple and clear. Ni '4Rs' yaani (Reconciliation, Resiliency, Reforms & Rebuild).

'Reconciliation'
– Kujenga uhusiano mwema miongoni mwa makundi yaliyokuwa yanahasimiana bila sababu. Hii ni kati ya vyama vya siasa, taasisi na mashirika, wadau wa maendeleo, Tanzania na nchi nyingine na ushirikiano wa kikanda na kimataifa, NGO's n.k.

'Resiliency' - Kuwaponya walioumizwa, kuwatetea waliodhulumiwa, kujaribu kuwarejeshea haki walipokonywa, kuleta furaha kwa wenye huzuni na kuwarudishia matumaini waliokata tamaa n.k.

'Reforms' – Kufanya marekebisho makubwa ya kimifumo ikiwemo kurekebisha sheria mbovu kila zilipobainika, Kutupatia katiba mpya (kwa wakati muafaka ), kufanya mabadiliko ya kiuchumi kutoka uchumi wa ku force hadi uchumi wa kuvutia kisayansi.

'Rebuild' – Kurekebisha penye makosa na kuendeleza kujenga miundombinu muhimu ambayo iko kwenye pipeline.

Na R zote zinaenda kwa mpigo, usiponufaika na 'R' utanufaika na 'R' na usipofikiwa na 'R&R' lazima Upate japo 'R". Enjoy 'R' inayokuhusu huku ukitimiza wajibu wako kwa kuwa mafanikio ya kweli hupatikana pale kila mmoja wetu anapotimiza wajibu wake kikamilifu huku akitanguliza dhamira njema.
Huyu hangaya hana sera wala maono.
 
Huyu hangaya hana sera wala maono.
Moja ya vitu muhimu ambavyo tunatakiwa tufanye lakini hatufanyi, ni kuwaunga mkono watu wema wanapofanya mambo mema kama 'incentive' ya wao kuendelea kufanya mambo mema.

Kwa kutokufanya hivyo, watu wema (wachache tulionao) wanakosa 'incentives' mwishowe wanaamua kuacha kufanya mambo mema na kuacha liwalo liwe, au kuamua kugeuka na kuwa watu wabaya.

Kisha tunatumia nguvu kubwa kulaumu na kulaani, kumbe sisi tumechangia kwa degrees fulani kufanya watu hao wageuke kuwa watu wa ovyo. Kumbuka katika hatua za awali watu wote huzaliwa wema na katika hatua fulani hubadilika kwa sababu mbalimbali ikiwemo mazingira na jinsi jamii inavyo behave dhidi ya wema au uovu.
 
Kuna watu wanauliza hivi maono ya mama ni yapi? nani anayejua Rais Samia anakotupeleka? hivi nyie mnamuelewa huyu mama? mbona kama hana vision? n.k haya ni maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na baadi ya wananzengo.

Jamani eeh; vision ya mama ni very simple and clear. Ni '4Rs' yaani (Reconciliation, Resiliency, Reforms & Rebuild).

'Reconciliation'
– Kujenga uhusiano mwema miongoni mwa makundi yaliyokuwa yanahasimiana bila sababu. Hii ni kati ya vyama vya siasa, taasisi na mashirika, wadau wa maendeleo, Tanzania na nchi nyingine na ushirikiano wa kikanda na kimataifa, NGO's n.k.

'Resiliency' - Kuwaponya walioumizwa, kuwatetea waliodhulumiwa, kujaribu kuwarejeshea haki walipokonywa, kuleta furaha kwa wenye huzuni na kuwarudishia matumaini waliokata tamaa n.k.

'Reforms' – Kufanya marekebisho makubwa ya kimifumo ikiwemo kurekebisha sheria mbovu kila zilipobainika, Kutupatia katiba mpya (kwa wakati muafaka ), kufanya mabadiliko ya kiuchumi kutoka uchumi wa ku force hadi uchumi wa kuvutia kisayansi.

'Rebuild' – Kurekebisha penye makosa na kuendeleza kujenga miundombinu muhimu ambayo iko kwenye pipeline.

Na R zote zinaenda kwa mpigo, usiponufaika na 'R' utanufaika na 'R' na usipofikiwa na 'R&R' lazima Upate japo 'R". Enjoy 'R' inayokuhusu huku ukitimiza wajibu wako kwa kuwa mafanikio ya kweli hupatikana pale kila mmoja wetu anapotimiza wajibu wake kikamilifu huku akitanguliza dhamira njema.
Tutawapa TBC wawe wanaisoma hii kwenye tunatrkeleza.

Umeiweka poa sana.
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Mama ni mtu mwema mwenye dhamira njema kwa watu wote. Yaani anataka aone kila mtu anafanikiwa. Hata asipofikia lengo hilo kikamilifu, bado ukweli utabakia huo huo.

Moja ya changamoto kubwa kwake na kwetu sote ni kwamba jamii yetu imejaa watu wengi wa ajabu ajabu. Kwa mfano watu wanaonun'guika kwa kila wanachofanyiwa, watu wenye shida ya kila solution inayotolewa huku wao wakiwa hawana solution, watu wanaopenda kuona wenzao wanaumia bila sababu n.k. Hivyo unapoongoza jamii ya watu wa namna hiyo, unaweza kuwa na dhamira njema, ukachukua hatua muhimu kwa kadiri ya uwezo wako na bado usifanikiwe sana.

Ndio maana tunasisitiza kuwa pamoja na reformations zinazofanyika, bado ni muhimu sisi kama raia mmoja mmoja tukawajibika kikamilifu vinginevyo bado ni tatizo.
Mkuu inabidi tubadilike sana, kama sio sisi basi tuhakikishe watoto wetu hawatabaki kama tulivyo sisi, nasema hivi kwa sababu ukiangalia Watanzania wengi, hasa hawa wanaopenda kuitwa WANYONGE, hawa watu wapo radhi kila mtu akose ili wote mufanane na muwe wanyonge, kuna rafiki yangu ana duka Kariakoo, kipindi cha nyuma hata kwenda dukani kwake ilikuwa shida maana kulijaa machinga mpaka mlangoni, ukipaki gari ukija wametundika nguo kwenye vioo, leo wameondoka wanalalamika kwa mbali eti huu sasa wakati wenu, wenye hela munathaminiwa, wakati huo huyu rafiki yangu alikuwa anakaribia kufunga biashara maana hakukuwa na wateja, tufanye kazi, kipindi huchu cha mama kina fursa nyingi, hela zimeanza kujaa mtaani, ninapoishi mimi kila kona sasa watu wanajenga, wakatu ndio huu.
 
Labda vision ya kuhamasisha ufisadi kwenye Taifa letu👇🤡🤡🤡
View attachment 2224528
Ndugu, hii mbona kuna mtu ashaileta hapa, tukafafanua tukasema: Urefu wa kamba maana yake upate malipo sawa na unachostahili kwa mujibu wa sheria na ukubwa wa kazi uliyofanya. Yaani usidhulumu wala kudhulumiwa. Haki bin haki. Aidha, usiingilie mamlaka yasiyo yako kwa kibri bali uwe mtu wa kadiri na unaye heshimu haki za watu wengine. Hii inaangukia kwenye 'R' zote.

Sasa labda useme wapi hujaelewa hapo. Vinginevyo wewe utakuwa una chuki zako tu ndugu yangu.
 
Mtashindana na Kivuli Cha Magufuli Kwa Kila aina.

Ila Watanzania hawawakubali ng'ooo!!.
 
Mkuu inabidi tubadilike sana, kama sio sisi basi tuhakikishe watoto wetu hawatabaki kama tulivyo sisi, nasema hivi kwa sababu ukiangalia Watanzania wengi, hasa hawa wanaopenda kuitwa WANYONGE, hawa watu wapo radhi kila mtu akose ili wote mufanane na muwe wanyonge, kuna rafiki yangu ana duka Kariakoo, kipindi cha nyuma hata kwenda dukani kwake ilikuwa shida maana kulijaa machinga mpaka mlangoni, ukipaki gari ukija wametundika nguo kwenye vioo, leo wameondoka wanalalamika kwa mbali eti huu sasa wakati wenu, wenye hela munathaminiwa, wakati huo huyu rafiki yangu alikuwa anakaribia kufunga biashara maana hakukuwa na wateja, tufanye kazi, kipindi huchu cha mama kina fursa nyingi, hela zimeanza kujaa mtaani, ninapoishi mimi kila kona sasa watu wanajenga, wakatu ndio huu.
Mkuu umeongea mambo ya msingi sana, unapoongoza watu wengi lazima kuwe na utaratibu, vinginevyo hufiki popote na sasa ndicho kinachofanyika.

Aidha, pamoja na fursa nyingi kufunguliwa ambapo pia naziona zikienda kupunguza tatizo la ajira, tatizo ninaloliona ni ukosefu wa uaminifu kwa wabongo na hivyo kutoajirika/kutofaa kupeana connection. Ni lazima tubadilike tuwe waaminifu ili tuweze kunufaika na fursa zinazofunguka.

Kuna watu wengi wenye mitaji lakini wanaopa kuwekeza na kuajiri wabongo sababu ya (wizi na uzembe) kuna wanataka kuwekeza kwenye kilimo lakini wanaogopa (Wizi na uzembe).

Kwa ujumla ili tuweze kunufaika na fursa zinazofunguka, uaminifu, kujituma na customer service ni muhimu sana. Tuna watu wengi ambao ukiwaajiri kwenye biashara yako au hata shambani ni hopeless kabisa.
 
Previous regime ilikuja na approach hiyohiyo kwani by then hali ya mambo ilikuwa hivi
kulikuwa na kundi la the oppressed ambalo tofauti na sasa lilijumuisha the majority ambao walikuwa wamechoshwa na upigaji, ufisadi na upapaa uliokuwa umekithiri sana walishuhudia rasilimali za umma zikiwa chini ya watu wachache waliozitumia dhidi yao Dowans Richmond IPTL Miamba kama akina the late Ditopile wazee wa Vijisenti nk walikuwa na uwezo wa kufanya watakalo uku hali ya uchumi ikizorota mgao wa umeme rushwa na ujanjaujanja vilikithiri na kuwa kero!

kwakuwa mtaji wa wanasiasa katika zama zote ni nguvu ya ushawishi kwa watu nchi hii ilimuhitaji mtu atakae waaminisha watu kuwa ataleta mabadiliko na kwa haiba ya JPM alionekana kuwa nabii anaefaa kwa zama hizo nae akaishika nafasi hiyo na kuicheza kama ilivyotakiwa

Katika kuicheza akawa anatembea kwenye circle ileile ya kutengeneza tabaka jingine la the oppressed this time the oppressed wakiwa ni the oppressor in the previous regime ambao kwa bahati mbaya ndio walio na real power kwani ndio haswa walimuweka alipo so to make the long story short we all know what happen..... the dude is no more

ukiwa kwenye meza ya wana wa nchi utaelewa kuwa watawala wanaimba wimbo tofauti kabisa huku "anaupiga mwingi" ni kauli iliyo synonymous na kufanya madudu ila kwakuwa watawala ndio wenye kila kitu kuanzia bunge ambalo ndio mdomo wa wana wa nchi, nchi itaendelea kuimba wimbo wa watawala tu

Deep down hiyo Reconciliation sio ya watawala na wana wa nchi ni watawala na makundi kadhaa yenye interest zao zingine hasa upigaji kama ulivyotoa mfano vyama vya siasa na mashirika blah blah ....
and so is hiyo Resiliency, reform na rebuild jiulize kwa dhati ya moyo wako ni nani mlengwa hasa wa hizo approach je ni the Majority (lower and middle income earners) au the minority super power
"kwa bahati nzuri kila zama huja na nabii wake na kwa bahati mbaya kila nabii huja kuserve interest za aliye mtuma si aliotumwa kwao and no compromise "
 
Ila Watanzania hawawakubali ng'ooo!!.
Kama tulivyoeleza hapo awali kwamba kwenye jamii za kiafrika kuna wachawi wengi; Kawaida ya mchawi, anafurahi kuona zaidi watu wakipata shida (hata kama naye anapata shida) kuliko anavyopenda kuona yeye mwenyewe akifanikiwa. Ndio maana mchawi yuko tayari alale nje akiwa uchi ili akufanye wewe uugue. Sasa mtu kama huyu unatarajia nini la maana toka kwake? ukiona umeungwa mkono na mtu wa namna hiyo, kuwa makini sana.
 
Back
Top Bottom