mahirtwahir
JF-Expert Member
- Jan 12, 2013
- 614
- 322
snowhite kwa hili shairi mwanafunzi anaruhusiwa kumletea mwalimu wake zawadi ya kikuba?sijitie jitimai,kukosa kilo moyoni
tamasha yu kifuani,lipi jibu watakani
wabusu kwake pajini,kututega tujibu nini
jipe raha ya moyoni,tamasha nawe penzini
situtie kashdani ,lawama ukatutwika
mlopendana ni ninyi,utotoni mlikoweka
wenu wa kwenu ubani,moyoni ukabebeka
jipe raha ya moyoni ,tamasha nawe penzini
Mkatalie.
Kama anataka kukumbushia, wewe gegedana
Huwezi kujua, labda amekukumbuka
Kabla hujaendelea, unaweza kuniambia
Muda gani hamjaonana, hebu funguka
Kama wewe kweli unampenda, usilaze damu kumbushia
Haina haja ya kuumia, huku tunda unalitaka
Kitu gani bana, maisha mafupi kula bata
Eti Wewe ulimtoa bikira, haina haja ya kumkatalia
Wazazi kawaida, msamehe kwa yaliyotokea
Maisha ni kusameheana, huwezi jua
Pengine mama mtarajiwa, watoto atakuletea
Tena narudia, usithubutu kumkatalia
Hebu malizia, anajua kupika
Jiko limejileta, chukua jumla
Kabla wakware kummendea, utakuja jijutia
Nakutakia mafanikio mema, endelea kula raha za dunia
mkatalie moyoni ,zama zake zimepita
jiwekee tumaini,mwingine utampata
mwenye uzuri wa shani,huyo anatapatapa
usilambe matapishi,ving'aavyo vingalipo
anaomba samahani,jua amekosa soko
akuona wa thamani, aache vyake vituko
suraye haina soni,kawa kama mbwa koko
usilambe matapishi,ving'aavyo vingalipo
kama wataka tulizo,niko hapa nibaini
njoo nikupe liwazo, achana na huyo haini
kwangu hakuna mizozo, wazazi wala jirani
usilambe matapishi, ving'aavyo vingalipo
nafasi hii i wazi, japo ina washindaniUlionena ni kweli,inangia akilini
Kua alikua ghali,ila sasa hana soni
atafuta afadhali,japo kwa kichochoeoni
Hata anambie nini,sirejei matapishi
Mwanzo nembembeleza,kwa wangu umasikini
Hampa nisivyoweza,ili asinighaini
ndipo alipo nibeza,kuona sina thamani
Nafasi ulionipa,ninaitamani kweli
Ni vipi nitakupata,unipoze yangu hali
mkatalie moyoni ,zama zake zimepita
jiwekee tumaini,mwingine utampata
mwenye uzuri wa shani,huyo anatapatapa
usilambe matapishi,ving'aavyo vingalipo
kama wataka tulizo,niko hapa nibaini
njoo nikupe liwazo, achana na huyo haini
kwangu hakuna mizozo, wazazi wala jirani
usilambe matapishi, ving'aavyo vingalipo
Hapo dada umetisha jamaa ashindwe mwnyewe, Big up to you
Mkuu shukurani ya punda?, umepewa ushauriUlionena ni kweli,inangia akilini
Kua alikua ghali,ila sasa hana soni
atafuta afadhali,japo kwa kichochoeoni
Hata anambie nini,sirejei matapishi
Mwanzo nembembeleza,kwa wangu umasikini
Hampa nisivyoweza,ili asinighaini
ndipo alipo nibeza,kuona sina thamani
Nafasi ulionipa,ninaitamani kweli
Ni vipi nitakupata,unipoze yangu hali