vipo vya kuagiza lakini hivi vimezidi

vipo vya kuagiza lakini hivi vimezidi

kidaganda

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2013
Posts
2,997
Reaction score
2,577
Watu bwana. Kila mji unaokwenda hawakosi cha kukuagiza.

Kama waenda Mbeya utasikia, "Tuletee maparachichi na mchele."

Ukienda Moshi unaagizwa, "Usisahau kutuletea kahawa."

Uendapo Dodoma utasikia, "Utuletee zabibu na karanga."

Ukienda Tabora wapo tu, "Pliiiiz utununulie asali huko."

Ukienda Morogoro wanaagiza, "Tuletee magimbi basi."

Kama waenda Bagamoyo waagizwa, "Mananasi ya kule matamu usisahau kutuletea."

Unapokwenda Tanga utasikia, "Tuletee machungwa jamani!"

Kama ni safari ya Songea, "Usisahau viazi vya Songea."

Unapokwenda Mtwara unaagizwa, "Tuletee korosho unaporudi."

Unapokwenda Kigoma, "Jamani rudi na mafuta ya mawese na migebuka."

Ukisema safari inaishia Singida wana wewe tu, "Basi utuletee mafuta ya alizeti."

Ukiwaambia unakwenda Mwanza wanaagiza, "Utuletee samaki sana sana Sato."

Kama waenda Bukoba hawachoki tu, "Tafadhali utuletee senene!"

Kasheshe sasa kama safari yako inaishia Iringa. Utasikia sasa, "Niletee mdada wa kazi jamani!"
 
Hii ya Iringa hiiiii Hahahahaaaaa nimecheka tu. ILA Wadada WA Iringa wakijanjaruka mmmgghhhh achana na hio habari
 
Kasheshe sasa kama safari yako inaishia Iringa. Utasikia sasa, "Niletee mdada wa kazi jamani!"

KWELI KASHESHE
 
Kasheshe sasa kama safari yako inaishia Iringa. Utasikia sasa, "Niletee mdada wa kazi jamani!"

KWELI KASHESHE

Unaweza kuniambia kwa ufupi sana kwanini unatumia ID hii?
 
beeee ndauli beee?? na kama waenda NJOMBE jee watakuagiza nini??
 
Ukitoka Iringa, niletee Kadada yake Chris Lukosi , teteteeeee 🙂
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom