Freewine
JF-Expert Member
- Jan 7, 2018
- 257
- 212
Wazungu kwa miaka mingi sana wamekuwa wakinyonya serikali maskani za Afrika ikiwemo Tanzania bila kuona haya. Chanzo cha mzungu kuibia waafrka hakuji bahati mbaya ni mipango mathubuti iliyopangws na serikali zao kuhakikisha nchi maskani zinaendelea kuwa maskini.
Wazungu hawa hawajileti kwenye nchi yoyote bila kujua kuna kipi kizuri wanaenda kuvuna kwa wingi. Kwa sababu hawawezi kufika kwenye fursa moja kwa moja wanatumia viongozi wazawa kujiharalishia Neema ndani ya nchi hizi maskini.
Viongozi ndani ya nchi maskini wananeemeka kwa kuwapa wazungu hao utajiri wa nchi huku RAIA Wao wakibaki matopeni chakali kwa umaskini uliokithiri. Na hapo ndipo neno WAZUNGU walipoanzia kuitwa jina MABEBERU kwenye nchi hizi za kimaskini. Hii iliotokana na baadhi ya viongozi wazalendo na waaminifu kukataa kujihusisha na ulaghai huo unaofanywa na mataifa yenye nguvu.
Mahusiano bora baina ya nchi moja na nyingine ni jambo muhimu sana kwenye dunia hii Kwa sababu ndani ya nchi hizi kuna watu na lazima watu wote waishi kwa msingi ya utu na kuheshimiana. Ubaguzi wa aina yoyote unakatazwa na jamii zozote duniani kwa sababu dhambi ya ubaguzi na udhalilishaji hauishii kwa nao uliowabagua Bali husogea mpaka ndani kwako.
Wafirika tumekuwa tukilalamika sana juu ya Kuitwa NYANI kwenye nchi za wazungu, jambo huwakera wazungu wenyewe hata kufikia hatua ya kuwaadhibu mashabiki wa timu Fulani endapo itagundulika walifanya ubaguzi huo kwa mchezaji yoyote kutokea Afrika. Na baada ya adhabu huyo waafrika huwa tunafurahi kwamba haki imetendeka. Vipi kiongozi wa nchi anaposimama mbele ya media na kuitwa wazungu ni MABEBERU hivi Wao huwa wanajisikiaje?
(Ebu ona kwanza sifa za beberu, ni mbuzi dume ambaye anaharufu Kali sana, Silaa yake IPO kichwani na akitaka mapenzi badala ya mwanamke kulia lenyewe ndo linalia) hizi sifa sio nzuri ni matusi.
Wazungu wanafadhili hizi nchi za kimaskini mambo mengi mfano suala LA madawa ya ARVs na matibabu ya UKIMWI sio jambo LA mchezo kama serikali itatakiwa ilisimamie kwa asilimia 100. katika uliza uliza ndipo nikapata taarifa kuwa baadhi ya vituo vya afya havina ARVs za Watoto, Second line ARVs za wakubwa na pia kuna punguzo kubwa LA watumishi linaenda kutokea kuanzia Oct 2019 kutokana na mhisani kupunguza budget ya uendeshaji masuala us CTC. Sasa najiuliza au ndo beberu ameanza kuitingisha serikali hii au ni hisia tu.
Lakini Mimi sidhani kama kuna mzungu mbaya kama utaingia kwenye agreement na yenye huku una maarifa ya kutosha juu ya jambo Fulani. Masuala ya kuitana Mara sijui nyani, beberu au jiwe hayafai kabisa huo ni udhalilishaji wa watu wengine.
Tuwaheshimu wengine wakubwa kwa wadogo ili nasi tuheshimiwe