Visa za Tanzania na maofisa uhamiahaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Visa za Tanzania na maofisa uhamiahaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NYENJENKURU, Jun 11, 2011.

 1. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndugu wana JF naleta kwenu hii maada na muone maafisa Uhamiaji wa Tanzania tulivyo wa ajaabu.Kisa ni kama hivi.Mtu anaenda Ubalozi wa Tanzania kama vile Marekani anataka kuja Tanzania kufanya workshop ya week moja au mbili anepewa visa yake anakuja Tanzania.Akifaka labda anaenda Ifakara Morogoro anakutana na afisa uhamihaji anamwambia wewe unafanya nini hapa Mzungu anamwabia nimekuja kwenye workshop hapa Ifakara.Afisa anamwambia hiyo visas yako waliyokupa siyo ya halali unatakiwa unipe tena dola mia nikupe nyingine.Mzungu anauliza kwa vipi unipe nyingine wakati mimi nimeenda kwenye ubalozi wenu hapo WDC nikawaelza nachotaka kwenda kufanya Ifakara halafu wewe unasema WALIKOSEA kukupa visa ya kufanaya workshop.Twende polisi.Je swali la nani wa kulaumiwa?Mgeni au Afisa uhamiaji wa Ubalozi?Au huyu wa Ifakara?Je wezentu wanyafanya hivyo?

  Naomba tutajidili kama labda kuna nini hapo kuhusu mfumo wetu wa Visa.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  kama mzungu akitoa pesa nyie pigeni hiyo pesa tu. hawa walituonea sana kipindi cha ukoloni
   
 3. MANI

  MANI Platinum Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280

  Mkuu lakini ndio sheria inavyotaka?
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Huko ni kujidhalilisha sana kwa watumishi na serikali kwa ujumla waambie wapunguze njaa hao uhamiaji......wanatia aibu taifa!!!!!
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mbona habari iko juu juu? Baada ya mgeni kusema waende polisi, nini kilichotokea? Walimruhusu kuingia au walimkatalia hata kwenda huko polisi? Au ni hadithi ya kutunga tu?

  Amandla..........
   
 6. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  kama vipi angemwambia alipe CTA mambo yaishe.
   
 7. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  tatizo hakuna ugawaji sawa wa keki ya taifa, wabunge wanajilipa mishahara mikubwa na hapohapo wanajilipa posho wakiwa kazini, maslah ya watumishi wengine ni duni, sasa tungeanza na kina lowasa tukomeshe wizi wanaofanya na tuwanyang'anye mali walizotuibia, kisha tuboreshe maslah ya watumishi wa chini.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hamna haja ya kujua kilichojiri. Mleta uzi alitaka tu kuonesha 'utendaji ulitukuka' ktk ofisi za umma. Hii ni aibu na inakatisha tamaa hata wageni wenye nia nzuri ya kuja Tz kwa minajili mbalimbali. Aina hii ya utendaji wa kihuni is another low kuonesha tulipo kama taifa.
   
 9. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nadhani wageni wanatakiwa wawe wanapewa maelezo kamili na balozi zetu wanapopewa visa. Yani waelezwe kuwa visa yako haikuruhusu kufanya kazi yoyote TZ, bali unaingia kama mgeni mshiriki kwenye mafunzo au utalii. Ukitaka kufanya kazi kama kuendesha semina taratibu zake ni 1,2,3,...
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hapana sikubaliani na wewe kabisaaaaaa
  hata sisi wengine tupo nje kwa sasa na hawa ambao tupo ktk nchi zao hawajatufanyia kama polisi wetu wanavyofanya sasa,kama ingekuwa ni hivyo tungekuwa tunapata tabu sana ktk nchi za watu

  kwa mfano,Australia,ujerumani na Uchina wao ukishaenda ubalozi wao na wakakupa viza hapo umamaliza kila kitu,utakwenda ktk nchi husika na utakaa kwa mda uliotakiwa kukaa na utarejea Tz bila matatizo yeyote yale,

  labda uwe umekata viza tofauti na kile ulichokusudia kufanya ndio mambo yanaweza kubadilika

  kwa mfano unakwenda kusoma nje utakata viza ya kiuanafunzi,kama ni biashara utakata viza ya biashara na mengineyo na pia kama ni kazi hilo ni swala la work permit halihusiani na viza,ila ktk maswala ya semina huwa inajulikana hata aina ya viza huwa ni tofauti na za biashara ama uwanafunzi na zina siku maalumu za kukaa nchi husika

  lakini bongo ni ushenzi mtupu,tumeweka umasikini mbele na ndio unaotufanya tutawaliwe kirahisi

  makosa yapo kwa huyo polisi aliyeomba tena 100$ kwani nadhani wale wa ubalozi walituwa viza kulingana na maombi ya mhusika.je anavyo kwenda kuibadilisha huwa inakuwa ileile ama ni tofauti na ile ya awali?

  Hii nchi umasikini ndio unasababisha tuendelee kutawaliwa
   
 11. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Thanks mtumia busara. Kwa kawaida balozi zetu haziruhusiwi kutoa vibali vya kufanya kazi ikiwa ni kwa muda mrefu au mfupi. Hata vile vya kufanya workshop muda mfupi (Carrying on temporaly assignment.. CTA). Vibali hivyo hutolewa na wiraza ya mambo ya ndani tu chini ya Uhamiaji.Ikumbukwe balozi zetu zipo Mambo ya nje. Tatizo lipo huko kwenye balozi zetu ndio wana wadanganya wageni kuwa wanaweza kuwapa kibali chochote kuja Tanzania wakati wao inavyofahamika wanaruhusiwa kutoa visitors pass tu. Hapo kuna mkanganyiko wa kimaslahi, balozi tezu hayo malipo ya visa huwa wanazitumia kundesha ofisi zao ukiwa ni pamoja na 'kununua mafuta'. Wakati idara ya uhamiaji wanataka fedha irudi Tanzania kuongeza 'makusanyo yao kwa mwaka'. Tusipende mara nyingi kutoa lawama tuu kwa watumishi wa serikali tunawavunja moyo. Huyo afisa uhamaji alikuwa sasa kumkakata huyo jamaa.Vibali vya seminar huwa vinaombwa na mwenyeji wako au ofisi iliyokualika kufanya seminar wala haviombwi na mgeni mwenyewe
   
 12. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sikubaliani na wewe kwa mambo mengi uliyondika fanya tafiti kwanza kwenye nchi yako kuna vibali vingapi vya ukazi na mamlaka zipi zinatoa vivyo vibali. Tupo wengi tulioshi nchi zingine. Nchi nyingi za magharibi hasa zile za Schengen ikiwemo Ujerumani uliyoitaja visa inatolewa kwa muda miezi mitatu tu. Kama unakaa zaidi ya hiyo miezi lazima kuna registration ambazo utatakiwa uzifanye ili upate resident permit. Mwanafunzi mbaye programme yake ni zaidi ya hiyo miezi lazima apate residence card. Nchi kama Uholanzi ndio inawawakilishi wa Uhamiaji hapohapo vyuoni, wanaita IND. Balozi za hizo nchi huwa zinaruhusiwa kutoa visa tu, unapofika kule kama utakaa zaidi ya miezi mitatu lazima ufanye registration hata kama ni kwa mtandao. Tofauti ya kwetu sisi na wao ni kwamba huwezi kukamatwa hovyo mtaani lakini yote hiyo naamini ni kwa sababu ya teknolog yao iko juu. Makazi yao yameorodheshwa vizuri kila mtu unatakiwa kuwa na anuani. Sioni ajabu kwa maafsa Uhamiaji kumkama mtu njiani, kwa technoj mbovu yetu, makazi hayajapangika, annual si lazima kuwa nayo etc
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Afisa uhamiaji alikuwa sahihi kumkamata huyo mgeni, na huko ubalozini nako walikuwa sahihi kumpa maelekezo ya uongo huyo mgeni. Inaonekana wewe ndio walewale.
   
 14. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ya ni kweli,tunachokiongelea ni visa,lakini ktk maswala ya residence permit ni kweli ni lazima ufanye maombi juu ya hiyo residence permit na kwa sasa baadhi ya nchi zimekuwa zikitowa mda wa mwaka mmoja tu hata kama utatakiwa kukaa hapo kwa miaka minne,

  lakini pia hapa nilipo niliwahi kukamatwa mtahani lakini lengo lao lilikuwa ni kuuliza kama nina passport na hawakutaka nitoe pesa tena kama tufanyavyo bongo

  kama ni hivyo ni bora tuwe wawazi kama wenzetu wafanyavyo,unaelezwa nini cha kufanya hata kabla ya kuingia ktk nchi husika
   
 15. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ni wapi nimesema afisa wa Ifakara alikuwa anataka chochote? Hapa lawama ni lazima tulaumu kwa sababu baina ya afisa wa Ifakara na wale wa ubalozini lazima upande mmoja wao una makosa na kusababisha usumbufu kwa wageni. Na sioni unachotetea hapa, labda utuambie wewe ni mmojawao. Mambo kama haya ni very basic na AIBU KUBWA kwa taifa.
   
 17. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mie sie wao ndugu nakushauri tu tembelea ofisa ya maafsa Uhamiaji iliyo jirani nawe wakupe taratibu zikoje. Ila mimi ninavyojua watu wanaokuja kwenye mikutano na seminar huwa wanapewa kitu kinaitwa CTA na ubalozi huwa hawatoi hicho kitu. Labda kama kuna vibali vya aina nyingi kwa shughuli ya aina moja.
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kwanini niende mie ambaye sihitaji hayo maelezo wakati mtu aliyehitaji hayo maelezo kwa ajili ya safari yake, wameshindwa kumpatia? this is a waste of time and space. Kwani unashindwa ku-admitt kwamba kuna tatizo?
   
 19. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Kwanini u-conclude kosa liko liko kwa uhamiaji au afisa wa ifakara tu? Kwani mwombaji hawezi kuwa alitenda kosa la kufanya shughuli isiyoendana na visa yake? Huwezi kuja na conclusion za aina hii bila kusikiliza pande zote.
   
 20. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndugu wana JF huyo mzungu kutoka Amerika amekuja kwa short vist katika tasisi fulani hapo Ifakara na hafanyi kazi yoyote ile.Anaagalia wenzeke wamefanikiwa vipi katki utafiti wa malaria hapo Ifakara.Ofisa uhamiahaji anakutana naye anaomba passport yake anamwambia wewe umepewe visa ambayo siyo lazima ulipe tena CTA mzungu anasema mimi nimeenda ubalozini nikaaambia nataka kwenda Ifakara kwa hiyo vist akagongewa visa kafiak Ifakara.Afisa uhamiaji anambiwa mimi sikuambiwa kama kuna malipo yoyote hapo Tanzania je kwa nini nilipe tena?Afisa uhamiaji anampleka polisi lakini baadae anachiwa je huyu mgeni anakosa gani?Kwa nini afisa uhamiaji asifike kwa wenji wake na kuwapa maelezo?Na kisa cha kwenda polisi ni baada ya kuombwa kitu kidogo na kukataa na baadae polisi afisi uhamiajia anasema jaamaa kamkataza kufanya kazi yake kwa makudi no nd maellezo aliyoandika polisi huyo jamaa wa Uhamiaji
   
Loading...