Virusi vya Homa ya Ini vyaupiku UKIMWI

Virusi vya Homa ya Ini vyaupiku UKIMWI

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema maambukizi ya ugonjwa wa Homa ya Ini yameongezeka mara mbili ya Virusi vya UKIMWI hivi nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari leo, Ijumaa Julai 28, Ummy amesema ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B) unaongoza kwa kuua Tanzania baada ya maambukizi kufikia asilimia 16, huku Virusi Vya UKIMWI, ikiwa ni asilimia 5.3.

Amesema ugonjwa huo huua taratibu ukilinganisha na magonjwa mengine kwa kuwa dalili zake huchukua muda mrefu kujulikana na kujitokeza wazi.

Amesema licha ya kwamba mpaka sasa hakuna takwimu halisi kutokana na watu kutokuwa na tabia za kupima afya zao, idadi ya wagonjwa wanaobainika kuwa na homa hiyo wengi huwa wamefikia hatua za mwisho za ugonjwa huo.

"Tunapata takwimu hizi kupitia uchangiaji wa damu, damu inayokutwa na Homa ya Ini ni nyingi zaidi ikilinganishwa na ile yenye Virusi vya UKIMWI,"amesema Ummy.

Chanzo: Mwananchi
 
huu ugonjwa ni nyoko, yaani ukimwi ukasome upya tena uende Makelele University ukaanze na cheti
Ukipiga Denda umeenda
ukigusana na jasho umeenda
damu ikipata kwenye ngozi umeenda
ukisex umeenda (hata kama na kondomu)
yote haya ukifanya na mwathirika imekula kwako na dalili hujitokeza baada ya miezi 30 tangu kuathirika
 
Niliugua sana last year mpaka nikahisi itakuwa ni huu ugonjwa aisee. Ila nashukuru Mungu sikuwa nao maradhi yaliyogundulika nilipata tiba na nikapona kabisa.
 
huu ugonjwa ni nyoko, yaani ukimwi ukasome upya tena uende Makelele University ukaanze na cheti
Ukipiga Denda umeenda
ukigusana na jasho umeenda
damu ikipata kwenye ngozi umeenda
ukisex umeenda (hata kama na kondomu)
yote haya ukifanya na mwathirika imekula kwako na dalili hujitokeza baada ya miezi 30 tangu kuathirika
Sasa SERIKALI YA MWENDO kasi imeweka maazimio gani baada ya kujua hizo takwimu. Mana naona nguvu nyingi bado ipo kwenye kampeni za kuzuia UKIMWI zaidi ya huu ugonjwa. Bila hii post mie nisingejua lolote kuhusu hizi takwimu. Hata kwnye bandiko la mleta mada sikuona onyo la namna ya kuuzuia. Labda aliongea mleta mada hajaiweka
Ndio maana tunasisitiziwa tupime afya zetu mara kwa mara huo ugonjwa ni hatari sana
Ni hatari kwa usafiri wetu huu wa Dar es salaam wa mabasi ya mwendo kasi/daladala.
Kuna ULAZIMA KUWE NA VIPIMO KILA KITUONI ILI ABIRIA ALIOKUWA NA DALILI APANDE BAJAJI KUELEKEA HOSPITAL Badala ya kuingia ndani ya basi kuambukiza watu.
MKUU PALE magogoni sitisha ujenzi wa airport kule home pesa zinunue vipimo viweke kila mahali, upimaji uwe lazima vinginevyo tunaangamia baba, Ndege sio wengi wenye uwezo wa kuzipanda. Ikifanyika kampeni ya kutosha Gonjwa litaisha. Chondechonde ukifanya hv kula yangu 2020 iweke kwenye hesabu zako
 
Wazo zuri boss
 
Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema maambukizi ya ugonjwa wa Homa ya Ini yameongezeka mara mbili ya Virusi vya UKIMWI hivi nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari leo, Ijumaa Julai 28, Ummy amesema ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B) unaongoza kwa kuua Tanzania baada ya maambukizi kufikia asilimia 16, huku Virusi Vya UKIMWI, ikiwa ni asilimia 5.3.

Amesema ugonjwa huo huua taratibu ukilinganisha na magonjwa mengine kwa kuwa dalili zake huchukua muda mrefu kujulikana na kujitokeza wazi.

Amesema licha ya kwamba mpaka sasa hakuna takwimu halisi kutokana na watu kutokuwa na tabia za kupima afya zao, idadi ya wagonjwa wanaobainika kuwa na homa hiyo wengi huwa wamefikia hatua za mwisho za ugonjwa huo.

"Tunapata takwimu hizi kupitia uchangiaji wa damu, damu inayokutwa na Homa ya Ini ni nyingi zaidi ikilinganishwa na ile yenye Virusi vya UKIMWI,"amesema Ummy.

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom