Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,636
- 11,119
Kuna tatizo nililipata na kuligundua jana, baada ya kuona vipele vidogo kuzunguka kichwa cha umme; vikiwa havina usaha wala muwasho au maumivu.
Sababu kuu iliyopelekea hivi nahisi ni jambo lililotokea juzi, nilikuwa chooni nikijisaidia (choo tunatumia watu wengi) ni choo kisafi lakini naamini choo hata kiwe safi bado huwa kuna bacteria wanaishi. Sasa wakati najisaidia kopo lilianguka wakati najaribu kutoa maji kwenye ndoo, baada ya kuanguka maji yalinirukia mpaka maeneo ya uume, hatua ya kwanza nilijisafisha na maji na baada ya hapo nilioga na sabuni nikihofia kupata magonjwa.
Nilijipa muda kuona kama nitapata mabadiliko yoyote ktk afya yangu, kesho yake ambayo ndio jana nikapata vipele hivyo na kuwa na mabadiliko kwenye uume wangu.
Hatua ya kwanza nilifanya uchunguzi na kusoma makala mbalimbali ili kupata habari zozote, nilipitia uzi humu JF kuhusu Pearly penile papules ila nina hakika tatizo langu na hilo havina uwiano japokuwa hakuna tofauti vipele vyote ni vidogo kimuonekano.
Baada ya kuona ni tofauti leo nikaamua kwenda hospitali kujua zaidi tatizo ni nini. Nilienda hospitali na nilifanikiwa kuonana na daktari (mwanamke) nikamuelezea tatizo na jinsi vilivyo na mahali, akauliza kama kuna muwasho au maumivu wakati wa kukojoa na vyote hivyo sina.
Basi akanishauri nichukue dawa ya kupaka inaitwa CLOTRIMAZOLE CREAM BP 1% w/w (Cani-Masks) ambayo nimeambiwa nipake mara mbili kwa siku baada ya kuoga na kujikausha vizuri.
Nataka nijaribu kutumia tiba hii ila nataka kupata msaada zaidi hapa kama kuna mtu aliwahi pata tabu kama hii na tiba ipi alitumia.
Nilitamani leo ningekutana na daktari wa kiume ili aone kabisa tatizo ila sikufanikuwa maana sikupata muda wa kutembelea hospitali nyingine zaidi. Hospitali niliyotembelea nilikuta daktari mmoja tu wa kike, nilienda jioni sana baada ya kumaliza shuhuli za siku.
Sent using Jamii Forums mobile app