hahaha! Wallah siyaoni naona tu yakina Obama!!
Hahaha Kaunda suti bana nakumbuka nilikuwa nayo moja tu nayo ni kwaajili ya kanisani tu basi..nikitoka church naivua inaiweka kwenye sanduku la bati lenye dawa ya Mende Basi inanukiaje vizuri....
Dah nimekumbuka mbali kidogo aisee sijui miaka ya ngapi ile !! Kulikuwa na maflana yenye picha za wanamuziki wa kikongo kama BONGOMANI,BOZIBOZIANA,AWILO ,nilikuwa na la Bongomani aisee nilikuwa nalipenda balaa..yapo wapi nowdays ?...,........-.........,..... kulikuwa na mashati yanaitwa BAWAMA yana pesa pesa kibao ya ujiuji hayapo siku hizi.........haya ukija upande wa urembo sijui ndo madawa yalikuwa hayajaingia loh! Akina dada/mama walikuwa wanachoma nywele zao eti ndo relaxer haha! Usiombe wakati wa sikukuu !!................ Kwenye maharusi sasa biharusi alikuwa anavaa skuna na soksi mkononi ana gloves hahaha kweli tumetoka mbali!!.........kwenye vipaimara binti bila gauni ya mashelashela na soksi ndeefu bado hajatokelezea hahaha! Ule mtindo wakuweka blue mashati ya shule sijui kama siku hizi bado unaendelea eti uonekane msafi aisee...nikumbusheni na vingine.....
tabia hubadilika kulingana na mazingira..na mambo huchange pia kulingana na wakat..kipind hicho kina bongo man n.k ndo walikua historia duniani saiv wameshapotea wamekuja wengine ndo hivyo tena..ila zamani ni zamani haitakaa ijirudie...
Nywele hata mi nilichomwa kwenye kipaimara asee nililia walikataa kuniweka dawa wakanichoma.na gauni langu la shela acha kabisa
tabia hubadilika kulingana na mazingira..na mambo huchange pia kulingana na wakat..kipind hicho kina bongo man n.k ndo walikua historia duniani saiv wameshapotea wamekuja wengine ndo hivyo tena..ila zamani ni zamani haitakaa ijirudie...
hahahaha! Chini skuna ! Umenichekesha sana! Kuna picha hapa nikiziangalia nacheka mwenyewe!! Btw-kuna siku nilisema jamani sitaki kuweka dawa nikatafuta mtu anichome nywele wee kwani nimekaa nazo? Mbona nikanyoa mana nilinyeshewa mvua aisee! Kweli usasa ni usasa tu!!
Teh teh ila ilikuwa raha sana na mama yangu alikuwaga na kalikiti kichwani inang'aa mafuta ajabu
miye nshasahau hata majina ni kitambo! asante kwa correction!! Loh! Btw- Uliyavaa??
kweli lakini mana nakumbuka enzi zile hata miziki iliyokuwa inatamba ni ya kizaire!!