Vipodozi visivyo salama na madhara yake - Sehemu ya Kwanza

Magnificient

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,162
705
VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA MADHARA YAKE
SEMINA HII IMEANDALIWA NA KULETWA KWAKO NA:
S&E HEALTH SOLUTIONS; WATAALAM NA WASHAURI WA AFYA, UREMBO NA VIPODOZI
ILALA BUNGONI, DAR ES SALAAM
0659 528 724 , 0784 082 847
IMG_20160605_085428.jpg IMG_20160605_085519.jpg IMG_20160605_085554.jpg

SEHEMU YA KWANZA
1.0 UTANGULIZI

Vipodozi visivyo salama ni vipodozi ambavyo vina kemikali zinadhuru au zinazoweza kuudhuru mwili na kuusababishia matatizo. Maana hii inaweza kuongezewa na kujumuisha vipodozi vyote ambavyo usalama wake unatia mashaka na vinaweza kuleta madhara kwa mtumiaji.

Hivyo hujumuisha :
-Vipodozi ambavyo havijasajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)
-Vipodozi vyenye viambata (kemikali) vya sumu na vilivyopigwa marufuku na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)
-Vipodozi ambavyo muda wake wa matumizi umeisha
-Vipodozi ambavyo havioneshi tarehe ya kuharibika (mwisho wa matumizi)
-Vipodozi ambavyo maelezo yake hayajaandikwa kwa Kiswahili au kiingereza

Vinaweza vikawa ni mafuta, losheni, krimu, pafyumu, poda na kadhalika.

1.1 VIAMBATA (KEMIKALI) VYA SUMU VILIVYOPIGWA MARUFUKU
Vingi vikiwa katika lugha ya kiingereza, hizi ndizo kemikali ambazo huongezewa katika vipodozi ili kufanikisha au kusaidia dhumuni lililolengwa kwa kipodozi husika. Viambato vyenye sumu vilivyopigwa marufuku ni:

1. Chloroquinone (Hydroquinone na kemikali zingine)
2. Steroids (Mifano ni Betamethasone, Beclomethasone, Hydrocortisone, Clobetasol, na Dexamethasone)
3. Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo
4. Chloroform
5. Bithionol
6. Hexachlorophene
7. Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo

8. Vinyl chloride
9. Zirconium na kemikali zinazotokana nayo
10. Methyelene chloride
11. Halogenated salicylanilides (Dimetabromsalan, Trimetabromsalan na Tetrabromsalan)
12. Chlorofluorocarbons (Kwenye pafyumu na deodorants)

1.2 JINSI YA KUJUA KAMA KIPODOZI KINA KIAMBATO (KEMIKALI) CHA SUMU KILICHOPIGWA MARUFUKU
Angalia kwenye lebo ya kipodozi chako sehemu waliyoandika Ingredients au Contents au neno jingine lolote lenye maana ya Vitu vilivyomo ndani. Hapo angalia kama kuna kiamabato au kemikali yoyote ambayo nimeiandika hapo juu kuanzia namba 1 mpaka 12.

Kama kuna kiambato au kemikali ambayo imepigwa marufuku basi jua kipodozi chako sio salama. Acha kukitumia mara moja na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA).

Kama hakuna kiambato cha sumu basi kipodozi chako kinaweza kuwa salama. Tatizo linakuja pale watengenezaji wanapofanya uhuni kwa kudanganya au kuficha na kuacha kuandika baadhi ya viambato vilivyomo ndani. Ambalo pia ni kosa kisheria.

MIFANO :

1. Sabuni ya JARIBU ina kiambato MERCURY. Sabuni hii sio salama, haifai kwa matumizi na imepigwa marufuku.

2. Losheni/krimu ya MEKAKO ina kiambato HYDROQUINONE. Losheni/krimu hizi sio salama, hazifai kwa matumizi na zimepigwa marufuku

3. Krimu za FAIR & LOVELY SUPER CREAM, VISIBLE DIFFERENCE CREAM, SKIN SUCCESS FADE CREAM, DEMOVATE NA DIPROSON CREAM zina viambata STEROIDS.
Krimu hizi sio salama kutumika kama vipodozi na zimepigwa marufuku
 
Asante sana kwa elimu hii. Sasa naomba kuelezwa bidhaa za Fair&white je zina madhara ama haziruhusiwi maana wameandika kwa kinafaransa.
 
Asante sana kwa elimu hii. Sasa naomba kuelezwa bidhaa za Fair&white je zina madhara ama haziruhusiwi maana wameandika kwa kinafaransa.
Kama imeandikwa kwa kifaransa tu bila kiingereza wala kiswahili kimsingi ilibidi isisajiliwe wala kuruhusiwa kwa matumizi hapa Tanzania. Endapo hauelewi lugha ya kifaransa ni vyema ukaacha kuitumia na kupata ushauri wa kipodozi cha kutumia kwa mahitaji yako
 
Kama imeandikwa kwa kifaransa tu bila kiingereza wala kiswahili kimsingi ilibidi isisajiliwe wala kuruhusiwa kwa matumizi hapa Tanzania. Endapo hauelewi lugha ya kifaransa ni vyema ukaacha kuitumia na kupata ushauri wa kipodozi cha kutumia kwa mahitaji yako
Mimi nafanya biashara ya vipodozi na mara nyingi nachukulia Kampala ama Mtukula, kinachonishangaza kwa nini Uganda na Congo wanauza tu pasipo kusumbuliwa kama hapo Tanzania? Hii imesababisha Watanzania wengi kufuata vipodozi nje ya nchi na huko Tanzania mmembaki kuvizia tu kukamata pasipo kudeal na sababu harisi ambayo ni technology yetu kwa kutengeza good cosmetics haipo. Ukifika Kampala utakuta hadi ma agent kama wa kampuni ya H Cosmetics wapo wakisupply na kumake a lot of money. Anyway asante kwa elimu lkn unaposema hadi waandike kwa kiswahili ama kiingereza ndipo isajiliwe hapo ni ngumu sana kwani vipodozi vizuri na quality viko chini ya viwanda vya wafaransa na wamewekeza sana Congo, Cameroon, Ivory Coast na kiasi Zambia
 
Back
Top Bottom