Vipi naweza kumsaidia huyu mdogo wangu rafiki yangu wa karibu?

Salummjr

Member
Aug 19, 2018
25
6
Habari wana JF kwa muda mrefu nimekuwa nikiishi nae huyu rafiki angu kama mdogo wangu wa karibu sana ila jambo alilokuja kuniambia leo na kunambia nimpe ushauri kidogo nilisita na nikamwambia anipe mda nitamjibu.

Picha ipo hivi: Ni kijana wa miaka 22 - 25 ametokea kupendwa na msichana ambae ni mke wa mtu kwa miaka sita (6) sasa yupo kwenye ndoa, ni kwa muda sasa anaishi nae kwa siri bila ya mtu yeyote kutambua lengo lao ni kuja kuwa mke na mume japokuwa mwanamke yupo kwa mumewe kwa sasa.

Mahusiano yao yalianza pindi msichana alipokuja kumuelezea huyu kijana jinsi gani anateseka na ndoa yake, anasema kwamba mumewe hana huduma, anamdharau na kumdhalilisha hivyo akaamua kuanzisha mahusiano na kijana huyo.

Hadi sasa wapo katika mahusiano ila alichokuja kugundua yule kijana kuwa huyu msichana ana mahusiano mengine na mzee mmoja pale pale mtaani kwao.

Nahitaji kumsaidia kama mdogo wangu nini afanye.

Nimeandika kwa ufupi kama kuna maswali unaweza kuniuliza.
 
Yaan mwanaume ana mume anaemnyanyasa.

Yupo na mdogo wako na wanatafuta ndoa

Yupo na mahusiano na mzee moja.

Yaana mwanamke yupo 1in3 alafu kama tukimuita kahaba kuna watu watamtetea na kuamini ni kweli ndoa yake inamtesa..

MWANAMKE AKIKUELEZA ANAYOYAPITIA BASI JUA KINYUME CHAKE NDIO SAHIHI!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaan mwanaume ana mume anaemnyanyasa.

Yupo na mdogo wako na wanatafuta ndoa

Yupo na mahusiano na mzee moja.

Yaana mwanamke yupo 1in3 alafu kama tukimuita kahaba kuna watu watamtetea na kuamini ni kweli ndoa yake inamtesa..

MWANAMKE AKIKUELEZA ANAYOYAPITIA BASI JUA KINYUME CHAKE NDIO SAHIHI!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sio mdogo wangu wa damu bali ni rafiki tu na ninaishi nae kama mdogo wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama tayari ameshagundua kuwa huyo mwanamke ana mwanaume mwingine hapo hapo mtaani ambaye ni tofauti na mumewe
Anaendelea kuwa na huyo mwanamke ili iweje

Hadi hapo tayari huyo mwanamke amekwisha dhihirisha kuwa kuwa na mabwana wengi na kutoka nje ya ndoa yake hicho ndio kipaji chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukute mdogo wako anahongwa na mke wa mtu.
Shemeji yako anaenda kumkamua mzee wa watu halafu anapelekewa mdogo wako.


mama wawili
 
Mimi ndo uyo mzee .uyo mwanamke ali nambia ivyo ivyo ame kua akini penda toka yupo mtoto ivyo ana taka nmuoe

Dark Side
 
Back
Top Bottom