VIRUSI vinavyoitafuna CCM-Rushwa na Ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIRUSI vinavyoitafuna CCM-Rushwa na Ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyami2010, Apr 9, 2011.

 1. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Virusi vinavyoitafuna ni CCM ni RUSHWA na UFISADI miongoni mwa WanaCCM.

  Ninaomba kueleza:

  Ukianzia ngazi ya shina, tawi, kata, wilaya, mkoa hadi taifa kuna watu wanaojifanya kuwa CCM ni yao. Mfano: Makatibu, wenyeviti na wajumbe wa kamati za siasa katika ngazi zote nilizotaja, asilimia kubwa ni wazee na watu wa makamo waliozoea kula rushwa. Ni watu wanao wakumbatia baadhi ya vigogo na hususani wabunge wakongwe (waliopitwa na wakati) ndani ya CCM na wanadhani bila wao hukuna CCM na Tanzania.

  Virusi hivi vilionekana rasmi kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka mwaka jana-2010. Katika CCM walijitokeza vijana wasomi, wenye damu changa na wenye mivuto kwa wananchi kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani. Katika sehemu zote nchini, vijana waliojitokez walikuwa ni NURU kwa CCM. Lakini kwa sababu ya makatibu, wajumbe wa kamati za siasa ngazi ya tawi, kata, wilaya, mkoa na taifa waliona ni vema wale rushwa na kuwatosa vijana. Wapenda rushwa na ufisadi hawa, waliona vijana ndani ya chama ni bure kwa vile hawana fedha lakini wakasahau kuwa vijana wana hoja, kisomo na ni damu changa na yenye mvuto kwa wananchi. CCM ilipoteza ushindi kwa asilimia kubwa, umaarufu na mvuto kwa watu. Ukweli, na BADO TU!

  Ushauri wangu kwa WanaCCM wote, hususani Mhe. Mwenyekiti Taifa: Kama kweli kuna nia mahususi ya kunusuru CCM, basi yafuatayo yafanyike:

  1. CCM kuanzia ngazi ya tawi, kata, wilaya, mkoa na taifa watafutwe makatibu wapya hususani miongoni mwa vijana wasomi na wenye mvuto.

  2. Wajumbe wa Kamati zote za siasa ngazi ya tawi, kata, wilaya, mkoa na taifa wapigwe chini na uitishwe uchaguzi mwingine wa kuwapata wajumbe wengine, hasa hasa vijana wasomi na wenye mvuto kwa watu.

  3. Uchaguzi wa 2012 kwa hali ya CCM ya sasa ni mbali sana, hivyo ninashauri katiba ya CCM irekebishwe na uitishwe uchaguzi mkuu kabla ya muda wake ili kunusuru janga linalonyemelea Chama na taifa.

  4. Mwenyekiti Taifa, lazima akubali kulaumiwa na hivyo afanye maamuzi magumu. Wale wote wanaotajwa kuwa vinara wa ufisadi (mafisadi na wanaounga mkono mafisadi hususani vijana) wanyang'anywe uanachama wa CCM. Sina sababu ya kuwataja maana wote wanafahamika na kundi la vijana wanaowaunga mkono.

  Ninajua reaction ya baadhi ya watu itakuwa ni kunitusi na kuona sina hoja kwa vile kipengele cha 4 kinapelekea kugusa penye shida, lakini ukweli unabaki pale pale.

  Ata Mzee Yusufu Makamba akiondoka CCM leo, mpasuko utaendelea kwa sababu chanzo chake ni kuanzia ngazi ya shina, tawi, kata, wilaya, mkoa hadi taifa. Rushwa na Ufisadi miongoni mwa wanaCCM ndiyo shida kubwa. Aslilimia kubwa ya wananchi wetu hususani vijjini bado wanaipenda CCM, lakini hawa wala Rushwa na Mafisadi ndiyo wanaowakatisha tamaa wananchi kote nchini. Hawa watu si wengi kiasi hicho. Kwanini watuharibie NCHI? Yanaendelea ni aibu kubwa kwa CHAMA na taifa kwa ujumla. Imagine, watu wameanza kuogopa na kuona aibu kutaja kuwa ni wanaCCM!!

  Hatua za haraka kunusuru hali hii ndani ya CCM lazima zifanyike. Macho na masikio yetu wananchi ni kwa Mwenyekiti Taifa-Mh. Dr. Jakaya Mrisho KIKWETE.
   
 2. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hali hii iendelee ili cdm tuchukue dola!
   
Loading...