Visa vya kusisimua katika maisha...

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
Jamani huku mtaani kwetu umetoke msiba ndugu wawili wa tumbo moja (kaka na dada) wamefariki wakiwa wamepishana masaa mawili ...nilipomuuliza mama yangu yeye akaniambia mwaka jana akiwa kijiji kuna jamaa na dada yake walifariki kwa staili inayofafana . Dada mtu ambae alianza kufa alikutwa na kadhia la njiwa wa porini kumtua begani, alipomfukuza ghafla anaanza kuumwa na kufikia hatua ya kuishiwa damu alipofikishwa hospitali akawa amekwisha poteza maisha..Haikupita mwezi, kaka wa huyo dada nae akatuliwa na niwa kichwani, akatahamaki..baada ya siku mbili nae akawa hajiwezi kwa homa baadae akawa amekufa.

Kisa kingine, kijana mmoja aliiba kuku toka kijiji cha pili toka pale alipokuwa akiishi..baada ya siku mbili kuku akaanza kusikika akilia tiumboni kila akipumua...hazikupita siku nyingi akawa amepoteza maisha...

Yupo mzee mwingine ambae alikuwa na ndoa yake, akamtongoza mke wa mtu, baada ya kufanya nae tendo tu wakiwa machakani , ghafla yule mzee akaishiwa nguvu akazimia (presha ikawa imepanda na mwili wote uka pooza)..yule mwanamke akakimbia. Baada ya muda akapita mchunga ng'ombe katika eneo hilo na kumkuta yule mzee taabani karibu kufa..akaita watu, lakini wakashangaa mzee amezimia akiwa nusu uchi na uume umesiamama..wakamsaidia..alipopata nafuu mzee akadai alikuwa anajisaidia tu..hali ya mzee iliendelea kuzohofika mpaka baade aakawaaambia baadahi ya nduguze kilichotokea (alitembea na mke wa mtu)..Nduguze wakamshauri ni vizuri kwa usalama wa maisha yake akamshike mguu (kumwomba radhi) jamaa mwenye mke. Baada ya jamaa kuombwa radhi, akakataa kuwa yeye hausiki lakini yule mzee alipofikishwa nyumbani tu baada ya lile tukio la kuomba radhio, mguu mmoja ukarejewa na fahamu..ila sasa bado anatembe kwa kujivuta mguu mwwingine haufanyi kazi. Kuna madai kuwa yule mwenye mke alisikika akisema ikiwa jamaa atapona kabisa miguu yote huenda akarejea ukwale wake. Hivyo abaki vile vile ili asisumbue wake za watu.
 
duh, ngoja nijitahidi kuamini
japo hainiingii akilini kabisa
 
Maaana hapo kama unataka kutuambia ushirikina upo....au?? Kama hicho kisa cha kuku kulia tumboni balaa...
:yawn:
 
Ushirikina upo....kwani we huamini?

Ili uamini kitu kiuhakika uwe umeshuhudia (sipendi kuviweka akilini kwakweli)...mi sijawahi kushuhudia vitu kama hivi,zaidi ya kusikia stori na kusoma kwenye magazeti hadithi kama 'mama anakula nyama za watu'...ila ukielekeza imani yako kwa Mungu,hivi vitu vinakuogopa!
 

Wala hujakosea cku zote mtu humtokea anachokiamin,mzima ww?
 
Haya mambo niyakuchukulia km story tu na kuyaacha ukiyaamin lzm utaishi aisha ya wac wac!
 
Mi binafsi nimeshuhudia aisee so huwa naamini kabisa uchawi upo ila kwa kutokewa hapana bado ila mitaani haya mambo yapo we amini tu ila sali sana pia kuepukana nayo.Usiogope
 
Haya mambo niyakuchukulia km story tu na kuyaacha ukiyaamin lzm utaishi aisha ya wac wac!
Sure....ukifuatilia ushirikina hutakuwa na amani hata kidogo...usiku ukisikia kitu kimegonga bati hata km ni jani utaanza kuhisi wanga wameshaanza kazi zao...hahahaaaaaaa kaaaaaaaaaazi kweli
 
Haya mambo niyakuchukulia km story tu na kuyaacha ukiyaamin lzm utaishi aisha ya wac wac!


kUAMINI KITU HAINA MAANA UFUATILIE..USHIRIKINA UPO LAKINI UKIUFUATA NAWE UTAKUWA MSHIRIKINA..NA UTAIHSI KWA WASIWASI..HATA ZAMA ZA ADAMU WA KWANZA ULIKUWEPO (TWASOMA KATIKA MAANDIKO) NA NDIO MAANA HATA KATIKA MAANDIKO KUNA NAFASI YA KUKEMEA UCHAWI ..NDIVYO BAADHI YA MAKANISA YANAVYOFANYA NA KUJIPATIA UMAARUFU (EG. MZEE WA HAMMER GWAJIMA ET AL..) WANAAMINI KATIKA MISUKULE AMBAYO NI UCHAWI MTUPU..VISA HIVI NI KAMA SIMULIZI LAKINI VINAUHUSIANO MKUBWA NA MAISHA YA KAWAIDA YA BINADAMU..UTOKEA.
SOMA:
Rick Godwin "​
Exposing Witchcraft in the Church" Excerpt Exposing Witchcraft in the Church - Christianbook.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…