Kama kuna kazi muhimu sana wanayoweza kuifanya wakati mgumu huu; ni kuhakikisha kwamba kila tukio la mTanzania kupotea kwa sababu kasema mambo wasiyoyataka watawala, ni kuhakikisha kwamba matukio yote ya aina hiyo yanawekewa kumbukumbu ndani ya chama; na kila tukio linajulishwa kwa umma wa waTanzania.
Naomba sana kazi hii wasiipuuze hata kidogo.
Waweke utaratibu mzuri wa kuzipokea taarifa hizo na kuzisambaza kwenye vyombo; kama mitandao ili zisambae kuwafikia waTanzania.
Hii itakuwa ni pamoja na kuwaTambua wahanga hawa kwa juhudi wanazo fanya zilizo sababisha wao kuwekwa katika hali hiyo ngumu.
Hawa ni wapambanaji wa taifa letu, mchango wa juhudi zao katika ukombozi wa taifa hili ni lazima zihifadhiwe na kuenziwa baada ya ukombozi kupatikana.