Vipimo vya kichina katika kupima afya

Vipimo vya kichina katika kupima afya

Eberhard

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
1,151
Reaction score
809
Serikali ya CCM ni dhaifu mno? Tena ni dhaifu sana. Hapa tuangalie swala moja tu. Swala la vipimo vya kichina. Last wiki nilikutana na vipimo vya kichina vya barabarani. Katika vipimo hivyo mashine ya kompyuta huwekwa kisha yule anayepimwa hushika kifaha furani mkononi na mpimaji uanza kufatilia kipimo kile kila mahali kinapoenda kama kwenye moyo au kongosho au kichwani. Binafsi yangu kabla ya kupima nilihoji mambo mengi sana likiwamo swala zima la mionzi. Wakati napimwa kipimo kilipofika kichwani nilikihisi sasa kipo kichwani( kwenye ubongo).

Mwisho wa vipimo nikagundua kuwa yule jamaaa aliyekuwa ananipima hajui hata difinition ya biology. Maana alikuwa ananielezea kwa kubunibuni tu. Mara utakuwa na tatizo kwenye uzazi yaani utakuwa hanisi mara utakuwa na mbegu nyingi sana za kiume na mengine kibao. Kijana ambaye hata lugha ya kiingereza hajui. Nilijiona nipo kwenye maigizo.Binafsi yangu nimejiuliza maswali yafuatayo
Kwa nini serikali iruhusu vipimo kama hivi kuingia nchini?

Kwa nini wamekaa kimya huku wakijua wale wanaofanya huduma hiyo ya kupima wengi wao hata biology ya shule ya msingi hawaijuhi? Ni watanzania wangapi wataasirika na mionzi hiyo ya kichini kwa kurudia rudia kupima na vipimo hivyo bila kujua madhara yake tena bila ya ushahuri wa madaktari?

Je serikali hii inafikiria wananchi au wanawaza wizi tu?
Je hakina athari ya mionzi(Uv)?
Je tunayo serikali kweli au tunaowatu wanaofikiria kuiba tu?
 
Hawa viongozi wetu ukiachilia mbali wizi wao, pia wana very poor vision. Wengi waliovuka umri wa miaka 55 wanajiandaa ku-staafu na sio kuwajali/kuwasaidia wananchi.
Swala la huduma za afya ni muhimu sana kuwa genuine, haya mambo ya fake physicians, yanaweza kusababisha vifo ambavyo vingeweza kucheleweshwa.
 
Back
Top Bottom