Acha uoga wa kifikra ndugu, na tatizo hili la uoga ndio uwamaliza watu sana tena sana Afrika. Ishi kwa matumaini na kujiamini , wewe mwenye jamaa ambaye unasema vipimo vinamchanganya unaonekana kupanik sana, je huyo mhusika hali yake hipo vipi kwa sasa , kama wewe tuu hivi?hakuna ugonjwa mzuri Duniani hila siku zote ishi kwa matumaini na ukiamini kwamba hapa duniani tunapita tuu. Watu wanakufa kwa kujiminya chunusi tuu kesho unasikia marehemu alijiminya chunusi akafa. Kifupi kakutwa na HIV ajakutwa nao mshauri tuu kwamba aishi kwa matumaini katika maisha yake Duniani , anaweza kuwa na huo Ugonjwa na walio wazima wakatangulia mbele ya haki na wakamuacha yeye anadunda tuu Duniani. Tujiwekee kila siku sisi ni wagonjwa tule vizuri na kwa wakati unaopaswa , tufanye mazoezi ,na mambo mengine mengi tuu ya kukufanya. Usijutie kwamba utakufa utaicha dunia, Dunia ilikuwepo na itakuwepo. wamekufa mama zetu baba zetu , manabii, watume, na bado Dunia hipo tuu. Ushauri wangu kuanzia leo wewe na huyo mlengwa achane uoga wa kifikra , uoga ndio utazidi kumuumiza tuu . Je angekuwa kama mama mkwe wangu aliyeambiwa na Dokta kwamba kansa yake imeshamtafuna sana hivyo miezi Sita ya kuishi kwa yeye Duniani ni kama 8 % tuu lakini mama aliishi kwa kuamini Mungu akavunja miaka 3 sio miezi 6 kama Dokta alivyomwambia ,alikufa akiwa na umri wa miaka 64 , Achana na kumbeep beep Mungu na vipimo mara kwa mara.